Nani bado anaamini Lowassa atashitakiwa mahakama ya mafisadi?

Bome-e

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
17,104
26,070
Kumekuwa na utitiri wa wafuasi wa CCM mitandaoni ambao wengi wao wanamwita lowassa ni fisadi namba moja nchini au fisadi kuu! Wengi wao wamekuwa wakiwaaminisha watu kuwa mahakama ya mafisadi itamshughulikia Lowassa!

Baadhi yetu hilo ndio lilikuwa ombi letu kubwa kuwa kuliko kuendelea kupiga kelele kuwa lowassa ni fisadi basi ni vema akafikishwa mahakamani ili mbivu na mbichi zijulikane! Tulisema mtu huyu hawezi fikishwa mahakamani kwani kwa kufanya hivyo wapiga deal halisi wa Richmond watajulikana ambao ndio hao wamehakikishiwa ulinzi toka juu!

Jana tumeshuhudia Rais JPM akisema mbele ya viongozi wa dini kuwa amepata Baraka za kipekee kwa kupeana mkono na Lowassa jambo ambalo limekuwa gumu tokea aingie madarakani!

Kwa kauli hizi za Rais kupata Baraka kwa kupeana mkono na Lowassa(au fisadi mkuu kama wanaccm wanavyomuita), kuna dalili zozote mtu huyu kufikishwa mahakama ya mafisadi kama wanaccm wengi walivyokuwa wanatuaminisha?

Je, wale vinara wa CCM humu mitandaoni wanaomchafua lowassa kwa kashfa mbalimbali na matusi, wanajisikiaje walipoona Rais anasema amepata Baraka kwa kupeana naye mkono?

NB: Vijana wa Lumumba, tumeshawaonya mara nyingi kuweka vifua mbele kwa mambo ambayo hata hamyajui, sijui sasa mtapata ujasiri wapi wa kuendelea kumtusi mtu aliyempa Baraka mtukufu Rais!
=============
Ni kiongozi gani wa CCM atakuwa na "Moral Authority" ya kumuita Lowassa fisadi na akaeleweka?

Binafsi sitaki kuamini eti Lowassa atarudi CCM bali naamini anafanya anayoyafanya kwasababu ni mtu mwenye foresight.

Kwa tukio la jana Lowassa alijua ni nini ata-achieve politicaly na sikuwa alienda kusaliti upinzani kama baadhi ya watu wanavyofikiri.

Kikubwa alichofanikiwa Lowassa kwa tukio la jana ni kuwanyamazisha CCM na zaidi kuwaondolea moral authority ya wao kumuita fisadi.Na kwa bahati nzuri Magufuli ndio kajichanganya kabisa kwa kumwagia sifa Lowassa na hiki ndicho Lowassa alikuwa anakitafuta.

Lowassa kwasababu ni mtu mwenye foresight aliona hii fursa mapema na akaitumia vizuri na kwakweli imemlipa barabara.

Kama mwenyekiti wa CCM leo hii anashikana mikono na Lowaasa tena kwa furaha mbele ya maraisi na mawaziri wakuu wastaafu tena huku akimiminia sifa kesho atapata wapi moral authority ya kumkejeli Lowassa?

Unapomuona Lowassa anateta friendly na Katibu Mkuu wa CCM ni mwanachama gani wa CCM atakuwa na nguvu ya kumkashifu Lowassa.

Nani asieona nafasi ya Lowassa leo hii kuwa kiungo kati ya upinzani na chama tawala.

Nani asieona nafasi alioyonayo Lowassa baada ya tukio hilo katika kupenyeza agenda za wapinzani kwa watawala kama vile kudai Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi?

Kama Lowassa leo hii ameweza kukaa na wapinzani atashindwa nini kukaa meza moja na waliokuwa wana-CCM wenzake katika kupatia ufumbuzi hoja za wapinzani?

Najua wako wengi wameamua na kukata tamaa kumuona Lowassa akikaa meza moja na viongozi waandamizi wa CCM na serikali na kuhisi anawasaliti lakini hakika nawaambieni siku si nyingi mnaweza kuona Lema na viongozi wengine wa upinzani waanachiwa bila mashariti na wengine kesi zao kufutwa.

Kama Nyerere alivyoweza kupigania uhuru wa nchi bila watu kumwaga damu hivyo ndivyo Lowassa anavyojaribu kupata suluhu ya tofauti zilizopo bila kuleta machafuko na ndio maana akipata fursa anaitumiaa effectively.
 
Wee huijui siasa... Tusubiri...

Angekuwa wa kupelekwa mahakamani angeshapelekwa siku nyingi...Tutakaa sana tukisubiri hata itakapofika kipindi kingine cha kampeni:(o_Oo_O
 
Muda ukifika kama ni kushtakiwa atashtakiwa akiwa msafi ataachiwa. Tusubiri.

NB: Wakuonywa ni wewe unayejipanga kwenda kuandamana uvunjwe miguu na wakati viongozi wako waliokutuma wanakunywa mvinyo na unaowapinga.
 
Wee huijui siasa... Tusubiri...

Angekuwa wa kupelekwa mahakamani angeshapelekwa siku nyingi...Tutakaa sana tukisubiri hata itakapofika kipindi kingine cha kampeni:(o_Oo_O
Hayo tuliyaona mapema ila vijana wa lumumba wakaaminisha watu tofauti!sasa waje hapa waseme
 
Muda ukifika kama ni kushtakiwa atashtakiwa akiwa msafi ataachiwa. Tusubiri.

NB: Wakuonywa ni wewe unayejipanga kwenda kuandamana uvunjwe miguu na wakati viongozi wako waliokutuma wanakunywa mvinyo na unaowapinga.
Uko nje ya mada,jikite kwenye mada!Unazungumziaje JPM kupata baraka kwa kumpa mkono lowassa?
 
Siasa tu hiyo, ila lazima afikishwe Mahakama ya Mafisadi. Kumbe ulikuwa na hofu,utashangaa mwenyewe wewe subiri tu
 
Wanasiasa wanacheza na watu wenye akili kama zako, hata kama huyo mzee ni mwizi sahau kuwa atashitakiwa kwenye hiyo mahakama ya mafisadi.


Hakuna tofauti ya wanasiasa wa chama tawala na wale wa upinzani.......hao wanasiasa wote mtaji wao ni wananchi wasiojitambua.
 
Wanasiasa wanacheza na watu wenye akili kama zako, hata kama huyo mzee ni mwizi sahau kuwa atashitakiwa kwenye hiyo mahakama ya mafisadi.


Hakuna tofauti ya wanasiasa wa chama tawala na wale wa upinzani.......hao wanasiasa wote mtaji wao ni wananchi wasiojitambua.
Ndio maana nikasema nani bado anategemea kuona jamaa kizimbani kwa ufisadi?Ndio watu wajue wanasiasa,mahakama ya mafisadi ni gia ya kuombea kura tu!
 
Back
Top Bottom