Nani kachoma soko la Sido?

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
5,583
11,659
Serikali iache siasa

Ili kutatua mgogoro wa masoko katika eneo hilo la Mwanjelwa, vongozi wanatakiwa kuacha siasa na kusimamia sheria.

Soko la Sido sio rasmi, lilianzishwa baada ya kuungua kwa Soko la Mwanjelwa kwa lengo la kuwahifadhi wafanyabiashara walioathirika na ajali hiyo ya moto.

Tangu awali ilifahamika kuwa ni makazi ya muda yaliyoombwa kutoka kwa wamiliki wa eneo hilo ambao ni pamoja na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo nchini (SIDO) na kiongozi mstaafu, Nsa Kaisi.

Hata hiyo, wafanyabiashara hao wakahalalisha kuwa maeneo yao ya kudumu. Tayari kesi ipo mahakamani ambapo mmoja wa wamiliki hao analihitaji eneo lake.

“Serikali isitoe majibu ya kisiasa, waamue kupunguza kodi ya vyumba kwenye soko jipya na wafunge Soko la Sido,” anasema mkazi wa jijini Mbeya aliyetambulika kwa jina la Method.

Hatua ya kufungwa kwa soko hilo inaelezwa kuwa itasaidia kuimarisha usalama wa wafanyabiashara na mali zao pamoja na eneo lote kwa ujumla ambalo katika miaka ya hivi karibu limekuwa kitovu cha vurugu.

Wapiga debe, vibarua na wabeba mizigo wanatajwa kuwa chanzo cha vurugu zinazotokea eneo hilo la Mwanjelwa, lengo lao likielezwa kuwa ni kupora mali.

Hoja hiyo ya baadhi ya wafanyabiashara wa Mwanjelwa, inaoana na ile ya Kamanda Mpinga ambaye alizielezea vurugu zilizotokea siku moja baada ya ajali hiyo ya moto kuwa zilisababishwa na wahuni.

“Wafanyabiashara walitoa malalamiko yao kwa DC, ndipo vijana wakatumia nafasi hiyo, lengo zitokee vurugu ili wapore,” alisema Kamanda Mpinga katika mahojiano yake na Raia Mwemakwa njia ya simu.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom