Nani atwambie shillingi yetu imeathirika kiasi gani kwa kupanda gharama za umeme (Inflation) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani atwambie shillingi yetu imeathirika kiasi gani kwa kupanda gharama za umeme (Inflation)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mghaka, Feb 19, 2012.

 1. M

  Mghaka JF-Expert Member

  #1
  Feb 19, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 320
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hivi nani anaweza kuwaambia wakulima na wafanyakazi ambao ujira wao thamani yake haitegemei mabadiliko ya gharama za uendeshaji wameathirika kiasi gani na upandaji wa gharama za TANESCO. Nimeona wafanyabiashara wote wamepandishga bei ya huduma wanazotupatia kwa sababu tu umeme umepanda bei, lakini sijaona wakulima wafanye hivyo, wafanyakazi nao pia wako kimya.

  Siamini kuwa mabadiliko ya gharama za umeme hayakuwagusa wakulima na wafanyakazi. Kazi kwenu jamii forum tungependa kuona mtu anatuambia mshahara wa Tshs 300,000 mwezi Novemba kabla ya mabadiliko ya bei za TANESCO ulikuwa unaweza kufanya nini na leo baada ya ongezeko hilo kubwa thamani ya mshahara huo ni kiasi gani, hivyo hivyo kwa wakulima ambao walivuna magunia ya mahindi 1000 Desemba na wale wanaovuna sasa hivi mabadiliko hayo yamewaathiri kiasi gani. Naomba tuwasaidie wanasiasa wetu kujenga hoja na kuzipeleka kwa wananchi ili wawezeshe wananchi waiulize serikali yao na ikibidi waikatalie kwani ongezeko hili linauhusiano wa moja kwa moja na ubadhilifu ulioikumba TANESCO na mikataba bomu walioingia na wabia wao.
   
Loading...