ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 42,813
- 49,503
Wakishindwa na kufirisika akili wanakimbilia kujificha kwenye kivuli cha uzalendoUko sahihi sana, ilikuwa ni rahisi sana, ukweli ni kuwa wenye uwezo wa kulima walikuwa ni wazungu, hao waafrika walikuwa ni wakuna ardhi hamna mkulima. Ungewekwa utaratibu mzuri wa mfuko maalum ambao kila mzungu anayemiliki ardhi akatwe kiasi walipwe wanaodai, au hizo pesa zianzishe viwanda na watakaopewa ajira kipaombele ni waliokua wameondolewa kwenye ardhi. Ila mihemko ya viongozi kujifanya wazalendo na kusaka kiki za kisiasa ndio matokeo yake. Je hao wafrika waliporudishiwa hizo ardhi walitoka kwenye umasikini au ndio walirudi rasmi kwenye umasikini wakiwa wanamiliki ardhi?
Kibaya zaidi huyo rais aliyekuwa anajifanya rais mzalendo akaishia kukaa madarakani kwa mrefu tena kwa mbinu chafu kuliko hata hizo za hao wazungu, huku akitumia ardhi alizowapa hao weusi kama kete ya kuendelea kukaa madarakani hata mambo yalipokuwa mabaya. Huu ni mchezo wa viongozi wengi wa kiafrika kujifanya wazalendo huku wakichezea box la kura ili wabaki madarakani. Mchezo huo wa kiongozi kujifanya mzalendo ili akae madarakani kwa kisingizio cha uzalendo uko hata hapa nchini, na tunaona kabisa chaguzi zenye dhuluma na matendo machafu kwa kisingizio cha kuleta maendeleo na uzalendo wa kuigiza.
Wananchi wanaimbiwa pambio za uzalendo kwa kiki wanashangilia huku wanaumia wanasiasa wanazidi kitumbua
Ifike mahala rais asiwe muamuzi wa kila akitakacho ona makinikia yalikoishia hamna kitu zaidi ya hasara sasa hivi wanataka walete malumbano yasiyo na msingi na mabeberu afu tunaumia saizi hakuna condom za jero hospitali dawa za kutafutiza sasa uzalendo njaa hautusaidii