Mheshimiwa rais anatumia nguvu kubwa sana kupingana na ukweli kwamba nchi hii kwa sasa inakabiliwa na njaa hasa kutokana na ukame.
Rais anasema hakuna njaa kwamba yeye ndio anajua kama kuna, hivi rais anaweza kujua kama mwananchi wa huko vijijini vya ndani amelala au hana chakula.
Kwanini anatumia nguvu kubwa kupingana na ukweli huu hasa ikitokana kwamba hata bei ya vyakula imepanda na hiyo ni kiashiria kimojawapo kwamba kuna njaa, nani atamlaumu rais kutokana na nchi kukumbwa na tatizo la njaa. Tatizo la njaa ni la kisiasa? Mpaka lazima atumie nguvu kubwa kupinga kwamba hamna njaa ili hali sisi wananchi wa kawaida tunaona hali halisi.
Kwanini rais asitumie nafasi aliyonayo kutoa tahadhari ya njaa baadala ya kupinga na kuwapa nafasi wafanyabiashara kuwauzia bei ghali chakula wananchi wanyonge walio lima mazao yao yakafa kwa ukame.