ubongokid
JF-Expert Member
- Apr 30, 2017
- 2,030
- 3,908
Kwa hakika hakuna lenye mwanzo lisilokuwa na mwisho.
Nimekaa na kutafakari yanayotokea sasa nchini, watu wanakufa bila kuwa na hatia. Mfano, mama mzazi wa Kabendera. Watu wanakufa wakiwa na uchungu moyoni, watu wanakufa bila kutarajia, watu wanapotezwa, watu wanawekwa jela bila haki, watu wanatishwa na kudhulumiwa haki zao. Watu wanaminywa uhuru wa maoni yao na haki ya kusema.
Tunaanza mwaka mpya hata hatutakiani heri ya sikukuu. Kweli kwa siku kama ya leo kweli tunashindwa kutakiana baraka kwa sababu ya hofu na vitisho?
Tanzania nchi yangu nini kimekupata? Ipo wapi Tanzania ambayo katika umaskini wetu tulifurahi pamoja, ipo wapi Tanzania ambayo katika tofauti yetu tulipendana? Ipo wapi Tanzania ambayo kila alikuwa na ndoto na ndoto zilitimia? Ipo wapi Tanzania nchi ya maziwa na asali?
Tanzania nchi yangu nini kimekupata?Kwa nini watu wako wanalia na kusaga meno?Kwa nini watu wako wanakula kwa mashaka na kuishi kwa hofu kama digi digi,Wenye kosa na wasio na kosa wote wana mashaka.Huwezi kupiga hadithi na kusimulia yanayojiri unaitwa mchochezi.Huwezi kufanya lolote bila hofu ya kupotezwa.
Matajiri wanaishi kama mafukara, mafukara wanaishi kama mateka na watumwa -- kila mtu ana hofu. Aliye mezani na aliye jikoni wote wanalia njaa.Tanzania nchi yangu nini kimekupata?
Kwanini Tanzania umekuwa dhalimu kwa watu wako? Kwanini sasa tuwe na hofu na mashaka? Watoto wetu hawawezi kusema chochote. Watoto wetu hawana ndoto, wazee wetu hawana maono. Tumekuwa taifa la waoga, wanafiki wasio na matumaini.Tunaishi kama ndege awindwaye.
Tanzania nchi yangu nini kimekupata? Kwa nini mashujaa wako wamenywea? Kwanini wasomi wako wamefunga akili zao? Kwanini wachapa kazi wako wanapiga uvivu? Kwanini wakuu wako waoneana kijicho. Tanzania nchi yangu umepatwa na nini?
Ni nani aliyewaloga Watanzania? Ni nani atakuwa wa mwisho kufa? Wa mwisho kupotea?
Tanzania,Tanzania, nakupenda kwa moyo wote!