Nani atakuwa wa mwisho kufa? Nani atakuwa wa mwisho kwenda Gerezani? Nani atakuwa wa mwisho kuisoma namba?

ubongokid

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Messages
1,814
Points
2,000

ubongokid

JF-Expert Member
Joined Apr 30, 2017
1,814 2,000
Kwa hakika hakuna lenye mwanzo lisilokuwa na mwisho.

Nimekaa na kutafakari yanayotokea sasa nchini, watu wanakufa bila kuwa na hatia. Mfano, mama mzazi wa Kabendera. Watu wanakufa wakiwa na uchungu moyoni, watu wanakufa bila kutarajia, watu wanapotezwa, watu wanawekwa jela bila haki, watu wanatishwa na kudhulumiwa haki zao. Watu wanaminywa uhuru wa maoni yao na haki ya kusema.

Tunaanza mwaka mpya hata hatutakiani heri ya sikukuu. Kweli kwa siku kama ya leo kweli tunashindwa kutakiana baraka kwa sababu ya hofu na vitisho?

Tanzania nchi yangu nini kimekupata? Ipo wapi Tanzania ambayo katika umaskini wetu tulifurahi pamoja, ipo wapi Tanzania ambayo katika tofauti yetu tulipendana? Ipo wapi Tanzania ambayo kila alikuwa na ndoto na ndoto zilitimia? Ipo wapi Tanzania nchi ya maziwa na asali?

Tanzania nchi yangu nini kimekupata?Kwa nini watu wako wanalia na kusaga meno?Kwa nini watu wako wanakula kwa mashaka na kuishi kwa hofu kama digi digi,Wenye kosa na wasio na kosa wote wana mashaka.Huwezi kupiga hadithi na kusimulia yanayojiri unaitwa mchochezi.Huwezi kufanya lolote bila hofu ya kupotezwa.

Matajiri wanaishi kama mafukara, mafukara wanaishi kama mateka na watumwa -- kila mtu ana hofu. Aliye mezani na aliye jikoni wote wanalia njaa.Tanzania nchi yangu nini kimekupata?

Kwanini Tanzania umekuwa dhalimu kwa watu wako? Kwanini sasa tuwe na hofu na mashaka? Watoto wetu hawawezi kusema chochote. Watoto wetu hawana ndoto, wazee wetu hawana maono. Tumekuwa taifa la waoga, wanafiki wasio na matumaini.Tunaishi kama ndege awindwaye.

Tanzania nchi yangu nini kimekupata? Kwa nini mashujaa wako wamenywea? Kwanini wasomi wako wamefunga akili zao? Kwanini wachapa kazi wako wanapiga uvivu? Kwanini wakuu wako waoneana kijicho. Tanzania nchi yangu umepatwa na nini?

Ni nani aliyewaloga Watanzania? Ni nani atakuwa wa mwisho kufa? Wa mwisho kupotea?

Tanzania,Tanzania, nakupenda kwa moyo wote!
 

Billie

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2011
Messages
10,069
Points
2,000

Billie

JF-Expert Member
Joined Aug 13, 2011
10,069 2,000
Kila mtu anateseka kinamna yake watu hatuna furaha,tunakunywa bia haziingii kichwani,tunahofu ya kutekwa ama kupotezwa.

Maoni na malalamiko siku hizi yanaitwa uchochezi,Upinzani wanakatazwa kupinga(ndo kazi yao ni sawa na kumzuia mbwa kubweka), KOSA LOLOTE LINAANGUKIA KWENYE UHUJUMU UCHUMI NA UTAKATISHAJI PESA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

kizaizai

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2010
Messages
3,489
Points
2,000

kizaizai

JF-Expert Member
Joined Mar 31, 2010
3,489 2,000
Kila mtu anateseka kinamna yake watu hatuna furaha,tunakunywa bia haziingii kichwani,tunahofu ya kutekwa ama kupotezwa.
Maoni na malalamiko siku hizi yanaitwa uchochezi,Upinzani wanakatazwa kupinga(ndo kazi yao ni sawa na kumzuia mbwa kubweka),KOSA LOLOTE LINAANGUKIA KWENYE UHUJUMU UCHUMI NA UTAKATISHAJI PESA.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nilikuwa sehemu napata Bieree, Meneja kaweka taarifa ya habari, mara Jiwe huyo anaongea, msela mmoja aliyekolea kilevi akasema mnamuona Magu Boy.. watu wote wakageuka kumcheki hakuna aliyemjibu wakabaki kuangaliana. Watu hawaaminiani tena.
 

erythroccyzed

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2019
Messages
307
Points
250

erythroccyzed

JF-Expert Member
Joined Jul 13, 2019
307 250
Ata uchaguzi huu atapita kwa mkono wa chuma
Nilikuwa sehemu napata Bieree, Meneja kaweka taarifa ya habari, mara Jiwe huyo anaongea, msela mmoja aliyekolea kilevi akasema mnamuona Magu Boy.. watu wote wakageuka kumcheki hakuna aliyemjibu wakabaki kuangaliana. Watu hawaaminiani tena.
 

Forum statistics

Threads 1,391,830
Members 528,473
Posts 34,090,699
Top