Bin Maryam
JF-Expert Member
- Oct 22, 2007
- 685
- 13
Mafuchila,
Mimi nina imani marais wastahafu hawa hawa Mh. Mzee wetu Benjamin William Mkapa na Mh. Mzee wetu Ali Hassan Mwinyi, wangekuwa marais kwenye jamii inayowajibika, inayofanya kazi tena kwa juhudi na maarifa bado hawa wazee wangekuwa mastaa wazuri sana.
Tatizo letu tunajiondolea wajibu wetu na kudhani marais ndio wafanye kazi yetu! Nitawapa mfano... matatizo ya Richmond kwa asilimia kubwa yamechangiwa na wataalamu wasioheshimu taaluma zao kutoka wizarani, na pale ofisi ya mwanasheria mkuu... hii sio rais.
Leo hii nakerwa sana kwamba watanzania wasiotoa kodi ndio mabingwa wa kutaka kufanyiwa kila kitu na serikali...
Kwa kweli taifa hili ambalo zinatenganisha HAKI na WAJIBU hatuwezi fika popote... unapotaka HAKI pia tekeleza wajibu wako... Jiulize kwa mwezi/mwaka unachaingia serikali kipato cha kiasi gani kama kodi?
Mwisho Mkapa aliitoa nchi mahali pabaya sana... nakumbuka UDSM, Mwinyi alipafanya pawe kama primary school. Mwinyi pia alituvusha vizuri kwenye siasa ya vyama vingi na mambo ya Utandawazi... tulikokosea... tulikosea, tuangalie tusijekosea tena....
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
UDSM inaongozwa na ma-Professor, je Mwinyi alifanyaje iwe primary school?