Nani kakisoma kitabu hiki? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani kakisoma kitabu hiki?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kautipe, May 6, 2011.

 1. k

  kautipe Member

  #1
  May 6, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Poleni sana na majukumu ya kila siku wana jamii, tafadhalini naomba sana msaada kwa yeyote ambaye amewahi kusoma kitabu kimoja kinachoitwa NDOA YANGU, NINGEJUA!

  Kwa mara ya kwanza, nilikiona kwa abiria mwenzangu miezi miwili iliyopita wakati naelekea Arusha. Kwa kweli kilinivutia sana hasa baada ya kusoma dondoo zake.

  Mwandishi wa kitabu hicho ambaye sijamfahamu, alifanya utafiti kujua kwa nini NDOA NYINGI HAZINA AMANI NA NYINGI ZINAVUNJIKA?

  Nilivutiwa zaidi na maswali yake: kwa mfano aliuliza (nadhani swali lake lililengwa kwa wale waliofunga ndoa)

  1. Kama ungejua mkeo au mumeo atakuwa na tabia alizonazo sasa, je ungekubali kufunga nae ndoa? swali hili na mengine yaliyomo ndani ya kitabu hicho ni ya msingi kwa wanandoa.

  Tatizo huku Arusha nimekitafuta sana sijakipata.

  Nisaidieni
   
 2. N

  Ndevu mbili JF-Expert Member

  #2
  May 6, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 382
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  umetafuta kwenye maduka gani hapo arusha?
  Anzia Kase bookshop!
   
 3. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #3
  May 6, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  kwa hivo umejiunga JF leo kwa ajili ya kuulizia anejua kitabu basi ama? umeingia mlango wa kukaribishwa ndugu? pipita kule tukufahamu kisha uje na mada yako. hata hivo karibu sana ingawa hujabisha hodi.watakaojua watakuhabarisha zaidi utakapo kipata.
   
 4. Utamaduni

  Utamaduni JF-Expert Member

  #4
  May 6, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 1,198
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  Hicho kitabu sio kipya,

  Jaribu kutafuta kwenye maduka ya KIKATOLIKI zaidi.

  Mwandishi wake anaitwa Misango (al maarufu MC MISANGO, anayepatikana katika kanisa katoliki parokia ya KIMARA DSM), niliwahi kuhudhuria mwaka juzi uzinduzi wa hicho kitabu katika kanisa katoliki mikocheni, kulikuwa na sherehe pale na nilialikwa na rafiki zangu.

  inawezekana ikawa havipatikani sana kwa sababu ya muda umepita na labda mwanshishi wake haja'print tena, ila kwa uhakika kama ukija Dar es Salaam pale kwenye duka la cathedral utakipata, nilisoma kidogo to me naona ni maswali ya kwaida tu,
   
 5. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #5
  May 6, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  mpigie mwandishi atajua vinapatikana wapi 0713235592
   
Loading...