Nani kaiona kesho!? Alikuwa Polisi sasa kondakta wa daladala

feyzal

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
6,803
12,666
MAISHA ni mapambano. Kuna kupanda na kushuka na Waswahili wana usemi unaosema ‘Kesho yako anaijua Mungu’.

Usemi huu unathibitishwa na Farahana Mwanjonde (40), ambaye alikuwa askari polisi na sasa ni utingo wa daladala. Nilivutiwa na muonekano wake na uchangamfu wake, hasa pale anapopishana na trafiki barabarani, ambapo huwa wanamchangamkia.

Siku niliyomhoji Farahana alinieleza kuwa aliwahi kuwa polisi na kwamba anapitia changamoto nyingi katika maisha.

Lakini, ukimuangalia tabasamu lake, huwezi kudhani anapitia magumu mengi. Sababu za kufukuzwa kazi Farahana anataja sababu iliyofanya afukuzwe kazi ni uzembe.

Anaeleza kuwa “mimi nilikuwa nalinda silaha, kuna siku kuna bastola ilipotea mikononi mwangu. Nikaulizwa ilipo na nilisema kweli sikufahamu ilipo. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya wakati huo alikuwa Suleiman Kova. Aliamuru niwekwe ‘lokapu’ kwa uzembe. Nilikaa ndani kwa siku tano kisha nikapandishwa mahakamani. Ile kesi iliendeshwa kwa siku kadhaa na hukumu ilipotoka nilishindwa, na hukumu ilikuwa na mambo mawili, ama nifungwe miaka mitano au nifukuzwe kazi.

Nikasaini hati ya kufukuzwa kazi. Kuanzia hapo maisha yangu yalibadilika na nikaanza kupoteza mwelekeo. Wakati kesi ile ilipokuwa ikiendelea, baba yangu alirukwa na akili akawa kichaa wa kuokota makopo na baadaye akafariki. Kuanzia hapo nikawa sina msaada wowote, kwani yeye ndio alikuwa tegemeo langu.”

Ageukia kuuza yeboyebo

Anasema baada ya kufukuzwa kazi na kumpoteza baba yake, maisha yake yalikuwa magumu sana. Hakujua anzie wapi. Hata hivyo, baadaye alipata mtaji na kuanza kuuza ndala maarufu kama yeboyebo maeneo ya Vingunguti.

Huko alikimbizana na mgambo wa jiji, ambao walikuwa wakikamata machinga. Wakati huo mume wake wa ndoa, alikuwa akifanya kazi Kiwanda cha Saruji Mbeya.

“Unajua niliolewa mwaka 2000 mara tu baada ya kumaliza Chuo cha Polisi Moshi (CCP). Nilipaswa kukaa miaka mitatu ndipo niolewe, lakini nilipata ujauzito wa mtoto wangu wa kwanza, ikabidi tufunge ndoa. Mume wangu baba yake alikuwa ni askari, wao pia walikuwa wakiishi kambini na tulifahamiana huko,” anasema.

Waswahili wana msemo usemao ‘Mchumba hasomeshwi’. Msemo huo pia ni mwiba kwa Farahana, ambaye anasema ‘Mume pia hasomeshwi’ kwani alijinyima na kumsomesha mume wake. Lakini, anasema baada ya kuhitimu, mume huyo alimuacha kwenye mataa. Vijana wa zamani wanasema aliachwa solemba

“Nilipokuwa nafanya biashara ya yeboyebo, nilipata fedha sana na maisha yakawa mazuri. Nikamshauri mume wangu arudi chuo kujiendeleza kielimu. Nilimtafutia Chuo cha Kilimo Uyole. Nilimlipia ada kwa miaka miwili, lakini alipomaliza tu chuo na kupata kazi akaniacha. Hakunijali mimi wala watoto wetu, aliniona sina thamani tena.

“Baada ya kuachwa na mume wangu, nikahamia rasmi Dar es Salaam na watoto wangu. Tangu wakati huo nimekuwa nihangaika peke yangu na watoto. Nikawa nafanya biashara zangu kwenye minada ya Tegeta, Bunju, Makumbusho na msingi wangu ukawa mkubwa. Nikawa naenda mikoani, naning’inia kwenye malori naenda Iringa kwenye minada mikubwa ya ng’ombe kama Pawaga, Kiwele, Mafinga na Ifunda na wakati wa Nane Nane naenda Uyole Mbeya. Pia nilikuwa naenda Dodoma na Kibaigwa nauza minadani kisha narudi Dar.

Maisha yangu yalikuwa mazuri tu, nikanunua pikipiki mbili za biashara. Niliweza kumudu maisha yangu na wanangu na walisoma vizuri,” anasema.

Farahana anasema alikuwa amepanga kwenye nyumba moja maeneo ya Kiwalani Kwa Gude Dar es Salaam. Katika maeneo hayo walimfahamu kwa jina la ‘Bosi Mtoto’ kutokana na kuwa na uwezo kifedha.

Aliishi alivyotaka na alikuwa anakunywa anavyotaka. Katika mitaa hiyo mtu aliyetaka kwenda kwake, alikuwa akiuliza tu kwa ‘Bosi Mtoto’ anapelekwa mpaka nyumbani kwake (Farahana). Lakini, alipata majaribio ambayo yamesababisha aishi maisha hayo anayoishi.

Anguko lake Farahana anasema alifanya alichopenda na hakuwa na mpango na mwanaume yoyote. Lakini kuna siku baba mwenye nyumba, aliomba amuazime Sh 15,000 na alipomrudishia, alimrudishia fedha za mazingara bila yeye (Farahana) kufahamu.

“Nilienda Karume kununua belo la viatu na nguo nipeleke Iringa. Mkosi ulianzia Chalinze. Nilipata ajali, nikaumia vibaya maeneo ya usoni na kushonwa nyuzi tatu. Sikukata tamaa nikaendelea na safari hadi Iringa.

Nilining’inia kwenye lori mpaka Iringa mnada wa Pawaga. Kulikuwa hakuna mtu wa kuniambia habari gani. Mzigo sikuuza hata kidogo. Wiki nzima nilikaa kule nikiwa nakula na kulala hoteli. Nikaenda mnada wa Kilolo nako sikuuuza. Wiki mbili sikuuza chochote. Ilibidi niuze mzigo kwa bei ya hasara.

Iliniumiza sana roho kama binadamu, niliumia kwa vile nilipata hasara na mtaji wangu ulikata. Nikarudi Dar es Salaam. Nilipoingia tu nyumbani baba mwenye nyumba akanidaka juu juu na kunihoji vipi biashara? Nikamwambia mbaya.

Aliangua kicheko kikubwa na kusema mbaya tena. Haaaaa! Sikuelewa maana ya kicheko chake. Kwa jinsi alivyocheka ni kama kuna kitu alikuwa anakifahamu. Nilikwazika sana. Sikusema kitu, nikaingia ndani kwangu,” anasema.

Asubuhi alipokuwa anafagia uwanja, alikutana na hirizi na vikaratasi vingine vimeandikwa maneno ya Kiarabu. Aliwaita wapangaji wenzake kuwaonesha. Alichukua mafuta ya taa akamwagia na kuvichoma moto vikaratasi na hirizi hiyo. B

aada ya hapo mambo yake yalizidi kuwa mabaya. Alifilisika na ilifikia mahali alikosa fedha za kununua unga wa kukoroga uji. Farahana anasema maisha yaliporomoka.

Alikuwa na pikipiki mbili za biashara, ambapo dereva wa bodaboda moja alipigwa risasi na pikipiki ikakamatwa na ikahusishwa kufanya ujambazi. Ilishikiliwa Kituo cha Polisi Buguruni. Alikwenda na vielelezo vyote alivyonunulia pikipiki yake.

Alifuatilia sana pikipiki hiyo, lakini hakufanikiwa kurudishiwa mpaka leo. “Pikipiki yangu nyingine kijana niliandikishiana naye mkataba, lakini alitoroka na pikipiki kwenda Tanga na mpaka leo sijamtia machoni. Nimetembea na RB mpaka nimechoka. Maisha yangu yaliporomoka sana. Nilihama nyumba niliyokua nakaa. Nikahangaika nikapata mtaji wa shilingi 50,000 nikaingia Soko la Karume na kuanza kununua nguo kupeleka kwenye minada Kisarawe, Manerumango, Chole na Msanga. Nilikuwa nauza kisha nanunua viroba vya mkaa narudi navyo mjini nauza, maisha yanaenda,” anaeleza.

Akutana na dereva wa daladala

Farahana anasema kuna siku alipanda daladala, akapata siti ya mbele kwa dereva. Dereva huyo alivunja ukimya na kumweleza hana mke na ana mpango wa kuishi naye (Farahana).

Alisema pia kuwa hana nia ya kumchezea. Kwa vile na yeye alikuwa hana mtu kwa kipindi kirefu na maisha yamempiga, aliamua kumkubali dreva huyo na wakaanzisha mahusiano.

“Akaja kwangu, tukawa tunaishi kama mke na mume. Hata hivyo, tabia zake hazikuniridhisha, kwani alikuwa mtu wa kutangatanga, leo yupo kwangu kesho yupo kwa mwanamke mwingine. Siku moja tuligombana sana.

Akachukua TV yangu akaivunja. Nikamtimua nyumbani kwangu. Siku moja nikamkuta amekaa Gongolamboto Mwisho wa Lami ana mawazo sana, anatia huruma. Nikamuita Papaa turudi nyumbani. Akasema wewe si ulininyanyasa?.

Nikamwambia wewe ulikuwa unanidanganya na kuna wakati uliaga unaenda Arusha kwenye msiba wa wanafunzi wa Shule ya Lucky Vincent lakini hukwenda. Sikumuona kwa siku tatu kumbe alikuwa kwa mwanamke mwingine. Basi tukazungumza yakaisha, akarudi nyumbani,” anasema.

Farahana anasema mwanaume huyo, ndiye aliyemuingiza kwenye kazi ya ukondakta. Alianza kumfundisha ukondakta mara tu baada ya kurudiana. Mwanzoni ilikuwa kazi ngumu sana kwake, kwani watu walikuwa wakimshangaa mno na kumuuliza kama ataweza ; na yeye aliwajibu kuwa ataweza.

“Kazi yoyote ya kuingiza kipato nafanya mradi tu isiwe ya kuuza baa au mwili. Kazi hii ndiyo inayonilisha mimi na familia yangu, maana mume wangu hana daladala ya kufanyia kazi muda mrefu, hivyo yupo tu. Wakati mambo yangu yakiwa mazuri, nilifanikiwa kujenga nyumba. Tunaishi naye katika nyumba hiyo pamoja na wanangu. Mwanangu wa kike alishamaliza shule na wa kiume yupo kidato cha nne,” anasema.

Kwa mujibu wa Farahana, mwanawe wa kwanza alipomaliza kidato cha nne, hakuwa na mtu wa kumuendeleza shule. Kuna mwanaume mmoja alijitokeza siku moja na kudai anataka kumuoa. Hata hivyo, kuna siku binti yake huyo alimpigia simu na kumueleza anajuta kuolewa na kuomba akamchukue huko aliko, kwani anateseka na anataka apelekwe shule.

“Nikamuuliza nikupeleke shule mume wako yupo wapi? Akasema tangu ameolewa miezi sita mwanaume hajampa haki yake ya ndoa. Akasema mama sijawahi kukutana na mume badala yake nimegeuzwa mfanyakazi wa ndani na mama mkwe wake.

Alifanyishwa kazi kama punda na matusi juu. Nikaita washenga, wazee wa kanisa na mchungaji, tukazungumza suala hilo ili mwanangu arudi nyumbani, na kweli alirudi,” anasema.

Farahana anasema mara mara baada ya mwanawe kurudi nyumbani, aliumwa ugonjwa wa kuchanganyikiwa, akawa kama kichaa. Ilimbidi Farahana ahangaike kumuguza. Majirani walimueleza ampeleke kwenye maombi katika Kanisa la Mlima Moto la Mama Lwakatare na kweli alifanya hivyo.

Alala madhabahuni, ‘vifungo’ vyafunguka

Anasema anakumbuka Desemba mwaka juzi, alienda madhabauni akalia sana na kumuambia Mungu, “Nimekukosea nini, kwa nini ni mimi tu ndio napata majaribu haya. Nililia kwa uchungu, nililala madhabauni pale siku tatu.

Nilifunga bila kula wala kunywa, nikasali sana na kumlilia Mungu wangu. Nashukuru mwanangu alipona na baada ya hapo maisha yangu yakaendelea. Vile nikaona vifungo vimefunguka. Nikifanya deiwaka kama hivi napiga debe naingiza siku. Imenisaidia kuweza kujimudu kimaisha.

Natoa fungu la kumi kanisani kila mwezi, ndio linaloniokoa mimi mpaka leo. Mama huyo anasema kuna mwanaume mwingine, alijitokeza kumchumbia mtoto wake.

Alieleza nia yake ya kutaka kumuoa binti huyo. Farahana alimueleza ukweli binti huyo kuwa alishawahi kuoelewa na mengine yote, hivyo aje na wazee wake na barua. Mtu huyo alikwenda na wajomba zake na walipewa masharti kuwa kabla ya kuleta barua, lazima kupima.

Kweli walienda kupima. Mwanaume huyo aliulizwa mara tatu kama ana mke, akasema hana. Walifunga ndoa katika Kanisa la Baptisti na kisha walifanya sherehe ndogo.

Baada ya siku tatu, mwanaume huyo aliondoka kwenda Tabora na alimuachia binti huyo Sh 2,000.

“Mwanangu akanipigia simu anaomba fedha ya kula. Nikamuliza unaomba fedha mumeo yupo wapi? Akasema amesafiri ameenda Tabora kaniachia shilingi 2,000 tu.

Mimi wakati huo nilikuwa nafanya ruti za Gerezani – Machimbo, nikifika Machimbo nilikuwa nampigia simu nampa shilingi 5,000 ya kula kila siku. Baadaye nikaona bora arudi nyumbani hadi mumewe atakaporudi. Nikamrudisha nyumbani, akakaa miezi miwili ndio mumewe akarudi na kusema mama asante kwa kunitunzia mke.

“Nilimwambia mwanangu una cheti chako cha kidato cha nne, nenda katafute ajira, na kweli alipata Kituo cha Mafuta cha Victoria. Baadaye mumewe aliporudi akamwambia hataki afanye kazi. Ukawa mzozo mkubwa. Baadae simu ya mwanaume ikaita, mwanangu alipoipokea alisikia sauti ya mwanamke inamwambia nipe Baba Rebeka niongee naye.

Akamuliza Baba Rebeka? Baba Rebeka ndio nani, mimi simjui?. Akasema hiyo namba ni ya mume wangu na mimi ndio mkewe. Mwanangu akasema mbona hata mimi ni mume wangu na hana mke wala mtoto. Yule mama akasisitiza kuwa ni mumewe. Basi mwanangu akamuuliza mumewe kama anamfahamu mama Rebeka, yeye akamwambia achane na hayo mambo. Mwanangu alichanganyikiwa sana,” anasema.

Farahana anasema mwanawe alirudi nyumbani, akamwambia mume wake ameoa na alimuonesha namba ya mke huyo mwingine. Mwanae alisema alimpigia simu mwanamke huyo, ambapo aliipokea na alipomuuliza alilia sana na akasema huyo ni mumewe na amezaa naye watoto wanne.

Kwamba kwa sasa ana mtoto wa nne mchanga wa mwezi mmoja tu. Kuna siku walifanya kikao, ambapo mwanaume huyo alipoulizwa kuhusu mtoto wa Farahana , alimkataa na kumkana binti huyo.

Hata wajomba zake walikana kuleta mahari. Ndipo mwanangu alibeba vitu vyake vyote na kurudi nyumbani. Baada ya siku chache mwanaume alikuja nyumbani, kuomba warudiane na binti huyo.

Farahana anasema alimtimua kama mwizi, maana alijua lengo lake lilikuwa kumchezea binti huyo. Farahana anasema mwanawe wa kiume yupo kidato cha nne na siku zote humuelekeza asome kwa bidii, kwa kuangalia maisha ambayo wanayoishi.

Changamoto zinazomkabili Anataja changamoto anazopata ni pamoja na kudharauliwa na baadhi ya abiria na kutukanwa. “Ni vigumu kupata gari la kufanyia kazi iwapo wewe ni mwanamke. Wanawake hufanya bidii mara tatu zaidi ndipo wapate kazi.

Makondakta wa kike katika daladala tunapitia mengi. Tunadhalilishwa kimapenzi na wengi tudhaniwa kuwa ni makahaba au watu walioshindikana katika familia. Jamii haitutazami kwa jicho zuri. Baadhi ya abiria wa kiume hukataa kulipa nauli na tunapowakabili huwa wanatutusi kwa maneno makali ya kashfa.

Wakati mwingine hutushambulia. Mimi kuna abiria wa kiume alishawahi kunisukumiza na kuniumiza. Unaona hili kovu mkononi?” anasema na kuonesha mkono wake wenye kovu kubwa. Anasema abiria aliyemfanyia hivyo alimpeleka polisi, lakini aliachiliwa na kesi ikaisha na hakulipwa fidia.

Ndoto yake Farahana anasema amejifunza kuendesha gari na kwamba ndoto yake ni kuendesha magari ya masafa marefu.

Ana leseni lakini bado hajafanikiwa kupata kazi katika kampuni ya kueleweka. Anasema mume wake anatamani awe dereva wa daladala jijini Dar es Salaam, lakini vizingiti vya hapa na pale anakutana navyo Fallana vinazuia ndoto yake hiyo. Kauli ya mumewe Mume wake anasema “Mimi ndio nimemuingiza kwenye kazi ya daladala.

Nilimwambia ajishikize, si unajua changamoto za maisha?. Hamuwezi kukaa wote nyumbani mnaangaliana. Lazima kupambana. Najua anapambana na vishawishi kibao. Kinachotakiwa ni yeye tu kuangalia atayashinda vipi. Mtu mzima hachungwi.”

Historia Yake Farahana Mwanjonde alizaliwa Mbeya mwaka 1980. Alisoma darasa la kwanza hadi la tano katika Shule ya Msingi Kiabakari iliyokuwa katika kambi ya Jeshi la Wananchi Musoma kisha alihamishiwa Shinyanga, ambako alihitimu darasa la saba mwaka 1995.

Alifaulu na kujiunga na Shule ya Sekondari ya Shycom, ambako alisoma kidato cha kwanza hadi mwaka 1999 alipohitimu kidato cha nne.

Alichaguliwa kwenda kozi ya uaskari polisi kwa miezi sita katika Chuo cha Polisi (CCP) na alipohitimu mwaka 2000 alipangiwa Kituo cha Musoma.

Alikaa Musoma kwa miaka kadhaa, lakini baadaye alihamishwa Mbeya, ambako alitumikia jeshi miaka mitano mpaka mwaka 2005 alipofukuzwa kazi kutokana na upotevu wa silaha.

Screenshot_20200316-135115_1.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MAISHA ni mapambano. Kuna kupanda na kushuka na Waswahili wana usemi unaosema ‘Kesho yako anaijua Mungu’.

Usemi huu unathibitishwa na Farahana Mwanjonde (40), ambaye alikuwa askari polisi na sasa ni utingo wa daladala. Nilivutiwa na muonekano wake na uchangamfu wake, hasa pale anapopishana na trafiki barabarani, ambapo huwa wanamchangamkia.

Siku niliyomhoji Farahana alinieleza kuwa aliwahi kuwa polisi na kwamba anapitia changamoto nyingi katika maisha.

Lakini, ukimuangalia tabasamu lake, huwezi kudhani anapitia magumu mengi. Sababu za kufukuzwa kazi Farahana anataja sababu iliyofanya afukuzwe kazi ni uzembe.

Anaeleza kuwa “mimi nilikuwa nalinda silaha, kuna siku kuna bastola ilipotea mikononi mwangu. Nikaulizwa ilipo na nilisema kweli sikufahamu ilipo. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya wakati huo alikuwa Suleiman Kova. Aliamuru niwekwe ‘lokapu’ kwa uzembe. Nilikaa ndani kwa siku tano kisha nikapandishwa mahakamani. Ile kesi iliendeshwa kwa siku kadhaa na hukumu ilipotoka nilishindwa, na hukumu ilikuwa na mambo mawili, ama nifungwe miaka mitano au nifukuzwe kazi.

Nikasaini hati ya kufukuzwa kazi. Kuanzia hapo maisha yangu yalibadilika na nikaanza kupoteza mwelekeo. Wakati kesi ile ilipokuwa ikiendelea, baba yangu alirukwa na akili akawa kichaa wa kuokota makopo na baadaye akafariki. Kuanzia hapo nikawa sina msaada wowote, kwani yeye ndio alikuwa tegemeo langu.”

Ageukia kuuza yeboyebo

Anasema baada ya kufukuzwa kazi na kumpoteza baba yake, maisha yake yalikuwa magumu sana. Hakujua anzie wapi. Hata hivyo, baadaye alipata mtaji na kuanza kuuza ndala maarufu kama yeboyebo maeneo ya Vingunguti.

Huko alikimbizana na mgambo wa jiji, ambao walikuwa wakikamata machinga. Wakati huo mume wake wa ndoa, alikuwa akifanya kazi Kiwanda cha Saruji Mbeya.

“Unajua niliolewa mwaka 2000 mara tu baada ya kumaliza Chuo cha Polisi Moshi (CCP). Nilipaswa kukaa miaka mitatu ndipo niolewe, lakini nilipata ujauzito wa mtoto wangu wa kwanza, ikabidi tufunge ndoa. Mume wangu baba yake alikuwa ni askari, wao pia walikuwa wakiishi kambini na tulifahamiana huko,” anasema.

Waswahili wana msemo usemao ‘Mchumba hasomeshwi’. Msemo huo pia ni mwiba kwa Farahana, ambaye anasema ‘Mume pia hasomeshwi’ kwani alijinyima na kumsomesha mume wake. Lakini, anasema baada ya kuhitimu, mume huyo alimuacha kwenye mataa. Vijana wa zamani wanasema aliachwa solemba

“Nilipokuwa nafanya biashara ya yeboyebo, nilipata fedha sana na maisha yakawa mazuri. Nikamshauri mume wangu arudi chuo kujiendeleza kielimu. Nilimtafutia Chuo cha Kilimo Uyole. Nilimlipia ada kwa miaka miwili, lakini alipomaliza tu chuo na kupata kazi akaniacha. Hakunijali mimi wala watoto wetu, aliniona sina thamani tena.

“Baada ya kuachwa na mume wangu, nikahamia rasmi Dar es Salaam na watoto wangu. Tangu wakati huo nimekuwa nihangaika peke yangu na watoto. Nikawa nafanya biashara zangu kwenye minada ya Tegeta, Bunju, Makumbusho na msingi wangu ukawa mkubwa. Nikawa naenda mikoani, naning’inia kwenye malori naenda Iringa kwenye minada mikubwa ya ng’ombe kama Pawaga, Kiwele, Mafinga na Ifunda na wakati wa Nane Nane naenda Uyole Mbeya. Pia nilikuwa naenda Dodoma na Kibaigwa nauza minadani kisha narudi Dar. M

aisha yangu yalikuwa mazuri tu, nikanunua pikipiki mbili za biashara. Niliweza kumudu maisha yangu na wanangu na walisoma vizuri,” anasema.

Farahana anasema alikuwa amepanga kwenye nyumba moja maeneo ya Kiwalani Kwa Gude Dar es Salaam. Katika maeneo hayo walimfahamu kwa jina la ‘Bosi Mtoto’ kutokana na kuwa na uwezo kifedha.

Aliishi alivyotaka na alikuwa anakunywa anavyotaka. Katika mitaa hiyo mtu aliyetaka kwenda kwake, alikuwa akiuliza tu kwa ‘Bosi Mtoto’ anapelekwa mpaka nyumbani kwake (Farahana). Lakini, alipata majaribio ambayo yamesababisha aishi maisha hayo anayoishi.

Anguko lake Farahana anasema alifanya alichopenda na hakuwa na mpango na mwanaume yoyote. Lakini kuna siku baba mwenye nyumba, aliomba amuazime Sh 15,000 na alipomrudishia, alimrudishia fedha za mazingara bila yeye (Farahana) kufahamu.

“Nilienda Karume kununua belo la viatu na nguo nipeleke Iringa. Mkosi ulianzia Chalinze. Nilipata ajali, nikaumia vibaya maeneo ya usoni na kushonwa nyuzi tatu. Sikukata tamaa nikaendelea na safari hadi Iringa.

Nilining’inia kwenye lori mpaka Iringa mnada wa Pawaga. Kulikuwa hakuna mtu wa kuniambia habari gani. Mzigo sikuuza hata kidogo. Wiki nzima nilikaa kule nikiwa nakula na kulala hoteli. Nikaenda mnada wa Kilolo nako sikuuuza. Wiki mbili sikuuza chochote. Ilibidi niuze mzigo kwa bei ya hasara.

Iliniumiza sana roho kama binadamu, niliumia kwa vile nilipata hasara na mtaji wangu ulikata. Nikarudi Dar es Salaam. Nilipoingia tu nyumbani baba mwenye nyumba akanidaka juu juu na kunihoji vipi biashara? Nikamwambia mbaya.

Aliangua kicheko kikubwa na kusema mbaya tena. Haaaaa! Sikuelewa maana ya kicheko chake. Kwa jinsi alivyocheka ni kama kuna kitu alikuwa anakifahamu. Nilikwazika sana. Sikusema kitu, nikaingia ndani kwangu,” anasema.

Asubuhi alipokuwa anafagia uwanja, alikutana na hirizi na vikaratasi vingine vimeandikwa maneno ya Kiarabu. Aliwaita wapangaji wenzake kuwaonesha. Alichukua mafuta ya taa akamwagia na kuvichoma moto vikaratasi na hirizi hiyo. B

aada ya hapo mambo yake yalizidi kuwa mabaya. Alifilisika na ilifikia mahali alikosa fedha za kununua unga wa kukoroga uji. Farahana anasema maisha yaliporomoka.

Alikuwa na pikipiki mbili za biashara, ambapo dereva wa bodaboda moja alipigwa risasi na pikipiki ikakamatwa na ikahusishwa kufanya ujambazi. Ilishikiliwa Kituo cha Polisi Buguruni. Alikwenda na vielelezo vyote alivyonunulia pikipiki yake.

Alifuatilia sana pikipiki hiyo, lakini hakufanikiwa kurudishiwa mpaka leo. “Pikipiki yangu nyingine kijana niliandikishiana naye mkataba, lakini alitoroka na pikipiki kwenda Tanga na mpaka leo sijamtia machoni. Nimetembea na RB mpaka nimechoka. Maisha yangu yaliporomoka sana. Nilihama nyumba niliyokua nakaa. Nikahangaika nikapata mtaji wa shilingi 50,000 nikaingia Soko la Karume na kuanza kununua nguo kupeleka kwenye minada Kisarawe, Manerumango, Chole na Msanga. Nilikuwa nauza kisha nanunua viroba vya mkaa narudi navyo mjini nauza, maisha yanaenda,” anaeleza.

Akutana na dereva wa daladala

Farahana anasema kuna siku alipanda daladala, akapata siti ya mbele kwa dereva. Dereva huyo alivunja ukimya na kumweleza hana mke na ana mpango wa kuishi naye (Farahana).

Alisema pia kuwa hana nia ya kumchezea. Kwa vile na yeye alikuwa hana mtu kwa kipindi kirefu na maisha yamempiga, aliamua kumkubali dreva huyo na wakaanzisha mahusiano.

“Akaja kwangu, tukawa tunaishi kama mke na mume. Hata hivyo, tabia zake hazikuniridhisha, kwani alikuwa mtu wa kutangatanga, leo yupo kwangu kesho yupo kwa mwanamke mwingine. Siku moja tuligombana sana.

Akachukua TV yangu akaivunja. Nikamtimua nyumbani kwangu. Siku moja nikamkuta amekaa Gongolamboto Mwisho wa Lami ana mawazo sana, anatia huruma. Nikamuita Papaa turudi nyumbani. Akasema wewe si ulininyanyasa?.

Nikamwambia wewe ulikuwa unanidanganya na kuna wakati uliaga unaenda Arusha kwenye msiba wa wanafunzi wa Shule ya Lucky Vincent lakini hukwenda. Sikumuona kwa siku tatu kumbe alikuwa kwa mwanamke mwingine. Basi tukazungumza yakaisha, akarudi nyumbani,” anasema.

Farahana anasema mwanaume huyo, ndiye aliyemuingiza kwenye kazi ya ukondakta. Alianza kumfundisha ukondakta mara tu baada ya kurudiana. Mwanzoni ilikuwa kazi ngumu sana kwake, kwani watu walikuwa wakimshangaa mno na kumuuliza kama ataweza ; na yeye aliwajibu kuwa ataweza.

“Kazi yoyote ya kuingiza kipato nafanya mradi tu isiwe ya kuuza baa au mwili. Kazi hii ndiyo inayonilisha mimi na familia yangu, maana mume wangu hana daladala ya kufanyia kazi muda mrefu, hivyo yupo tu. Wakati mambo yangu yakiwa mazuri, nilifanikiwa kujenga nyumba. Tunaishi naye katika nyumba hiyo pamoja na wanangu. Mwanangu wa kike alishamaliza shule na wa kiume yupo kidato cha nne,” anasema.

Kwa mujibu wa Farahana, mwanawe wa kwanza alipomaliza kidato cha nne, hakuwa na mtu wa kumuendeleza shule. Kuna mwanaume mmoja alijitokeza siku moja na kudai anataka kumuoa. Hata hivyo, kuna siku binti yake huyo alimpigia simu na kumueleza anajuta kuolewa na kuomba akamchukue huko aliko, kwani anateseka na anataka apelekwe shule.

“Nikamuuliza nikupeleke shule mume wako yupo wapi? Akasema tangu ameolewa miezi sita mwanaume hajampa haki yake ya ndoa. Akasema mama sijawahi kukutana na mume badala yake nimegeuzwa mfanyakazi wa ndani na mama mkwe wake.

Alifanyishwa kazi kama punda na matusi juu. Nikaita washenga, wazee wa kanisa na mchungaji, tukazungumza suala hilo ili mwanangu arudi nyumbani, na kweli alirudi,” anasema.

Farahana anasema mara mara baada ya mwanawe kurudi nyumbani, aliumwa ugonjwa wa kuchanganyikiwa, akawa kama kichaa. Ilimbidi Farahana ahangaike kumuguza. Majirani walimueleza ampeleke kwenye maombi katika Kanisa la Mlima Moto la Mama Lwakatare na kweli alifanya hivyo.

Alala madhabahuni, ‘vifungo’ vyafunguka

Anasema anakumbuka Desemba mwaka juzi, alienda madhabauni akalia sana na kumuambia Mungu, “Nimekukosea nini, kwa nini ni mimi tu ndio napata majaribu haya. Nililia kwa uchungu, nililala madhabauni pale siku tatu.

Nilifunga bila kula wala kunywa, nikasali sana na kumlilia Mungu wangu. Nashukuru mwanangu alipona na baada ya hapo maisha yangu yakaendelea. Vile nikaona vifungo vimefunguka. Nikifanya deiwaka kama hivi napiga debe naingiza siku. Imenisaidia kuweza kujimudu kimaisha.

Natoa fungu la kumi kanisani kila mwezi, ndio linaloniokoa mimi mpaka leo. Mama huyo anasema kuna mwanaume mwingine, alijitokeza kumchumbia mtoto wake.

Alieleza nia yake ya kutaka kumuoa binti huyo. Farahana alimueleza ukweli binti huyo kuwa alishawahi kuoelewa na mengine yote, hivyo aje na wazee wake na barua. Mtu huyo alikwenda na wajomba zake na walipewa masharti kuwa kabla ya kuleta barua, lazima kupima.

Kweli walienda kupima. Mwanaume huyo aliulizwa mara tatu kama ana mke, akasema hana. Walifunga ndoa katika Kanisa la Baptisti na kisha walifanya sherehe ndogo.

Baada ya siku tatu, mwanaume huyo aliondoka kwenda Tabora na alimuachia binti huyo Sh 2,000.

“Mwanangu akanipigia simu anaomba fedha ya kula. Nikamuliza unaomba fedha mumeo yupo wapi? Akasema amesafiri ameenda Tabora kaniachia shilingi 2,000 tu.

Mimi wakati huo nilikuwa nafanya ruti za Gerezani – Machimbo, nikifika Machimbo nilikuwa nampigia simu nampa shilingi 5,000 ya kula kila siku. Baadaye nikaona bora arudi nyumbani hadi mumewe atakaporudi. Nikamrudisha nyumbani, akakaa miezi miwili ndio mumewe akarudi na kusema mama asante kwa kunitunzia mke.

“Nilimwambia mwanangu una cheti chako cha kidato cha nne, nenda katafute ajira, na kweli alipata Kituo cha Mafuta cha Victoria. Baadaye mumewe aliporudi akamwambia hataki afanye kazi. Ukawa mzozo mkubwa. Baadae simu ya mwanaume ikaita, mwanangu alipoipokea alisikia sauti ya mwanamke inamwambia nipe Baba Rebeka niongee naye.

Akamuliza Baba Rebeka? Baba Rebeka ndio nani, mimi simjui?. Akasema hiyo namba ni ya mume wangu na mimi ndio mkewe. Mwanangu akasema mbona hata mimi ni mume wangu na hana mke wala mtoto. Yule mama akasisitiza kuwa ni mumewe. Basi mwanangu akamuuliza mumewe kama anamfahamu mama Rebeka, yeye akamwambia achane na hayo mambo. Mwanangu alichanganyikiwa sana,” anasema.

Farahana anasema mwanawe alirudi nyumbani, akamwambia mume wake ameoa na alimuonesha namba ya mke huyo mwingine. Mwanae alisema alimpigia simu mwanamke huyo, ambapo aliipokea na alipomuuliza alilia sana na akasema huyo ni mumewe na amezaa naye watoto wanne.

Kwamba kwa sasa ana mtoto wa nne mchanga wa mwezi mmoja tu. Kuna siku walifanya kikao, ambapo mwanaume huyo alipoulizwa kuhusu mtoto wa Farahana , alimkataa na kumkana binti huyo.

Hata wajomba zake walikana kuleta mahari. Ndipo mwanangu alibeba vitu vyake vyote na kurudi nyumbani. Baada ya siku chache mwanaume alikuja nyumbani, kuomba warudiane na binti huyo.

Farahana anasema alimtimua kama mwizi, maana alijua lengo lake lilikuwa kumchezea binti huyo. Farahana anasema mwanawe wa kiume yupo kidato cha nne na siku zote humuelekeza asome kwa bidii, kwa kuangalia maisha ambayo wanayoishi.

Changamoto zinazomkabili Anataja changamoto anazopata ni pamoja na kudharauliwa na baadhi ya abiria na kutukanwa. “Ni vigumu kupata gari la kufanyia kazi iwapo wewe ni mwanamke. Wanawake hufanya bidii mara tatu zaidi ndipo wapate kazi.

Makondakta wa kike katika daladala tunapitia mengi. Tunadhalilishwa kimapenzi na wengi tudhaniwa kuwa ni makahaba au watu walioshindikana katika familia. Jamii haitutazami kwa jicho zuri. Baadhi ya abiria wa kiume hukataa kulipa nauli na tunapowakabili huwa wanatutusi kwa maneno makali ya kashfa.

Wakati mwingine hutushambulia. Mimi kuna abiria wa kiume alishawahi kunisukumiza na kuniumiza. Unaona hili kovu mkononi?” anasema na kuonesha mkono wake wenye kovu kubwa. Anasema abiria aliyemfanyia hivyo alimpeleka polisi, lakini aliachiliwa na kesi ikaisha na hakulipwa fidia.

Ndoto yake Farahana anasema amejifunza kuendesha gari na kwamba ndoto yake ni kuendesha magari ya masafa marefu.

Ana leseni lakini bado hajafanikiwa kupata kazi katika kampuni ya kueleweka. Anasema mume wake anatamani awe dereva wa daladala jijini Dar es Salaam, lakini vizingiti vya hapa na pale anakutana navyo Fallana vinazuia ndoto yake hiyo. Kauli ya mumewe Mume wake anasema “Mimi ndio nimemuingiza kwenye kazi ya daladala.

Nilimwambia ajishikize, si unajua changamoto za maisha?. Hamuwezi kukaa wote nyumbani mnaangaliana. Lazima kupambana. Najua anapambana na vishawishi kibao. Kinachotakiwa ni yeye tu kuangalia atayashinda vipi. Mtu mzima hachungwi.”

Historia Yake Farahana Mwanjonde alizaliwa Mbeya mwaka 1980. Alisoma darasa la kwanza hadi la tano katika Shule ya Msingi Kiabakari iliyokuwa katika kambi ya Jeshi la Wananchi Musoma kisha alihamishiwa Shinyanga, ambako alihitimu darasa la saba mwaka 1995.

Alifaulu na kujiunga na Shule ya Sekondari ya Shycom, ambako alisoma kidato cha kwanza hadi mwaka 1999 alipohitimu kidato cha nne.

Alichaguliwa kwenda kozi ya uaskari polisi kwa miezi sita katika Chuo cha Polisi (CCP) na alipohitimu mwaka 2000 alipangiwa Kituo cha Musoma.

Alikaa Musoma kwa miaka kadhaa, lakini baadaye alihamishwa Mbeya, ambako alitumikia jeshi miaka mitano mpaka mwaka 2005 alipofukuzwa kazi kutokana na upotevu wa silaha.

View attachment 1392244

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli ukiwa na amani, unakula, unalala, una hela muda wote ni jambo la kumshukuru Mungu. Story yake inaweza kutengeneza tamthilia nzuri sana au movie nzuri mno.
 
Back
Top Bottom