G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Kwakweli huu mradi kila nikiuangalia na complications zake huwa nakuna kichwa sana na kujiuliza kina nani walipendekeza mradi wa aina hii?
Pamoja na usanifu wake kujikita kwenye gharama za juu bado sijawahi kuona faida ya mradi huu na sijui kama utakuja kukamilika. Mbaya zaidi umeshatushinda kuuendeleza kwa wakati.
Kiukweli nchi yetu ni masikini sana na hakukuwa na tija yoyote kubuni mradi ambao utakula zaidi ya trilioni 7 Tshs fedha za awali huku ukiwa hauna maana kwa nchi.
Hivi ni mizigo kiasi gani itakayo kuwa inapita kwenye hiyo reli hadi tuigharamie hivyo?
Bomba la mafuta limefeli na sasa Uganda ameamua kuegemea Kenya zaidi, serikali yetu bado haijatueleza ni kwanini? Huu mradi utakuwa unatumiwa na watu wa kanda ya ziwa kusafirisha matikiti maji?
Yani Rais Magufuli kwakuwa ana nguvu ya kutumia fedha za nchi basi amekuwa akizitumia kwa utaratibu mbovu kweli.
Sioni pia tija kwenye daraja la coco beach baada ya serikali kuhamia Dodoma, sioni tija yoyote kwenye daraja la huko sijui busisi kanda ya ziwa dah yani watanzania wengi wanataabika ili kugharamia miradi isiyo na tija yoyote ile.