Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 8,936
- 6,846
Marehemu Kijazi aliteuliwa kuwa balozi akiwa mtumishi wa umma. Kabla ya kuwa balozi, alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na kabla ya hapo alishika nyadhfa mbalimbali kama mhandisi.Hawa wenzetu ni watu wa ajabu sana, hawana facts wao ni ushabiki wa hovyo tu
Uteuzi wa balozi Dr Bashiru Ally kuwa katibu mkuu kiongozi, uko sawa kabisa hakuna kifungu chochote cha katiba kilichovunjwa
Ndio maana mheshimiwa Rais alianza kwa kumteua kuwa balozi ( mtumishi wa umma) na hata kuapa leo alianza kuapa kwanza kuwa balozi na ndipo baadaye akaapa kuwa chief secretary( Katibu Mkuu Kiongozi)
Na hii sio mara ya kwanza kwa balozi kuteuliwa kuwa katibu mkuu kiongozi
Mheshimiwa Rais wa awamu ya nne, Dr Jakaya Kikwete, alimteua balozi Ombeni Sefue kuwa katibu mkuu kiongozi , akiwa balozi wa Tanzania nchini Marekani
Mheshimiwa Rais Dr John Pombe Magufuli, alimteua balozi Injinia John Kijazi kuwa katibu kiongozi, akiwa balozi wa Tanzania nchini India
Sasa iweje leo kwa balozi Dr Bashiru Ally kuteuliwa kuwa katibu kiongozi ndio iwe ajenda????
Amandla...