Nani Juha Zaidi

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,810
Majuha watatu walikuwa wakishindana kuhusu nani juha zaidi kati yao...

Juha 1: Mi siku moja nilivyokuwa nje ya nchi nilimpigia mke wangu simu usiku kafungua simu hakusema haloo... kulaleki! na mimi nikakaa kimya sikuongea mpaka alfajiri wakati simu ilikuwa wazi inasoma masaa na madakika kibao.

Juha 2: Mbona hiyo cha mtoto, mi siku moja nimerudi home nikagonga mlango mke wangu akaufungua lakini hakusema karibu mume wangu... aliniangalia tu... nikaona analeta madharau! sikuingia ndani nikasimama hapo hapo mlangoni mpaka asubuhi... huyoo nikatimua zangu job.

Juha 3 akaunganisha: Hiyo nayo mbona cha mtoto tu, mi mke wangu tulipo oana alikuwa anaona haya kunigusa... ananidengulia eti! Na mimi sikumgusa na mpaka leo hatugusani.

Juha 1 na 2: Aaaaaaaah fazaaa! wacha usanii weweee, nyie si mna watoto watatu sasa...!!?

Juha 3: Na kudadeki hao watoto sijamuuliza kawaokota wapi... mi nataka mchezo kwani...!
 
Back
Top Bottom