Elections 2010 Nani atashinda kati ya hawa?

Dr Shein lazima apite, ni mtu makini mchapa kazi, asiye fisadi, mwenye shule iliyonyooka na mawazo chanya.
 
Jamani kwani wanayemtaka si ndo mshindi!!
Tujuavyo hapa Dakitari ndo anayetakiwa kuachiwa mikoba!!!

Kuna jipywa hapa kweli?
 
atashinda yule CCM ambaye ana sifa kuu zifuatazo...wadau tuongeze sifa nyingine
1. si tishio kwa Mafisadi
2.atakaye kuwa tayari kulinda maslahi ya Viongozi (vigogo)wanaomaliza muda wao
3
 
asante kaka hapa mtiani mtupu...... dr shein ni dr siye na kikwazo nadhani hata GPA yake ni yenye mvuto pale, kwanini ashindwe. hata mimi najiuliza kwa nini dr gharib bilali anapambana nae ingawa nae ni msomi lakini pana kitu hapa
 
Shamsi Vuai ndio anafaa sema inaonekana watashindwa kumburuza watakavyo kwahio watampa Dr Shein hili wafanye wanachotaka.
 
Mwenye nguvu kisiasa na rahisi kuchagulika ni Bilal ila katika system ya CCM Bara kuna wamtake ambae ni Shein.....Motto wa CCM sote tunaujua "USHINDI LAZIMA" so obvious Shein ataiongoza Zanzibar....................
 
Questt uko na mimi,

Me naona hivyo ndivyo ilivyo na ndivyo itakavyokuwa.

Ila mzee bilal anafaa sana na naona anakubalika na wazenji wengi kwa hiyo ana political capital atamudu mapambano.
 
Dr. Shein hawezi kumshinda Seif kama uchaguzi utakuwa wa huru na haki; kiongozi toka CCM ambaye anaweza kuchuana na Seif ni Bilal kwani awali ya yote ni msomi na mzaliwa wa Unguja na si Pemba!! Shein hata kule kwao Pemba hawezi kumshinda Seif! Sasa kama CCM watamuengua Bilal kwa sababu ya Inferiority complex ya Kikwete basi wajue wanachimbia kisima!
 
asante kaka hapa mtiani mtupu...... dr shein ni dr siye na kikwazo nadhani hata GPA yake ni yenye mvuto pale, kwanini ashindwe. hata mimi najiuliza kwa nini dr gharib bilali anapambana nae ingawa nae ni msomi lakini pana kitu hapa
Heb eleza uzuri hoja yako!! kwani ukiwa msomi katika level ya DhD unaweza kuongoza?
 
Back
Top Bottom