Nani hatari zaidi kati ya malaika aliyegeuka shetani, Au shetani aliyegeuka malaika?! | Page 6 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani hatari zaidi kati ya malaika aliyegeuka shetani, Au shetani aliyegeuka malaika?!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pascal Mayalla, Sep 2, 2015.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Sep 2, 2015
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,639
  Likes Received: 23,821
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Leo tena naendelea na zile makala zangu za malaika na shetani.

  Kwa wasomaji wapya katika kukumbushana tuu, hapo hapo mwanzo, shetani alikuwa malaika kabla hajawa shetani, tena ndio alikuwa malaika Mkuu! .

  Kwenye himaya ya mashetani shetani hayuko peke yake, yuko na wale malaika wengine waliojiunga nae ambao sasa wote ni mashetani wengine walioamua kujiunga nae!.

  Katika la jeshi la malaika wa mbinguni from time to kuna baadhi ya malaika huwa wana defect na kumfuata shetani na hivyo hugeuka mashetani.

  Vivyo hivyo kwenye jeshi la shetani kuna mashetani huwa wanatubu na kumrudia Mungu hivyo hurejea na kuwa malaika. Hawa sasa ni harmless kwa sababu ushetani wao wote wanakuwa wameuacha kule ushetanini!.

  Lakini inapotokea malaika akaamua kufanya kazi ya shetani huku amepose kama malaika!, huyu ni hatari kuliko hata shetani mwenyewe!, maana you can't tell!. Watu wa Mungu watamsikiliza wakidhani ni malaika kumbe nje na ngozi tuu ndio ya malaika lakini ndani ni ibilisi mwovu shetani wahedi! .

  Swali ni jee?, nani ni hatari zaidi kati ya shetani aliyetubu na kugeuka malaika au malaika aliyegeuka shetani kwa kufanya kazi ya shetani huku akiendelea kupose as malaika?!.

  Tafakari na chukua hatua.

  Nawatakia Jumatano njema.

  Pascal

   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #101
  Oct 9, 2017
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,639
  Likes Received: 23,821
  Trophy Points: 280
  Mkuu mkombengwa, ile tuu hali ya kuwa shetani, tayari ni auasi, hivyo shetani hasi , tayari ni hasi, ila wako mashetani ambao wanatubu na kumrudia Mungu, hawa hugeuka tena malaika.

  Hatari zaidi ni wale malaika ambao kwa nje ni malaika lakini kwa ndani ni mashetani!, hivyo hawa wame pose kama malaika but in fact ni mashetani. Malaika hawa ndio waliopanga shambulizi la Lissu, kwa nje ni malaika lakini kwa ndani ni mashetani.

  P.
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #102
  Oct 30, 2017
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,639
  Likes Received: 23,821
  Trophy Points: 280
  Naendelea na tafakuri yangu kuhusu malaika na shetani, leo nimepokea taarifa ya kuna mtu mmoja ameasi, ila sijajua kama ni alikuwa malaika au shetani. Kama alikuwa malaika na huko alikoasi ni umalaikani, hivyo sasa amegeuka shetani. Lakini kama alikuwa shetani na huko alikoasi ni ushetanini, then atakuwa amegeuka malaika.

  Swali la msingi bado limebaki pale pale, nani hatari zaidi kati ya malaika Aliyegeuka shetani na shetani aliyetubu ushetani wake wake na kuondoka kutoka ushetanini ?.

  Paskali


  shetani
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...