Kanyunyu
JF-Expert Member
- May 2, 2012
- 335
- 495
Nani Kachora Nembo ya Taifa: Mzee Farahani (Farhan), Ngosha, au Jeremiah Wisdom Kabati?
Kuna wanaosema Mzee Jeremiah Wisdom Kabati kachora nembo ya Taifa. Wengine wanasema Mzee Ngosha kachora. Kwa sasa mimi nipo upande wa Professor Elias Jengo anayesema nembo ilichorwa na Mzee Abdallah Farahani kutoka Zanzibar. Professor Jengo aliandika kwenye kitabu kwamba Mzee Farahani ndio aliyechora nembo ya Taifa.
Inasemekana mtoto wa Mzee Farahani, Iddi Farahani alikuwa na sketches za baba yake za hii nembo. Mzee Farahani alisoma na Mwalimu Nyerere Makerere. Professor Elias Jengo kutoka Chuo Kikuu anaandika kwenye kitabu “East Africa Art Biennale” kwamba “As a designer, Abdallah Farahani will be remembered for his design of the national emblem. The emblem was recently criticized by a legislator for depicting barefooted human figures.” Ukurasa 44.
Kaka Dominicus Makukula, msanii na mwalimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, anaamini kwamba Mzee Furahani ndio aliyechora ile nembo ya taifa. Anasema mjukuu wa Mzee Farahani yupo Music Academy Zanzibar na pengine anaweza kutoa majibu kama kuna atayeweza kwenda kuongea nae zaidi. Mpaka tutapopata habari zaidi, inaonenaka kwamba Mzee Farahani kutoka Zanzibar ndio aliyechora ile nembo. Tusubiri tuone kama serikali itafuta mavumbi na kufungua maboksi yenye nyaraka husika.
FACT NUMBER 2
Tukiangalia nembo hii ya Tanganyika 1961, ile ya Tanzania 1964 na ule mchoro usio na rangi uliopo katika nyaraka ya National Flag and Coat of Arms Act ya 1971, tunapata nafasi na sababu ya kudhani kuwa mchoraji na mbunifu halisi wa nembo ya Taifa si Ngosha wala marehemu mzee Jeremiah Kabati. Familia ya kabati inasema mzee alichora nembo hiyo mwaka 1960 na katika mahojiano na TBC Taifa, Ngosha alisema kuwa alisanifu nembo hiyo na mwenzake mwaka 1957.
Prof. Jengo anathibitisha kuwa mchoro wa Farahani kwa ajili ya Tanganyika uliandaliwa mwaka 1961 na kuboreshwa 1964 wakati wa maandalizi ya nembo ya Jamhuri ya muungano. Swali la msingi, je yawezekanaje pasiwe na kumbukumbu hali miaka kumi baadae, marehemu Mwl. Nyerere alipatiwa mswada wa sheria ya nembo ya Taifa ileile ya mwaka 1961 pia 1964 (isiyonakshiwa kwa rangi) kwa ajili ya kuisaini ili iwe sheria kamili. Je walioandaa mswada walitoa wapi blue print ya nembo halisi mwaka 1971?
Tatizo si kukosekana kwa nyaraka wala kumbukumbu, bali tatizo ni kukosekana watu wenye weledi kweye eneo la historia ya sanaa katika kuhifadhi amali hizi za Taifa katika mamlaka za kusimamia sanaa na utamaduni wa Taifa. mzee Mbughuni Sr. alifanya kazi kama Promoter of national arts miaka ya 1960s na hatimaye kuwa mkurugenzi wa idara ya sanaa miaka ya 1970s mwishoni, alianzisha Chuo cha Sanaa Bagamoyo mwaka 1981 baada ya kuvunja kikundi cha sanaa cha Taifa mwaka 1979 (Kelly Askew 2005:304-309), hawa ndio aina ya watu tuliowakosa katika miaka hii Tanzania.
Imechukuliwa kutoka bandiko la Azaria Mbughuni
May 26, 2017