Nani Bingwa wa Ushairi Tanzania baada ya Shaaban Robert na Kezilahabi?

Team JPM

JF-Expert Member
Nov 11, 2018
1,074
1,608
Leo ni siku ya ushairi Duniani, Nawapongeza watunzi wote wa ushairi nchini Tanzania, Afrika na duniani kote.
Wengi tunamsikia Shaban Robert na Kezilahabi kama watunzi mashuhuri wa Mashairi nchini Tanzania lakini hatukuwahi kuwaona wala kufundishwa nao ingawa kazi zao twazisoma na kuzisikia.
Katika maadhimisho ya siku ya ushairi duniani, Nguli yupi ni zaidi baina ya Theobald Mvungi mtunzi wa Diwani ya Chungu Tamu, Mohamed Khatibu wa Mashairi ya Wasakatonge na Fungate ya Uhuru katika watunzi wa Vitabu vya ushairi?
Je, kwa wahadhiri wa sanaa ya Ushairi pale chuo kikuu cha Dar es salaam, nani bingwa kwa mwenzake baina ya Profesa Kahigi na Mulokozi?.
Nitumie siku hii kuwapongeza watunzi na wahadhiri wote wa sanaa ya ushairi maana ushairi ndio umezaa muziki.
 
Mimi kwangu Washairi wazuri ni Andanenga,Mtu chake,Adam Mussa(pande LA jitu) Sihiyana Swalehe Mandevu, Mwamshindo nk hawa ki ukweli mashairi yao yalikuwa yanaburudisha sana kipindi chao

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom