Nani chanzo cha records za mawasiliano zinazosambaa mtandaoni?

Wapo bize kusikiliza simu za watu badala ya kuwaletea wananchi maendeleo ,miaka minne unashindwa kuwaunganisha watu ndani ya chama chake na kuwa wamoja nchi ndio utaiweza .
 
Wapinzani ndio walianza huo mtindo kwa lengo la kuwashughulikia watu ndani ya Chama chao hasa Chadema.
Sasa CCM wakitumia Kosa lao nini?
.Tuwaache CCM wawashughulikie wasio wanaCCM wa kweli.
Chama kibaki Cha Wajamaa.
Mabepari wote watoke wanzishe chama Chao.
Hata hao waliobakia bado wanafiki ni wengi.
Nchi maskini kama hii Watawala hawana uhalali wa kimaadili ya Siasa za kijamaa kutembelea Magari yenye Bei sawa na Zahanati Moja ya Kata.
Wanatembelea Magari ya kifahari kwa faida ya Nani na kwa Hasara ya Nani?
Kwa nini wastarehe kwa gharama za walipa Kodi wanaoumizwa kila siku huku wafanyakazi wa Chini wakikosa kuongezwa mishahara hata kifikia ⅛ ya ile ya Kwao.
Bado tunadanhanyana kwa michezo hii ya Kushughulikiana na Kukomoana.
Ni vyema iendelee ili Wabakie Wajamaa halisi kwenye Hicho Chama au mabepari halisi.
Ni bora wawe Moto au Baridi kuliko kuwa Viguvugu.
Uvuguvugu ni unafiki.
Nchi hii hatuendelei kwa sababu ya unafiki mwingi.

Washughulikiwe tu wote wenye hulka za kusaliti Chama.
Japo kusaliti Chama au kumsaliti Mtu sio kusaliti Nchi mana nchi ni zaidi ya Chama.
Tunataka tu wasishughulikiane kwa sababu ya kusaka vyeo maslahi jambo linaloligharimu taifa kukosa watu wenye uwezo na kubaki na wanafiki wanaojiita waunga mkono mtu na juhudi zake bila wao kujua la kufanya ili kuleta ubunifu na tija kwa taifa.
 
Israel imeleta balaa, iliziuzia nchi nyingi duniani Software za kudukua watu basi imekuwa shida kubwa
Hata Kashoggi alikuwa akidukuliwa na mamlaka za Saudi Arabia kwa kutumia software hii ya Israel
Kwenye Software hii Usidhani kuwa Whatsapp iko salama, Jamaa wana uwezo wa kudukua maongezi hata text!
Software mojawapo ya waisrael ya kufanya udukuzi inaitwa PEGASUS
aisee, naipataje hii? kudukua watu ni raha sana
 
Tafuta usome article ya " Phone tapping national leaders "Normal"

Tukio la 2013 nchini Indonesia ,Badan intelijen Negara(BIN),walivyoshutumiwa ku tap maongezi ya simu ya wanasiasa wa Australia,sikia majibu ya kiongozi Mstafu wa shirika la kijasusi la BIN , Mr.Hendropriyono alivyosema alisema "Tapping and counter tapping is quete common in the intelligence life, because it is one of their jobs "
Kwa kiswahili wanasema kuingilia mawasiliano na kuzuia kuingiliwa ni jambo la kawaida katika maisha ya kijasusi , kwasababu ndio moja ya kazi zao.

Akaendelea kusema ,mara nyingi nchi hufanya kwa wanasiasa wake wa ndani kujua yupi adui ,yupi sio adui ,pia hata ikivuka nje ya nchi ina lengo la kujua Kama nchi jirani yako uliyenaye kama ni adui au rafiki na sio vingine.

My Take.

Kila kazi ina ni dhamu zake ,ni sawa wewe ni daktari kazi yako Kama daktari una kazi ya kutibu mgonjwa ,anaweza kuvua nguo zote kwa lengo la kumtibu aidha kumchoma Sindano au operation ,vyote vinawezekana ila ni kwa lengo kuu moja tuu la kumpatia matibabu ,na baada ya kumpatia matibabu kimaadili hutakiwi mtangaza alivyo ,au ugonjwa anao umwa, na hata kama uta record ugonjwa wake iwe ni kwa lengo maalumu kuweka kumbu kumbu au kujua kiasi ugonjwa ule umetawala ili kutoa Kinga na tahadhari sio kutaja fulani anaumwa .

Mashirika mengi ya Kijasusi yana vyombo vyao binafsi vya kuingilia mawasiliano ya watu nchini ili kutambua maadui ,na kutumia njia hiyo kuzuia adhari kabla ya kutokea,au kujua nyendo za mtu fulani ambaye ana lengo la kuvuruga usalama wa nchi au Taifa .

Nchi za Afrika wamechelewa kupokea vyombo hivyo ,labda ndio sababu kubwa ya kuvitumia kwa kukeuka maadili ya kazi zao.Ila wanaruhusiwa na wanaweza ku tap ila kwa matumizi yao sio ya umma.

Msiwalaumu TCRA wala makampuni ya Simu.
Nondo,
Ulikuwa na mjumbe mzuri mno lakini nimeusoma kama mara mbili na kuhisi ya kuwa hukuandika wewe!
Style yako ya uandishi kawaida ina mtirirko mzuri.
Yote kwa yote ni kweli kuwa ni lazima tuwe salama na hata hapa inapoingia usiku kuna watu hawalali kwa ajili ya usalama wetu.
Udukuzi upo lakini udukuzi bila maadili ni hasara.Kasome "The watergate scandal"
Ikiwa mawaziri wanadukuliwavipi Halima Mdee,Maalim Seif,Zitto,Mbowe n.k?
Tuna la kujifunza katika hili.
 
Back
Top Bottom