nani ataongoza halmashauri hanang cdm au ccm a

AMARIDONG

JF-Expert Member
Jun 24, 2010
2,502
0
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mgombea wa uenyekiti wa Baraza la Madiwani la Halmshauri la wilaya ya Hanang mkoani Manyara kwa tiketi ya Chadema, Peter Lori, ametamba na kutabiri kuwa kwa mara ya kwanza halmashauri hiyo sasa itaongozwa na Chama Cha Maendeleo na Demokrasia (Chadema).[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Lori ambaye ni Diwani wa Kata ya Kateshi Mjini, aliiambia NIPASHE kuwa kwa mara ya kwanza wananchi wa Wilaya ya Hanang watarajie kuona mabadiliko ya mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya akitoka Chadema.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Hata hivyo, kauli na utabiri huo umepingwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho kimedai kuwa hakitashidwa kumpata mwenyekiti wa halmashauri anayetoka katika chama chake.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Katika kinyang’anyiro hicho, CCM imemteua Anju Mang’ola, Diwani wa Kata ya Ghehandu atakayepambana na Lori katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Desemba 17, mwaka huu.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 31, mwaka huu, CCM ilishinda viti 13 vya madiwani huku Chadema ikinyakua viti 11, Chama cha Wananchi (CUF) kiti kimoja.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Lori alisema licha ya kuwepo kwa tofauti hiyo ndogo anaamini kuwa mtandao walionao na kampeni iliyopo hivi sasa lolote linaweza kutokea kwa madiwani wa kambi ya CCM kumpa kura za ndiyo mgombea wa Chadema ikiwemo na kura moja kutoka CUF.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema matokeo hayo yatawashangaza wengi hasa wanaCCM na kudai kuwa hayo yatatokana na kuwepo kwa uelewa wa madiwani na mabadiliko yaliyopo kwa madiwani waliochaguliwa mwaka huu.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Lakini kwa upande wake. Katibu wa CCM wa Wilaya ya Hanang, Marco Thasara, alisema anamini kila diwani alichaguliwa na wananchi kwa kura na imani kubwa kwao na kuwa hakuna diwani atakayekidhalilisha chama chake na kuhujumu kura yake.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]"Matambo, majigambo na utabiri wa mgombea wa Chadema ni kujifurahisha tu na ana imani kuwa CCM ndiyo itakayoendelea kuongoza halmashauri hiyo licha ya kuwepo kwa madiwani wa Chadema na CUF,” alisema.[/FONT]
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom