tikatika
JF-Expert Member
- May 6, 2011
- 2,330
- 4,119
Ndugu wanajamvi nauliza kwa masikitiko makubwa sana juu ya hili!!
Jana raisi kasema anatafuta na kupora sukari toka kwa watu binafsi, NANI ATAMKATAZA??
Hebu tujiulize kidogo , tamko la kusitisha sukari toka nje limetolewa tar 8 mwez wa 3 na yeye mwenyewe!!
Ni takribani mwezi mmoja na siku kumi!! Kwanza huku ni kufeli kwake yeye binafsi, haiwezekani mkuu wa nchi utoe tamko ndani ya mwezi mmoja lizae matokeo tofauti, kwa lugha rahisi alitudanganya kwamba sukari ipo ya kutosha bila kujali yeye naye alidanganywa!!
Yeye alipoona mkuu wa mkoa kadanganywa alimtimua, sasa kwa hili nani wa kutimuliwa?
Swali ni tani elfu 4 huku elfu tatu na kule 3500 zinazalishwa na viwanda kwa muda gani?
Hivi unaweza kuikusanya sukari tani elfu 4 kwa muda gani ? roli moja ni wastan tani 30 , kwa tan 4000 ni maloli karibu 133 , hayo maroli yatakuchukua siku ngapi kuyasafirisha na kupakua gharani?
Hoja yangu ni kwamba hii sukari imeanza kukusanywa hata kabla ya tamko lake , then mfanyabiashara anaisambaza kutegemea na wateja wake na mahitaji yao.
Pia tukumbuke mfumo wa ujamaa tumeubomoa , wafanyabiasha wako huru kuagiza kwa kadri ya waonavyo wao, hivi leo nchi ikiishiwa unga mtaenda Azamu kumdhulumu eti kahifadhi unga mwingi?
Sasa tunafukuza wafanyabiashara wakubwa na kukaribisha wamachinga pekee!! Sijaona biashara ya jumla isiyo na stoo mimi!!
Hawa watu wakipolwa sukari wataenda mahakamani na watashinda tu!!
Je? HAKUNA WA KUMKATAZA RAIS AACHE HAYO?
Hakuna askofu wala jaji si umoja wa wafanyabiashara kila mtu anamuogopa JPM.
Nakulilia Tanzania!!!