Nani atakayeokoa tume ya nguvu za atomiki Tanzania

Feb 3, 2018
13
6
NANI ATAKAYEOKOA TUME YA NGUVU ZA ATOMIKI TANZANIA

Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania ni Taasisi ya serikali iliyoundwa kwa sheria ya Nguvu za Atomiki Na. 7 ya mwaka 2003. Tume hii inayo majukumu makubwa mawili yakiwa ni kusimamia matumizi salama ya vifaa vyote vinavyotoa mionzi ayonisha na isiyoayonisha kwa ajili ya usalama wa wagonjwa, wafanyakazi, wananchi na mazingira kwa ujumla na kuishauri serikali matumizi ya teknolojia ya nyuklia kwenye maeneo mbalimbali kwa ajili ya maendeleo endelevu ya Taifa.

Itakumbukwa kwamba mnamo Juni 2016 Mkurugenzi Mkuu wa Tume hii Prof. Iddi Nyangarika Mkilaha alifariki kwa kujipiga risasi nyumbani kwake jijini Dar es salaam na kufanya Tume kuongozwa na kaimu Mkurugenzi Mkuu aliyekuwa ameteuliwa na Bodi ya Wakurugenzi ya Tume mpaka Septemba 2016 ambapo Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ilipoleta Kaimu Mkurugenzi Mkuu kutoka Jeshi la Wananchi Brigedia Jenerali Fulgence Simon Msafiri kukaimu nafasi hiyo mpaka sasa.

Ijulikane wazi kuwa tangu kupewa nafasi ya kukaimu Mkugenzi huyu Mkuu sasa ni zaidi ya mwaka mmoja kama inavyojieleza hapo juu. Mkurugenzi huyu amekuwa akifanya mabadiliko mbalimbali katika Tume ambayo mengi ya mabadiliko hayo yamekuwa ni kwa manufaa yake binafsi pamoja na baadhi ya viongozi ambao amekuwa akiambatana nao katika kufanya maamuzi ambayo yamekuwa yakiumiza Taasisi pamoja na wafanyakazi na kuwapunguzia morali za kufanya kazi hii ikiwa ni pamoja na kuhamisha wafanyakazi na wengine kuwafukuza kazi bila hata sababu za msingi na kufuata taratibu za utumishi wa umma.

Aidha yapo mambo ambayo wanaohusika na usimamizi wa TUME hii muhimu kwa maendeleo na usalama wa Taifa katika matumizi ya teknolojia ya nyuklia wanatakiwa kuyangalia kwa ukaribu ili kuifanya Tume hii itimize majukumu yake ya msingi katika ofisi zake ambazo ni Arusha Makao Makuu, Dar es salaam, Zanzibar, Mpaka wa Namanga, Mpaka wa Sirali, Ruvuma, Mtwara,Mpaka wa Holili, Mpaka wa Tarakea, Mpaka wa Tunduma, Mpaka wa Rusumo, Mpaka wa mutukula, Mpaka wa Horohoro na Bandari ya Tanga. Ijulikane pia kuwa ukiacha ofisi ya Makao makuu na Ruvuma ofisi zingine zote zinajishughulisha zaidi na usimamizi wa viwango vya mionzi kwenye vyakula vya binadamu na mifungo ambavyo vinaingizwa na kutolewa nje ya nchi ambayo ni sehemu ndogo ya majukumu ya msingi ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania.

Yapo mambo ambayo ni vizuri kuyaonyesha ambayo yanaendelea katika TUME ili wanahusika waweze kuyafanyia kazi kama itapendeza ni kama ifuatavyo

i. Mahusiano ya kiutendaji kati ya Menejimenti na Wafanyakazi,

ii. Uwepo wa chama cha wafanyakazi na uanachama wa wafanyakazi,

iii. Kutokufanyika kwa vikao vya Baraza la Wafanyakazi,

iv. Fukuza fukuza ya wafanyakazi kwa makosa ya kusingiziwa

v. Mahusiano ya kiutendaji kati ya Menejimenti na Bodi ya wakurugenzi, na

vi. Uhamisho wa wafanyakazi usio na tija

vii. Ufisadi ndani ya Tume

Mahusiano ya kiutendaji kati ya Menejimenti na Wafanyakazi

Kumekuwa na mahusiano mabaya na uoga kati ya watumishi wa Tume na timu ndogo ya menejimenti (Kaimu Mkurugenzi mkuu, Mkurugenzi wa utawala na fedha na Mwanasheria wa Tume) na wafanyakazi wengine kwamba wafanyakazi wanatakiwa kufanya lile ambalo hawa wanalitaka liwe vinginevyo utakuwa mhanga katika utumishi wako katika tume hii. Hili limepelekea mpaka hata vikao vya mikutano kati ya wafanyakazi na Menejimenti vimekuwa ni vya maagizo tu na hakuna kutoa mawazo wala kuuliza swali ukifanya hivyo unakuwa unatafuta tatizo katika utumishi wako. Aidha imepelekea hata wageni wa wizara wanapotembelea TUME hii kukosa kujua ukweli wa hali ya TUME maana ripoti za uongo zimekuwa zikitolewa kuwa mahusiano kati utawala na wafanyakazi ni mazuri na akitokea mfanyakazi akauliza swali katika ugeni huo basi atengemee mambo mawili kuhamishwa makao makuu au kufukuzwa kazi. Jambo hili limechangiwa kwa sehemu kubwa na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia hususani Naibu Katibu Mkuu (Sayansi) ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila ambaye alitoa maelekezo yasiyo sahihi kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu. Tunaomba Wizara iliangalie upya suala hili katika Tume ili kufanya tume ifanye kazi kwa mafanikio na kurejesha morali ya wafanyakazi ya kufanya kazi kwa ufanisi na si kwa vitisho ambavyo vinaendelea ambavyo havina tija kwenye Tume na Taifa kwa ujumla. Tunashauri uchunguzi ufanyike ubaini ukweli wa jambo hili.

Uwepo wa chama cha wafanyakazi na uanachama wa wafanyakazi

Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania ni moja ya Taasisi za utafiti na zinazojishughulisha na mambo ya Sayansi na Teknolojia ikiwepo ukaguzi wa vifaa na majengo yanayotumika vifaa vinavyotoa Mionzi ya Nguvu za Atomiki (geji zinazotumika katika utafiti wa madini na gesi, mashine za uchunguzi na matibabu ya kansa kwa mionzi, mashine za X-ray, mashine za CT na mashine zinazotumika viwandani na katika matengenezo ya barabara ambazo zinatoa mionzi, n.k) hivyo kuifanya wafanyakazi wake kuwa chini ya Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu, Sayansi, Teknolojia, Ufundi Stadi, Habari na Utafiti (RAAWU). Tangu Kaimu Mkurugenzi Mkuu aanze kazi Septemba 2016 amekuwa akifanya kazi ya kuwatoa wafanyakazi kwenye chama cha wafanyakazi kwa kigezo cha kuwapa madaraka ya ukuu wa Idara, Vitengo na Ukurugenzi. Jambo ambalo UTUMISHI kupitia nyaraka mbalimbali lilishatolewa maelekezo katika utekelezaji wako. Hili lilifanya viongozi wa chama cha wafanyakazi Tawi, Mkoa, Kanda na Taifa kumshauri Kaimu Mkurugenzi Mkuu kutokuwatoa wafanyakazi katika chama kwa kuwa ni haki yao ya msingi ila tu pale anapowateua kwa nafasi ya uongozi katika taasisi basi waache nafasi za uongozi katika chama na kutumikia nafasi zao za uteuzi lakini waendelee kuwa wanachama wa chama cha wafanyakazi kwa mujibu wa sheria. Pamoja na ushauri huo Kaimu Mkurugenzi Mkuu hakuwa tayari kubadili msimamo wake wa kuwatoa wafanyakazi kwenye chama jambo ambalo lilifanya aingie kwenye mgogoro na viongozi wa Tawi wa chama cha wafanyakazi kwa kuwahusisha na tuhuma ambazo sio za kweli ikafikia wengine kuwahamisha kutoka kwenye Tume na viongozi wengine kuwaondoa makao makuu na kuwapeleka ofisi za kanda na mipakani kama adhabu. Moja ya viongozi walihamishwa katika Tume ni Katibu wa Chama Tawi ambaye alihamishwa mwezi Aprili 2017. Mahusiano mabaya na chama hayakuishia hapo bali yaliendelea mpaka ilipofika mwezi Oktoba 2017 alimfukuza kazi Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi kwa kosa la kutumia simu ya ofisi kwa mawasiliano na wafanyakazi katika kutimiza majukumu yake ya Chama cha wafanyakazi. Kutokana na unyanyasaji huu kwa viongozi wa chama cha wafanyakazi viongozi wengine wa chama katika Halmashauri ya Chama Tawi waliomba kuachia nafasi zao za uongozi na kubaki wanachama wa kawaida ili kuepusha migongano katika Tume. Mpaka tarehe ya ujumbe huu kuanzia Oktoba 2017 hakuna kiongozi hata mmoja wa chama cha wafanyakazi maana mwenyekiti ndio alibaki ambaye amefukuzwa kazi. Kutokana na mgogoro huo hakujafanyika kikao chochote cha Baraza la Wafanyakazi tangu Aprili 2017 mpaka sasa na nyaraka mbalimbali zimelazimishwa kupitishwa bila ushiriki wa baraza la wafanyakazi. Hili pia wanaohusika na usimamizi wa utendaji wa TUME wanaweza kulifuatilia na kujua ukweli wake.

Kutokufanyika kwa vikao vya Baraza la Wafanyakazi

Kaimu Mkurugenzi Mkuu amekuwa akiendesha Tume bila kuwepo kwa vikao vya mabaraza ya wafanyakazi kutoka mwezi Aprili 2017 alipofanya kikao cha mwisho kwa dakika tatu (3) na kuwalipa wajumbe zaidi ya Ishirini na Tano (25) kila mmoja 150,000/= ambayo kwa upande mmoja yalikuwa ni matumizi mabaya ya fedha ya serikali ila kwa kuwa kulipa au kutokulipa ni maamuzi yake na timu yake hili lilifanyika. Vikao hivyo vya Baraza havijafanyika mpaka sasa ni zaidi ya vikao vitatu kutokana na mgogoro wa kutokutaka chama cha wafanyakazi katika Tume. Hali kadhalika jambo hili linaweza kufanyiwa uchunguzi wa kina ili kujua ukweli wake na wahusika wenye dhamana ya kusimamia utendaji wa Tume. Ijulikane wazi kwamba kuwa kutokufanyika vikao hivi ni kupunguza ushirikishwaji wa wafanyakazi katika utendaji kazi wa Tume na kujua mwenendo wa utendaji kazi na matumizi ya Tume kwa ujumla na kupunguza uwajibikaji kwa viongozi wa Tume.

Mahusiano ya kiutendaji kati ya Menejimenti na Bodi ya wakurugenzi

Kila taasisi ya serikali ikiwa ni pamoja na Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania inasimamiwa na Bodi ya wakurugenzi katika kutimiza majukumu yake. Naomba ijulikane wazi kuwa kumekuwa na mahusiano yasiyo sawia kati ya Menejimenti ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania inayoongozwa na Brigedia Jenerali Fulgence Msafiri kwa zaidi ya miezi mitano na Bodi ya wakurugenzi ya Tume ambayo imepelekea kutokufanyika kwa vikao vya Bodi ya wakurugenzi tangu kikao cha mwisho kilichokaliwa mwezi Julai 2017. Kwa kawaida vikao vya bodi za wakurugenzi hutanguliwa na vikao vya Baraza la wafanyakazi lakini kikao hiki kilifanyika bila vikao vya Baraza kutokana na mahusiano mabaya kati ya menejimenti ya Tume na uongozi wa chama cha wafanyakazi ambapo Mkurugenzi mkuu amehamisha viongozi wote na kuwafukuza kazi viongozi wa chama cha wafanyakazi katika Tume. Tunaomba wanaohusika kufanya uchunguzi wa mahusiano kati ya Bodi na Menejimenti ya Tume hii ili kuokoa Tume hii iweze kutimiza majukumu yake ya kisheria kwa kulinda, kusimamia matumizi salama ya nguvu za Atomiki Tanzania kwa wagonjwa, wafanyakazi , wananchi na mazingira kwa ujumla.

Uhamisho wa wafanyakazi usio na tija

Ukirejea maelezo ya awali kwenye utangulizi utakumbuka kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyu amehamishiwa Tume kuanzia mwezi Septemba 2016. Kuanzia mwezi Novemba 2016 kumekuwa na uhamisho usio wa kawaida na tija kwenye Tume na Taifa, aidha wafanyakazi na wengine kufukuzwa kazi kwa sababu zisizokuwa na msingi wowote. Naomba nitoe mfano wa mkaguzi mkuu wa ndani kuhamishiwa ofisi ya Zanzibar kuwa mhasibu wa kawaida kwa kuhoji na kuibua maovu ya menejimenti hii ya watu watatu. Wafanyakazi wawili waliofukuzwa kazi katika kipindi hiki, Mfanyakazi Mmoja ni dereva ambaye alifukuzwa kazi kwa kosa la kuendesha gari akiwa na leseni iliyokwisha muda wa matumizi bila onyo lolote. Mfanyakazi wa pili ni mhudumu wa ofisi ambaye pia ni Kaimu Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi ambaye alifukuzwa kazi kwa kosa la kupigia simu wafanyakazi wenzake watatu kupitia kwa mhudumu anayeruhusu kupiga simu za nje ya Tume bila onyo lolote, hii ni mifano tu ya wafanyakazi waliofukuzwa kazi mpaka sasa. Ifahamike kuwa Tume hii imekuwa na upungufu wa wafanyakazi kwa miaka mingi tangu kuanzishwa kwake na pia upungufu wa fedha za kufanyia kazi, aidha kwa kipindi mpaka oktoba 2017 Mkurugenzi huyu amehamisha zaidi ya wafanyakazi kumi na tano ndani ya vituo vya kazi vya Tume na wafanyakazi watatu nje ya Taasisi. Hivi sasa Tume ina mradi mkubwa wa ujenzi wa Maabara baada ya kupata msaada wa vifaa vya kisasa kutoka Umoja wa Ulaya (European Union). Pamoja na vifaa hivyo, umoja huo wa ulaya ulitoa mafunzo kwa baadhi ya wafanyakazi wa Tume ili kuboresha usimamizi wa matumizi salama ya nguvu za atomiki, lakini baadhi ya wafanyakazi hao wamehamishiwa nje ya Tume huku uongozi ukidai kuwepo kwa upungufu wa wataalamu katika kutekeleza majukumu yake. Tunaomba pia wanaohusika na usimamizi wa Tume hii kufanya uchunguzi wa tija wa uhamisho huu wa wafanyakazi kwa Tume na Taifa kwa ujumla.

Mambo haya yote yamefanya wafanyakazi wa Tume kufanya kazi katika mazingira magumu na wasiwasi na hivyo kupunguza ufanisi wa kazi zao za kila siku. Bidii za makusudi zifanyike na wahusika pamoja na wizara husika kuiponya Tume hii. Kwa kufanya ukaguzi na uchunguzi wa mambo hayo yapo mambo mengine yanayoweza kujulikana kwa kuwa maamuzi mengi katika Tume yanafanyika kwa maslahi ya kundi dogo la wenye maslahi na maamuzi hayo kuhusu wafanyakazi.

Ufisadi ndani ya Tume ya Nguvu za Atomiki

Baada ya ziara ya Waziri Joyce Ndalichako mapema 2017, gazeti la Habari Leo la 3 Aprili 2017 liliandika “Ndalichako anusa ufisadi tume ya nguvu ya atomiki”. Ikumbukwe kwamba pamoja na mambo yote yaliyotangulia kusemwa hapo juu timu hii hii ya watu watatu imekua ikichukua fedha za serikali na kuzielekeza kwenye mifuko yao binafsi kwenye manunuzi mbalimbali mfamo magari, hongo kwa wageni ,kujinunulia likizo zao bila ulazima wowote, kumtengenezea kaimu mkurugenzi mkuu safari zisizo na tija ikiongozwa na ofisi ya mwanasheria wa Tume na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala ambao ndio maswaiba wa Brigedia Jenerali Fulgency Simon Msafiri. Kitengo cha upimaji wa vyakula ndicho kinaongoza kwa mapato japo ukaribu wa mwanasheria wa Tume na Mkuu wa kitengo cha upimaji wa sampuli za vyakula una ishara ya ufisadi. Vilevile kumuweka mwanadada mchumi ambae hana uwezo kwenye kitengo cha fedha na mipango ili waweze kudhibiti wanapofanya ufujaji. Yapo mambo mengi ambayo tunaamini yakichunguzwa Tume ya Nguvu za Atomiki itakombolewa na kufikia malengo ya serikali ya awamu ya tano ya uchumi wa viwanda

WAFANYAKAZI TUME YA NGUVU ZA ATOMIKI TANZANIA

Sehemu ya pili: ===>> Nani atakayeokoa tume ya nguvu za atomiki Tanzania

Sehemu ya tatu: ===>> Nani atakayeokoa tume ya nguvu za atomiki Tanzania
 
Aisee, ila naona mna vidalili vya uoga. Kama mliyoandika yana msingi ni bora muite press au mumuandikie Waziri moja kwa moja. Kusema tu ni wafanyakazi mumeandika wakati mtoa mada hata id yako ni fake inafanya hizi tuhuma kupungua Nguvu. Hivi kwa mfano leo hii Rais au Waziri akiwaita mzungumzie kwa kina waraka wenu sijui mtajitokeza wangapi. Nauona uoga umewajaa. Jilipueni kwenye media. Lakini kwa upande mwingine kwa nini kuwe na kaimu DG muda wote huo.. Je, Huyo Mjeshi ana taaluma ya mionzi? Mi nadhani atafutwe DG aliyebobea katika matumizi ya mionzi alitumikie taifa letu. Changamoto za matumizi ya mionzi ni nyingi kwa kipindi hiki. Serikali iingilie kati haya matatizo ya taasisi hii nyeti kwa usalama wa raia katika matumizi ya vyanzo mbalimbali vya mionzi.
 
Huu waraka ni mzito kama ni kweli na sio chuki na fitina. Kwa nini msiandike majina yenu tuwatafute kwa kupata details ili tufanyie kazi? Mmesema wafanyakazi, wangapi? Tum contact nani? Acheni uoga kwenye kudai haki.
 
Ikumbukwe kwamba pamoja na mambo yote yaliyotangulia kusemwa hapo juu timu hii hii ya watu watatu imekua ikichukua fedha za serikali na kuzielekeza kwenye mifuko yao binafsi kwenye manunuzi mbalimbali mfamo magari, hongo kwa wageni ,kujinunulia likizo zao bila ulazima wowote, kumtengenezea kaimu mkurugenzi mkuu safari zisizo na tija ikiongozwa na ofisi ya mwanasheria wa Tume na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala ambao ndio maswaiba wa Brigedia Jenerali Fulgency Simon Msafiri. Kitengo cha upimaji wa vyakula ndicho kinaongoza kwa mapato japo ukaribu wa mwanasheria wa Tume na Mkuu wa kitengo cha upimaji wa sampuli za vyakula una ishara ya ufisadi. Vilevile kumuweka mwanadada mchumi ambae hana uwezo kwenye kitengo cha fedha na mipango ili waweze kudhibiti wanapofanya ufujaji. Yapo mambo mengi ambayo tunaamini yakichunguzwa Tume ya Nguvu za Atomiki itakombolewa na kufikia malengo ya serikali ya awamu ya tano ya uchumi wa viwanda

Will soon be no longer at ease
 
Mamlaka husika kama Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia ambayo inasimamia Tume, Ofisi ya Rais, TAKUKURU na wengineo wakichunguza watapata majibu watu wako tayari kutoa ushirikiano hilo halina shaka yoyote na ushahidi upo.
 
Aisee, ila naona mna vidalili vya uoga. Kama mliyoandika yana msingi ni bora muite press au mumuandikie Waziri moja kwa moja. Kusema tu ni wafanyakazi mumeandika wakati mtoa mada hata id yako ni fake inafanya hizi tuhuma kupungua Nguvu. Hivi kwa mfano leo hii Rais au Waziri akiwaita mzungumzie kwa kina waraka wenu sijui mtajitokeza wangapi. Nauona uoga umewajaa. Jilipueni kwenye media. Lakini kwa upande mwingine kwa nini kuwe na kaimu DG muda wote huo.. Je, Huyo Mjeshi ana taaluma ya mionzi? Mi nadhani atafutwe DG aliyebobea katika matumizi ya mionzi alitumikie taifa letu. Changamoto za matumizi ya mionzi ni nyingi kwa kipindi hiki. Serikali iingilie kati haya matatizo ya taasisi hii nyeti kwa usalama wa raia katika matumizi ya vyanzo mbalimbali vya mionzi.

Imagine kuna aliyekua mfanyakazi wa Tume na Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wakati huo kabla hajahamishiwa kuwa mwalimu wa chuo aliwahi kuongea mbele ya Waziri na waandishi wa habari kuhusu mambo yanayoendelea ndani ya Tume lakini kilichofuata anajua ni kumhamisha na hamna hatua zozote zilizochukuliwa.
 
DSC_0361.JPG
Ndugu watanzania, wafanyakazi wa Tume ya Nguvu za atomiki Tanzania -TAEC tunatoa shukrani zetu kwenu kwa kusoma waraka wetu wa sehemu ya kwanza ya Nani atakayeiokoa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania”. Usomaji wenu umekuwa ni mchango mkubwa wa mabadiliko katika Tume yetu. Kwa nia ya pekee tuwashukuru wasimamizi wa Tume hii katika ngazi zote yaani Bodi ya wakurugenzi, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa hatua za makusudi mlizoanza kuzichukua kwa malalamiko ambayo wafanyakazi wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania tuliyatoa katika waraka wa kwanza. Mabadiliko tuliyoanza kuyaona ni pamoja na kuanza kuwepo kwa vikao vya Bodi ya wakurugenzi ambacho kilifanyika tarehe 8/2/2018 makao makuu ya Tume, Arusha Tanzania na kikao cha Menejimenti ya Tume kilichopewa jina la kikao cha maandalizi ya Baraza la Wafanyakazi yaani Executive Committee tarehe 9/2/2018.

Kama tulivyoeleza katika waraka wa awali vikao vya mwisho vya mabaraza ya wafanyakazi vilifanyika mwezi Aprili, 2017 na vile vya Bodi ya wakurugenzi vilifanyika Julai, 2017. Ikumbukwe kwamba mabaraza ya wafanyakazi yanaundwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za kazi zinazotambua kuwepo kwa Serikali, Mwajiri na Wafanyakazi. Baraza la wafanyakazi linaundwa kwa makubaliano ya pamoja kati ya Mwajiri na Chama cha wafanyakazi eneo la kazi. Vikao vya baraza la wafanyakazi katika Tume vinakuwa na wajumbe wafuatao;

· Mwenyekiti na Katibu wa Baraza

· Wajumbe wa Menejmenti

· Viongozi wa Chama cha wafanyakazi

· Wakuu wa idara na vitengo na wakuu wa ofisi za kanda na mipakani

· Wawakilishi wa wafanyakazi kutoka katika idara.

· Mwakilishi wa vyama vya wafanyakazi kutoka ofisi ya chama Mkoa na wengine wanaoingia kwa mujibu wa nafasi zao kama vile afisa rasilimali watu kama hayupo kwenye makundi mengine hapo juu.

Tuombe kutoa ufafanuzi wa kikao cha Executive Committee kilichofanyika tarehe 09/02/2018 kwa malengo ya maandalizi ya kikao cha Baraza la wafanyakazi ili kupitisha ajenda za kikao cha Baraza na baadaye Baraza kuandaa ajenda za kikao cha Bodi ya wakurugenzi ambacho kinatarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Kikao cha Executive Committee kina wajumbe wa aina tatu kwa mujibu wa mkataba wa uundwaji wa Baraza uliosainiwa na Mkurugenzi Mkuu kwa niaba ya Menejimenti pamoja na upande wa Chama cha Wafanyakazi tawi la Tume nao ni;

· Mwenyekiti na Katibu wa Baraza

· Wajumbe wa Menejmenti ya Tume

· Mwenyekiti na Katibu wa Chama cha wafanyakazi

Kutokakana na kukosekana kwa Mwenyekiti na Katibu wa Chama cha wafanyakazi, Mwenyekiti wa Baraza ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu alijaribu kulazimisha wafanyakazi kuteua viongozi watakao wakilisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu wa Chama Cha Wafanyakazi katika kikao hicho. Zoezi hilo lilishindikana kwa kuwa hakuna hata kiongozi mmoja wa Chama kwa wakati huu kwa kuwa viongozi wengi wa Halmshauri ya Chama cha wafanyakazi upande wa tawi walijiuzulu kutokana na vitisho vya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume vilivyopelekea viongozi waliokataa kujiuzulu akiwemo katibu wa Chama Kuhamishwa katika Tume na Mwenyekiti kufukuzwa kazi katika Tume bila sababu ya msingi kwa kuwa tu viongozi wa Chama.

Hata hivyo mgogoro huu kati ya Menejimenti na Chama cha wafanyakazi ulifikishwa kwenye idara ya Kazi ngazi ya Mkoa wa Arusha kwa ushuluhishi na Viongozi wa Chama wafanyakazi ngazi ya Tawi na Uongozi wa Chama ngazi ya Mkoa wa Arusha lakini kwa masikitiko makubwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu na Menejimenti hawakuweza kufika katika idara ya usuluhisho pamoja na kuitwa zaidi ya mara tatu kuanzia Julai 2017 mpaka sasa. Tunaamini hili ndilo lilipelekea kutokuwepo kwa vikao vya Baraza katika Tume kwa kipindi chote. Hili linaweza kufanyiwa uchunguzi na wasimamizi wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania kujua ukweli wake. Japokuwa bidii zinafanyika na uongozi wa Tume kuhalalisha kikao hiki batili cha Baraza la wafanyakazi, tunaomba Bodi ya Wakurugenzi kuwa macho maana bajeti hii ina uwezekano wa kuletwa kwenye kikao tarajiwa cha Bodi bila kupitiwa na Baraza la wafanyakazi.

Tunazo taarifa ambazo zinasema kuwa baada ya kushindikana kufanyika kikao hicho cha tarehe 9/2/2018 bidii zinafanyika ili wafanyakazi waliokuwa wanachama wa Chama cha wafanyakazi waondolewe kwenye uanachama kwa kujengewa hoja kuwa hakuna faida wanayoipata kwenye chama cha wafanyakazi, hii ikiwa ni kama mwendelezo wa kuhakikisha kunakuwa hakuna chama cha wafanyakazi katika Tume. Jambo hili litafanyika kwa mtindo uleule uliofanyika kwa viongozi na wafanyakazi wengine waliokuwa na nyadhifa mbalimbali katika Tume ambao kwa sasa wamebaki bila kuwa na nyadhifa baada ya kubadilishwa. Ni vizuri wafanyakazi tukaelimishana kuwa Chama cha wafanyakazi ni umoja wa hiari na wa kidemokrasia unaoanzishwa na wafanyakazi wenyewe kutokana na mahitaji yao bila ya kushawishiwa na bila ya kuingiliwa na chombo chochote na ni kwa mujibu wa sheria za nchi. Tunaomba kwa pamoja tuwe na ushirikiano na mshikamano ikitokea una ulazima wa kuacha uanachama kwa jambo lolote basi omba maelekezo ili kufuata taratibu za kufanya hivyo isiwe kwa kulazimishwa na mtu yeyote.

Wafanyakazi tunaomba Bodi ya wakurugenzi ifanye kuchunguza sababu zilizopelekea Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi kufukuzwa kazi kwa kuwa zinauhusiano na mahojiano yake na Bodi hiyo katika kikao cha Bodi ya wakurugenzi kilichofanyika tarehe 18/07/2017. Mahojiano hayo yalipelekea Mwenyekiti kutafutiwa sababu mbalimbali ambazo hazina mashiko hadi alipofukuzwa kazi na Mkurugenzi wa fedha na utawala pamoja na kwamba kikao hicho cha Bodi kiliahidi kumlinda. Uchunguzi wa jambo hili utaibua mambo mengi yaliyojificha ambayo wafanyakazi tunayatolea malalamiko. Mambo haya tukiyauliza kwa viongozi wanaotembelea Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania iwe ni Waziri, Naibu Waziri na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara husika, baada ya wageni hao kuondoka huwa ni manyanyaso kwa wafanyakazi husika mpaka inapelekea kuhamishwa kutoka makao makuu kwenda vituo vya pembezoni mwa nchi au kufukuzwa kazi tunayo mifano ya matukio hayo ikiwemo mfano wa Katibu wa Chama cha wafanyakazi na viongozi wengine wa halmashauri ya Chama cha wafanyakazi.

Wafanyakazi wa Tume tupo tayari kuhojiwa na kutoa ushirikiano kwa uchunguzi wa mambo ambayo yametolewa kwenye waraka huu na ule wa awali pale ambapo tutahitajika ilimradi tukihakikishiwa usalama wa vitisho na usalama wa ajira zetu baada ya mahojiano hayo kutoka ofisi ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu pamoja shwahiba zake wakuu ambao ni mwanasheria na mkurugenzi wa fedha na utawala wa Tume.

Wafanyakazi tunatoa shukrani kwa hatua za haraka zilizoanza kuchukuliwa na wahusika japo kwa kweli vitisho vimeongezeka sana tangu waraka wa awali ulipotoka ila hatuwezi kukoma kutoa taarifa kwa kuwa maisha haya ya vitisho kwenye ajira zetu tunaendelea kuyazoea huku tunachapa kazi maana kwa kweli hapa ni kazi tu hakuna kurudi nyuma katika juhudi za kulijenga Taifa.

Imeandikwa na Wafanyakazi wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania
 
Hii sehemu ya pili imenishawishi kuitafuta sehemu ya kwanza,nimeisoma pia.
Nadhani Mamlaka husika zifanyie kazi haya malalamiko ya waliojiita Wafanyakazi, ili kubaini ukweli wa hayo mambo.
Waweza kuta ni majungu tu ya watu wachache kuuchafua uongozi uliopo.
 
Tuwashukuru tena wasomaji wetu wa nyaraka hizi za “Nani atakayeiokoa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania” kwa muda wenu mnaoutumia kusoma na kutusaidia kupeleka ujumbe wetu kwa wanaohusika na kuiokoa Tume hii. Kwa kweli mmekuwa msaada mkubwa maana wanaohusika kwa nafasi tofauti wameanza kuchukua hatua za awali kuiokoa Tume hii pamoja na ustawi wetu wafanyakazi. Aidha kumekuwa na kuongezeka kwa vitisho kwetu wafanyakazi kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Brigedia Jenerali Fulgence Simon Msafiri, pamoja na timu yake ya Mwanasheria na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala kama tulivyokwisha kueleza katika waraka wetu wa kwanza. Badala ya kutekeleza maagizo yanayotolewa na wasimamizi wao kwa kufuata taratibu za utumishi wa umma wameanza kutisha wafanyakazi kwa kuanza kutafuta na kuhisi wafanyakazi wanaotoa na kuandaa taarifa hizi. Wafanyakazi tunaomba kuwajulisha viongozi wetu wa Tume wanaoongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu kuwa tumezoea kuishi katika maisha ya vitisho kama swala wa porini ila hali hii tumeichoka ndio maana tunapaza sauti zetu kwa wenye mamlaka watusaidie kutuokoa katika mateso haya. Tupo tayari kutoa ushahidi wa mambo haya popote tutakapoitwa endapo tu tutahakikishiwa usalama wa ajira zetu kama tulivyoeleza kwenye sehemu ya pili ya mfululizo wa nyaraka hizi. Wafanyakazi hatuwezi kuacha kutimiza wajibu wetu wa kufanya kazi kwa weledi na ufanisi kwa sababu ya kuogopa vitisho vya watu wanaotumia vibaya madaraka yao katika ofisi za umma. Wafanyakazi tulieleza vizuri katika sehemu ya kwanza ya waraka huu kuwa mambo haya yanahitaji uchunguzi wa karibu sana kwa kuwa Mwanasheria wa Tume Ndg. Allen Kitutu ameshikilia vitengo karibu vyote vya Tume, huku ukiacha kazi zake za msingi yeye ni Afisa Rasilimali watu, Afisa manunuzi (Procument Officer), Mtaalamu wa maabara ya kupima viwango mionzi kwenye vyakula na mazingira, Afisa usafirishaji, Afisa majengo (Estate Officer) n.k kwa kweli huyu anaingia sekta zote bila hata kujali ushauri kutoka kwa wataalamu husika hivyo amesababisha Tume kupoteza mwelekeo wa kuundwa kwake na hata kukatisha tamaa ya wafanyakazi kufanya kazi zao.

Tunaomba tujikumbushe kidogo Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania ni nini?

Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) imeundwa kwa Sheria ya Bunge namba 7 ya mwaka 2003, yaani, “The Atomic Energy Act No. 7 of 2003.” Kulingana na Sheria hii, Tume imepewa mamlaka ya kisheria kwa niaba ya Serikali ya kusimamia na kudhibiti na kuhamasisha/kukuza (promote) matumizi salama ya vyanzo vya mionzi kwa usalama wa jamii na maendeleo ya Taifa. Tume inaongozwa na Bodi ya Wakurugenzi na Sekretarieti chini Mkurugenzi Mkuu, Tume inazo Kurugenzi tatu zinazoongozwa na Wakurugenzi.

Kulingana na kifungu Na. 7(4) cha Sheria ya Nguvu za Atomiki yaani Kurugenzi ya Fedha na Utawala, Kurugenzi ya Udhibiti wa Mionzi Ayonisha na Kurugenzi ya Teknolojia ya Nyuklia zimeundwa.

Majukumu ya TUME ni yafuatayo: -

(a) Kusimamia na kudhibiti matumizi salama ya mionzi nchini;

(b) Kuhamasisha (promote) matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia na

(c) Kuishauri Serikali kuhusiana na mikataba ya kimataifa kuhusu matumizi salama na uhamasishaji wa teknolojia ya nyuklia.

Katika waraka huu wa tatu yapo mambo ambao wafanyakazi tunaomba wanaohusika na usimamizi wa Tume kulingana na kifungu Na. 7 (1-4) cha sheria inayoongoza Tume, wayafanyie uchunguzi kutokana na maelezo tutakayo yaeleza ili kuwa na utendaji kazi wenye mafanikio katika Tume kwa kuwa kwa sasa Tume inaelekea kupoteza mwelekeo wake kutokana na aina ya viongozi tulionao kujali maslahi yao binafsi na kusahau kabisa kusudi la uundwaji wa Tume na kuelekeza nguvu kubwa katika upimaji wa mionzi kwenye vyakula na ukusanyaji wa fedha na kusahau usalama wa mionzi katika maeneo mengine kama vile Viwanda (mabati, nondo, vinywaji na uundaji na uunganishaji wa mabomba ya gesi na mafuta), Migodini, kwenye utafiti wa gesi na mafuta, Viwanja vya ndege, Ujenzi wa barabara na Mahospitalini ambako athari za mionzi ni kubwa kuliko kwenye vyakula ambako umekuwa mkazo mkubwa wa uongozi wetu.

Mambo yafuatayo tunaomba yafanyiwe uchunguzi ili kubaini kwa nini yanatokea katika Tume;

a) Uteuzi na uthibitishaji wa Wakurugenzi wa kurugenzi usiofuata taratibu zilizopo kwenye sheria kifungu na. 7 cha Sheria iliyounda Tume

b) Upimaji wa uonevu na usiokuwa na tija kwenye fomu za OPRAS kwa wafanyakazi

c) Kutokuwa na mpango wa kukaa na wafanyakazi wanaoajiriwa na wale waliopo katika Tume “retention scheme of workers”

d) Kuzuiwa wafanyakazi wanaopata ufadhili wa masomo ya juu kwenda masomoni bila sababu za msingi

e) Uuzaji wa liquid nitrogen gas inayozalishwa kwa matumizi ya maabara zilizopo makao makuu ya Tume, Arusha

f) Matumizi mabaya ya madaraka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu

g) Uhalisia wa gharama zilizotumika katika ukarabati wa nyumba za Tume na maabara ya wet Chemistry

h) kutoshiriki Wafanyakazi Kwenye Shughuli na Sherehe za Kitaifa

i) Sababu za Kushuka kwa Utendaji Ndani Ya Tume

Uteuzi na Uthibitishaji wa Wakurugenzi wa Kurugenzi Usiofuata Taratibu Zilizopo Kwenye Sheria Kifungu Na. 7 cha Sheria Iliyounda Tume

Itakumbukwa kuwa tangu Kaimu Mkurugenzi Mkuu aletwe na Wizara Septemba 2016 kama ilivyoelezwa kwenye sehemu ya kwanza ya waraka huu ameachwa kufanya teuzi na kuthibitisha Wakurugenzi bila kufuata taratibu zilizopo. Tangu Februari 2017 amefanya mabadiliko mara tatu ya wakurugenzi bila sababu za msingi ikiwa ni pamoja na kuondoa wale ambao wanakuwa wadadisi kwa mambo ambayo yeye binafsi pamoja na timu yake wanapendelea yafanyika kwa kulazimisha kuyapitisha katika vikao mbalimbali.

Alipoingia katika Tume aliwakuta wakurugenzi wafuatao;

i. Innocent Mapendo …………. Mkurugenzi wa Fedha na Utawala (Finance and Adminstration)

ii. Dkt. Mwijarubi Nyaruba …………. Mkurugenzi wa Teknolojia ya Nyuklia (Nuclear Technology)

iii. Dkt. Wilbroad Muhogora ………… Mkurugenzi wa Uthibiti wa Mionzi Ayonisha (Radiation Control)

Wakurugenzi hao wote watatu waliondolewa kwa kigezo tu kuwa utendaji wao wa kazi uko chini ya kiwango kwa kupewa alama (5) katika OPRAS zao za mwaka 2016 kwa tathmini aliyoifanya mwezi Februari 2017 japo kuwa katika ripoti zilizokuwa zinapelekwa katika Bodi ya Wakurugenzi na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia ilikuwa inaonyesha utendaji wa kazi za Tume unaimalika tangu Septemba 2016 alipokabidhiwa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu, kinyume na utendaji wa wasaidizi wake wa karibu yaani wakurugenzi kuonekana utendaji wao umeshuka na ni mbovu. Hizi zilikuwa ni mbinu tu zakuondoa wakurugenzi walikuwa wanaijua miundo mbinu ya utawala uliokuwepo na kuweka utawala wake ili awezekutimiza malengo yake. Alifanya uteuzi mpya na kuweka Makaimu wakurugenzi wapya katika kurugenzi zote tatu (3) hapa hatujua kama hata Bodi ya Wakurugenzi ilishirikishwa au la, wafuatao aliwateua kuwa wakurugenzi;

i. Naiman Mchomvu …… Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Utawala (Finance and Adminstration)

ii. Dkt. Firmi Banzi …………. Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia ya Nyuklia (Nuclear Technology)

iii. Dkt. Justine Ngaile ………… Kaimu Mkurugenzi wa Uthibiti wa Mionzi Ayonisha (Radiation Control)

Ijulikane wazi kuwa wakurugenzi hawa waliondolewa walirudi kwenye nafasi zao kulingana na utaalamu wao walioajiriwa nao, jambo ambalo lilionyesha wafanyakazi hawa kukata tamaa ya kufanya kazi. Kutokana na mabadiliko haya Innocent Mapendo alirudi kwenye nafasi yake ya awali ya mkaguzi mkuu wa hesabu za ndani ambayo alikuwa ameikaimisha kwa mfanyakazi mwingine ambaye pia hakuwa na sifa za kufanya kazi hiyo kwa muda mrefu tu. Aidha ijulikane wazi kuwa Naiman Mchomvu ndiye alikuwa msimamizi mkuu wa idara ya fedha (Chief accountant) nafasi ambayo ilikaimishwa kwa Hamida Mkunga ambaye hana utaalamu wa uhasibu kwa kuwa yeye aliajiriwa kama Afisa Uchumi na Mipango wa Tume (Economist and Planning officer). Mabadiliko haya ukiyangalia yalikuwa na jambo ndani yake maana baada ya muda si mrefu mkaguzi wa ndani Innocent Mapendo alihamishwa makao makuu ya Tume na kupelekwa ofisi ya Zanzibar ambako anatumika kama mhasibu wa kawaida mpaka wakati waraka huu unaandikwa na wafanyakazi wa Tume. Hatujui kama mabadiliko haya ya mkaguzi wa ndani yalibarikiwa na Bodi ya wakurugenzi au Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, pia jambo hili tunaomba lifanyiwe uchunguzi kwa kuwa nafasi ya mkaguzi wa ndani na msimamizi mkuu wa uhasibu/fedha zinatia mashaka sana kwa usitawi wa Tume. Baada ya mabadiliko hayo uongozi wa wakurugenzi, Kaimu Mkurugenzi Mkuu alifanya mabadiliko ya wakurugenzi hao kwa kumthibitisha Naiman Mchomvu kuwa mkurugenzi wa fedha na utawala na kumuondoa Dkt. Justine Ngaile na kumpeleka ofisi ya mpaka wa Namanga hivyo kufanya orodha ya wakurugenzi kuwa kama ifuatavyo mpaka wakati waraka huu unaandikwa;

i. Naiman Mchomvu …………. Mkurugenzi wa Fedha na Utawala (Finance and Adminstration)

iii. John Ngatunga …………Kaimu Mkurugenzi wa Uthibiti wa Mionzi Ayonisha (Radiation Control)

Wafanyakazi tunaamini mabadiliko ya namna hii yanaondoa kujiamini katika utendaji kazi kwa viongozi wanaoteuliwa hivyo inapunguza ubunifu katika utendaji wao wa kazi, mabadiliko haya kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu yamekuwa yakifanyika pia kwa wakuu wa idara mbalimbali ikiwa ni pamoja na idara ya Mionzi Ayonishi, Idara ya kupima viashiria vya mionzi kwenye chakula na mazingira, Ofisi ya mpaka ya Namanga na Ofisi ya kanda ya Dar es salaam. Kuongezeka kwa mabadiliko haya ya mara kwa mara kunatia wasiwasi kwa wafanyakazi na viongozi wanaoteuliwa hivyo kufanya utendaji kazi kushuka tofauti na inavyoripotiwa na utawala wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu kuwa kumekuwa na mafanikio makubwa katika kipindi tangu septemba, 2016. Tunaomba wanaohusika kufanya uchunguzi katika jambo hili na kumshauri Kaimu Mkurugenzi Mkuu kuwaamini watu anaowateua ili Tume iwezekufanya kazi zake kulingana na sheria iliyoiunda na kwa mafanikio.

Upimaji wa uonevu na usiokuwa na tija kwa wafanyakazi kwenye fomu za OPRAS

Tangu ateuliwe Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyu na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kumekuwa na ukatishaji tamaa mkubwa sana kwa wafanyakazi na kupunguza morali kwa kiwango cha juu sana. hili linatokana na kuwepo kwa vitendo vya kutuambia wafanyakazi hatufanyi kazi ilikuwa ripoti mbalimbali wanazoziandika kwenye mamlaka husika zinakuwa zikionyesha kuwa utendaji kazi katika Tume umeongezeka pamoja na kuwa hatuelewi ni vipimo gani vinatumika katika kutoa na kupata takwimu hizo. Aidha wafanyakazi tulikatishwa tamaa zaidi kipindi ambapo tathmini ya kazi zetu ilifanyika kwa kupitia kazi ambazo kila mmoja wetu alizijaza kwenye fomu za OPRAS na kuambiwa ni wafanyakazi wanne tu ambao walikuwa wamefikia viwango vya ufanyaji kazi ambavyo alikuwa ameviweka Kaimu Mkurugenzi Mkuu na wengine wote tulikuwa chini ya wastani hivyo hawa wafanyakazi wanne ndio walikuwa wanastahili kupandishwa daraja. Wafanyakazi hao ni Naiman mchovu( Mkurugenzi Fedha na Utawala), Allen kitutu (Mwanashria wa Tume), Hamida Mkunga(Kaimu Msimamizi wa uhasibu) na Abel Ntwa (Mkuu wa Idara ya maabara ya upimaji wa Mionzi kwenye vyakula na Mazingira). Ukweli jambo hili linatukatisha tamaa wafanyakazi, tunaomba wanaohusika na usimamizi wa utendaji kazi wa Tume walisimamie na kulikemea jambo hili kwa kuwa linapunguza ustawi kwa wafanyakazi. Aidha tunaamini kwamba tathmini katika mfumo huu wa OPRAS ni wa mwendeleo na si wa wakati mmoja hali ambayo kama kulikuwa na kutokuwajibika kwa wafanyakazi kungekemewa na kushauriwa mapema badala ya kusubiri na kutoa tathmini za aina hii. Tunaamini kuwa pamoja na kukatishwa tamaa kwa kiwango hiki wafanyakazi tumeendelea kufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu pamoja na kuwa na mazingira hatarishi katika utumishi wetu. Wizara husika na Bodi ya wakurugenzi tunawaomba mfanyie uchunguzi jambo hili ili kutujengea wafanyakazi mazingira salama katika utumishi wetu.

Kutokuwa na mpango wa kukaa na wafanyakazi wanaoajiriwa na wale waliopo “retention scheme of workers”

Ukisoma taarifa nyingi sana za Tume kwenda Bodi ya wakurugenzi na Wizarani kumekuwa na malalamiko mengi ya kuwa Tume ina upungufu mkubwa wa wafanyakazi, ni kweli Tume ina upungufu wa wafanyakazi hasa maeneo ya utaalamu hili linatokana na unyeti wa taaluma yenyewe “ Nguvu za Atomiki” ambapo sio wataalamu wengi wanaosoma masomo ya Fizikia, Kemia, Biolojia na Hisabati katika ngazi za Elimu ya juu zikiwemo Teknolojia ya Nyuklia. Aidha hili lililoelezwa ni kwa upande mmoja bali hata hawa wataalamu wanapopatikana ofisi ya Mkurugenzi Mkuu imekuwa haina mpango wa kukaa nao na kuwaendeleza kwa makusudi na hili limekuwa tatizo kubwa zaidi kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyu “Brigedia Jenerali Fulgence Msafiri” tangu alipoteuliwa na wizara Septemba, 2016. Tunaomba tutoe mifano michache tu katika jambo hili, Kaimu Mkurugenzi Mkuu alimkataa Bw. Atumaini Makoba aliyekuwa ameajiriwa kupitia Tume ya Utumishi, Ofisi ya Raisi na Menejimenti ya utumishi wa umma kama Mtaalamu wa Fizikia ya Mionzi daraja la I na kumrudisha manispaa ya Temeke alikokuwa ameajiriwa awali bila sababu za msingi. Pili mahakama ilimurudisha kazini mfanyakazi ambaye alikuwa amefukuzwa kazi bila kosa la msingi Didas Shao na Kaimu Mkurugenzi huyu akamkataa Didas Shao ambaye alikuwa ni Mtaalamu wa Teknolojia ya Nyuklia daraja la I pamoja na kuwa mpaka sasa hataki kumlipa haki zake. Aidha Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyu amewahamisha wafanyakazi wawili kwenda Wizara ni ambao ni Edwin Konzo – mtaalamu wa Fizikia ya Mionzi daraja la II na Ebenezer Kimaro Mtafiti wa Sayansi ya Nyuklia daraja la I bila kuombwa na wizara husika, jambo ambalo tunajua ni kwa sababu tu za kuwa viongozi wa chama cha wafanyakazi ambayo tumeyaeleza vizuri katika waraka wa kwanza na wa pili wa Nani atakayeikoa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania. Kutokana na sababu za vitisho na matumizi mabaya ya madaraka na kutokujali utaalamu wa wafanyakazi Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyu alisababisha Sadiki Mutabuzi kuamua kuacha kazi katika Tume, huyu alikuwa ni mtaalamu mwandamizi daraja la I katika matengenezo ya vifaa vinavyotoa Mionzi ayonishi nchini ikiwa ni pamoja na mashine za X-ray, CT Scanner, Mashine za kupimia kansa ya Matiti nk. Hii ni mifano michache tu ambayo tumeona tuitoe, tunaamini uchunguzi ukifanyika katika jambo hili mengi yatajulikana ambayo yanafanya wafanyakazi kukataliwa, kuhamishwa, kufukuzwa na wengine kuacha kazi au kuomba kuhamishia utumishi wao kwa waajiri wengi. Ifahamike kuwa mifano hiyo yote imetokea kati ya Septemba, 2016 na sasa yaani kipindi ambacho Kaimu Mkurugenzi Mkuu amekuwa akiisimamia Tume. Vyombo vinavyosimamia Tume tusaidieni kuiokoa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania.

Kuzuiwa wafanyakazi wanaopata ufadhili wa masomo ya juu

Ni jambo la kisheria kwa mwajiri kuwaendeleza wafanyakazi wake kimasomo ili kuongeza uwezo wa wafanyakazi katika utendaji wa kazi kwa ufanisi. Wafanyakazi tunatoa malalamiko yetu kwa uongozi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume kwa tabia iliyojitokeza katika kipindi cha utawala wake kutoruhusu wafanyakazi kwenda masomoni wanapopata nafasi hizo za masomo ya juu mara nyingi bila hata kupewa sababu za kuzuiwa. Ifahamike wazi kuwa wafanyakazi tunasema haya baada ya zaidi ya wafanyakazi watano (5) kutopewa ruhusa ya masomo ya masters degree, mmoja degree na wengine wawili (2) Phd degree wakiwa na udhamini wa masomo hayo kwa muda wote wa masomo. Aidha wafanyakazi walioko masomoni ulikuwepo utaratibu wa kupewa baadhi ya allowance ambazo zilikuwa zinatolewa na mwajiri kama vile house allowance wanapokuwa masomoni kulingana na taratibu za Tume. Kaimu Mkurugenzi Mkuu amezifuta ili kujenga mazingira magumu kwa familia za wafanyakazi waliopo masomoni. Mambo haya yanatokana na kutokuwepo kwa utaratibu unaofahamika na wafanyakazi wa kuwaendeleza kimasomo (Training Scheme for workers). Kwa wakati huu wapo wafanyakazi waliopo masomoni ambao ruhusa za masomo walipewa wakati wa Mkurugenzi Mkuu aliyepita. Umuhimu wa wafanyakazi wa Tume kujiendeleza kimasomo unatokana majukumu iliyonayo Tume hii kwa maendeleo tarajiwa ya taifa kwa ujumla katika nyanja za viwanda na miundombinu. Tunaomba Bodi ya Wakurugenzi na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kuchunguza uhalisia wa mambo haya ili kuongeza ustawi wa wafanyakazi na Tume kwa ujumla.

Uuzaji wa liquid nitrogen gas inayozalishwa kwa matumizi ya ofisi

Kwenye waraka uliotangulia wafanyakazi tulieleza matumizi mabaya ya Madaraka ya viongozi wa Tume hasa timu iliyoundwa kati ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Mkurugenzi wa fedha na utawala na Mwanasheria wa Tume. Kumekuwa pia na ukaribu unaotia wasiwasi kati ya Mwanasheria wa Tume na Mkuu wa Idara inayosimamia maabara ya upimaji wa mionzi kwenye vyakula ambayo pia ndio inazalisha gesi ya liquid nitrogen ambayo inatumika katika mitambo inayotumika katika upimaji wa viasili vya mionzi kwenye sampuli za chakula cha binadamu na mifugo. Mtambo unaotumika katika uzalishaji wa gesi hii ni sehemu ya vifaa vilivyoletwa chini ya mradi mkubwa wa umoja wa nchi za ulaya “European Union” ambao ulianza kuratibiwa kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu aliyepita, marehemu Iddi Mkilaha Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, kutoka na Tume kununua gas kwa wazalishaji wengine nchini tangu miaka ya 1998 Tume ilipoanza kutoa huduma ya upimaji vyakula. Uzalishaji wa gesi hii katika Tume ilichukuliwa pia kama mradi wa uzalishaji fedha kwa ajili ya kuimalisha matengenezo ya vifaa vya maabara ili kuwe na huduma ya uhakika na yenye kuendelea kwa usalama wa wananchi kwa ujumla. Wafanyakazi tunaamini kuwa mipango ya uuzaji wa gesi hii umewekewa taratibu nzuri ambazo zinaweza kuwa na manufaa kwa Tume na Taifa kwa ujumla. Kumekuwa na mwenendo unaoonyesha kuwa Mkuu wa Idara na Mwanasheria wa Tume wamekuwa wakiuza gesi siku za jumamosi na jumapili mara kadhaa jambo ambalo linaleta wasiwasi mkubwa kama uuzaji huu unafuata taratibu zilizowekwa maana katika siku hizi ofisi zingine za Tume kama uhasibu huwa zimefungwa. Tunashauri taratibu za uuzaji gesi hii zifahamike, uchunguzi kwa wahusika ufanyike japo kuwa inawezekana kukawa na ugumu kulingama na mfumo wa uongozi uliopo kama tulivyoeleza hapo juu kuwa uongozi unawekwa kwa matakwa ya kundi fulani kwa manufaa binafsi ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu na washirika wake.

Matumizi mabaya madaraka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu

Baada ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu kupanga vizuri safu yake ya madaraka kwa jinsi ilivyompendeza imetengeneza mianya ya kufanya anavyotaka katika matumizi na malipo katika mali na fedha za Tume. Wafanyakazi tunaona tuwajulishe wasimamizi wa Tume mambo machache yanayofanyika na Brigedia Jenerali Fulgence Simon Msafiri.

· Amekuwa akiondoka na gari la Tume kwenda katika likizo zake za mwaka na dereva kwa wakati wote wa likizo yake, dereva amekuwa akilipwa pesa ya kujikimu wakati wote wa likizo ya Mkurugenzi Mkuu, rejea likizo yake ya Januari 2018. Ambapo katika kipindi hicho cha likizo gari mbili za Tume aina ya Nissan zimepata ajali zikiwa katika harakati za kutumika wakati wa likizo.

· Mkurugenzi huyu anaishi katika nyumba ya serikali ambayo inahudumiwa kwa gharama zote ikiwemo umeme, maji na mlinzi kwa gharama ya Tume pamoja na kupewa huduma ya usafiri muda wote anapokuwa katika majukumu yake ya kazi jambo linaloshangaza ni kwamba kila mwezi analipwa tena allowance ya mafuta, nyumba na utility ambazo hatuamini kuwa anasitahili kulipwa. Tunaomba jambo hili liweze kuchunguzwa kama halipo sawa kwa kuwa linaitia hasara Tume isio ya lazima.

· Kutokana na unyeti wa taaluma ya nguvu za Atomiki (Teknolojia ya Nyuklia) Shirikika la Nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) linaendesha semina nyingi kwa viongozi na wafanyakazi wa Taasisi zinazofanana na Tume duniani. Kutokana na ukweli huu baada ya mwongozo wa serikali kuhusu kutokujihusisha na ulipaji wa gharama za safari za nje ya nchi kwa sehemu kubwa. Menejimenti ya Tume ikiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyu iliamuru kuwa viongozi na wafanyakazi watashiriki kwenye mafunzo na semina hizo bila kuwa na malipo yeyote ya ziada kutoka kwenye Tume isipokuwa gharama zote zitagharamiwa na Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) na si vinginevyo na ndivyo imekuwa ikifanyika kwa kuwa mafunzo haya hufanyika mara nyingi kwa wafanyakazi na viongozi duniani kote kwa ajili ya kuhakikisha kunakuwa na matumizi salama kwa vyanzo vyote vya mionzi duniani. Aidha, Kaimu Mkurugenzi Mkuu amekuwa akijilipa tofauti ya fedha ya kujikimu (Perdiem allowance) nje ya nchi tofauti na makubaliano aliyoyaweka kwa safari zake zote za nje. Jambo hili tunaomba lichunguzwe na wasimamizi kama lipo kinyume cha utaratibu kwa kuwa IAEA huwa katika malipo unayopewa muhusika wa mafunzo inahusiwa pia perdiem allowance kulingana na nchi ambayo mafunzo, semina, kongamano au mkutano unapofanyika.

· Kutokana na mfumo wa uongozi aliouweka kama tulivyoeleza hapo juu yaani wa Kurugenzi ya Fedha na Utawala pamoja na mwanasheria Kaimu Mkurugenzi Mkuu amekuwa akilipwa fedha za safari za kikazi hata anapokuwa likizo, kwa mfano kuna malipo ya safari ya kikazi Dodoma ya 16/01/2018 wakati alikuwa likizo tangu mapema Januari, 2018 mpaka 29 Januari, 2018 alipomaliza likizo yake.

· Kwa mujibu wa taaluma yake ya kijeshi tunaamini anastahili kujilinda wakati wote, lakini tunaamini pia jambo hili linatakiwa kufanyika kwa usiri hasa anapokuwa ofisini akitimiza majukumu yake ya Mkurugenzi Mkuu kwa kuwa amekuwa akija na bastola ofisini na wakati mwingine akiwa na uniform za kijeshi. Wafanyakazi tunaomba apunguze haya maana tunaheshimu na kufahamu taaluma yake hii muhimu kwa usitawi wa taifa letu. Vifaa hivi visitumike kama sehemu ya utisho kwa wafanyakazi kudai haki zao wakati wakiwa wametimiza wajibu wao.

Uhalisia wa gharama zilizotumika katika ukarabati wa nyumba za Tume

Tume inamiliki nyumba nne (4) kwa makazi ya watumishi ikiwa ni pamoja na nyumba ya Mkurugenzi Mkuu iliyopo eneo la SDA Njiro, Nyumba mbili za watumishi zipi eneo la Nalopa Njiro na nyumba moja ipo eneo la sokoni Mbauda. Nyumba hizi zote wanaishi watumishi wanazilipia kodi kwa kila mwezi. Mwanzo mwa mwaka huu umefanyika ukarabati wa nyumba mbili zilizopo Nalopa Njiro, ukarabati huu unakadiliwa kutumia takribani 117,000,000/= kwa taarifa, ikijumlisha ukaratabati wa wet chemistry lab ambayo tunaamini itakuwepo kwenye jengo jipya linalojegwa kwa hiyo hakuna ulazima wa kupoteza gharama zingine kwenye kukarabati vyumba ambavyo vinaweza kutumika kwa kazi zingine. Kufikia wakati huu waraka unaandikwa kiasi cha shilingi 40,000,000 zilikuwa zimeshalipwa kwa ajili ya hiyo kazi. Wafanyakazi tunaomba uchunguzi wa gharama hizi ufanyike kwa kuwa hazina uhilisia na kilichofanyika. Aidha ukumbukwe fedha ilitumika bila uthibitisho wa Baraza la wafanyakazi na Bodi ya wakurugenzi. Kumekuwa na ukarabati tofauti tofauti ukiendelea hapa ofisi ambao wafanyakazi unatumika na watawala katika kuiba fedha za Tume kwa kuwa mipango ya karabati hizi hupangwa na watu watatu tu kwa kweli hapa panakuwa na kitu cha tofauti.

Kutoshiriki Wafanyakazi Kwenye Shughuli na Sherehe za Kitaifa

Kutakana na Brigedia Jenerali Fulgence Simon Msafiri kuchukia uwepo wa chama cha wafanyakazi eneo la kazi imefikia mahali kwamba ushiriki wawafanyakazi kwenye sherehe za kitaifa zinazoratibiwa na vyama vya wafanyakazi duniani imekuwa kama hisani kwa wafanyakazi mpaka inafikia mahali pa kuzuwia kushiriki kwenye shughuli na sherehe hizo. Tunaomba kutoa mfano wa hivi karibuni ambapo mwaliko wa ushiriki wa wafanyakazi wanawake katika maandalizi ya siku ya wanawake duniani yaani (8/3/2018) ulipoletwa katika Tume Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyu aliukataa eti kwa sababu tu viongozi wa Halmashauri ya Chama cha Wafanyakazi haikuwepo ili hali uongozi wa wanawake katika Tume upo na unajitegemea ila Halmashauri ya Chama cha wafanyakazi hutumia wajumbe wake kama sehemu ya ushirikishwaji wa wanawake katika mambo ambayo vikao vya Chama hujadili kwa ajili ya wafanyakazi. Aidha kwa sababu hiyo kutokuwepo kwa viongozi wa Halmashauri ya Chama cha wafanyakazi hakukuwa sababu ya msingi kwake kuwazuia wafanyakazi wanawake kushiriki katika siku yao muhimu “Siku ya Wanawake Duniani”.

Hata hivyo Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyu anajua sababu za kwanini Halmashauri ya Chama cha wafanyakazi kutokuwepo katika Tume kulikotokana na unyanyasaji wake kwa viongozi wa Chama cha wafanyakazi kama tulivyoeleza kwenye nyaraka zilizopita, unyanyasaji huu wa viongozi ndio ulipelekea kumufukuza kazi mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi ndugu Barnaba Chimatila bila sababu za msingi baada ya kuwa ndio kiongozi peke yake wa Chama cha wafanyakazi aliyekuwa amebaki baada ya wengine kuhamishwa nje na ndani ya Tume na wengine kuchukua hatua za kujiuzulu kutokana na manyanyaso ya wazi kwa viongozi wa Halmashauri ya Chama cha wafanyakazi, ambayo yalihusisha kulazimishwa kushiriki kwenye vikao ambavyo havikuwa halali, baada ya kufukuzwa kwenye vikao hivyo Mwenyekiti na Katibu wa Chama cha wafanyakazi. Tukitoa mifano tu ya viongozi wa Halmashauri waliopewa manyanyaso ya wazi kwa kulazimishwa kushiriki vikao hivyo ni Christina Nyakyi na Agrey Kitosi ambao baadae kama mwendelezo aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya wanawake Christina Nyakyi alimhamisha makao makuu ya Tume kwenda kituo cha Tarakea mpakani na Kenya ambako yupo mpaka wakati waraka huu unapoandikwa. Tuendelee kuwaomba Bodi ya wakurugenzi na Wizara ya Elimu sayansi na Teknolojia mtusaidie ili tuweze kuwa na nafasi za ushiriki katika matukio ya kitaifa yanahusisha wafanyakazi wote duniani maana hii inatupa dalili za sisi wafanyakazi kutoshiriki sikukuu za Meimosi 2018 labda kwa sababu hizi hizi zilizotolewa kwa wanawake kutokushiriki Sikukuu ya wanawake duniani.

Sababu za Kushuka kwa Utendaji Ndani Ya Tume

Kaimu Mkurugenzi Mkuu katika vikao vyake na wafanyakazi vya tarehe 7/3/2018, 8/03/2018 na 9/03/2018 alikiri kushuka kwa utendaji kazi katika Tume, ambao kwa maelezo yake mwenyewe, uzorotaji huu wa utendaji umeanza kipindi cha mwaka 2016 hadi sasa japokuwa alikiri pia kuwa hapa katika utendaji ulipanda kidogo na kuanza kushuka tena. Ikumbukwe kwamba Mkurugenzi huyu aliletwa hapa kwenye Tume ili kuboresha utendaji wa Tume ambao ulikuwa umezorota kwa mujibu wa waliomleta. Lakini kinyume chake utendaji wa Tume umezidi kuzorota zaidi katika kipindi chote ambacho ameongoza Tume hii. Lakini uzorotaji huu wa utendaji kazi katika kipindi hiki sio jambo la kushangaza hata kidogo kutokana na mambo kadhaa yaliyojitokeza katika kipindi chake. Mambo haya yamejitokeza kutokana na yeye (Kaimu Mkurugenzi mkuu) kutegemea kupewa ushauri na “akili ndogo” (Mwanasheria wa Tume na Mkurugenzi wa fedha na utawala) ambazo hazina uzoefu wowote na majukumu ya msingi ya Tume kwa mujibu wa sheria iliyounda Tume ama kwa makusudi ili kumharibia na kujineemesha wao au kwa ujumla wao wa kutokujua makujumu ya msingi ya Tume kama yalivyoelezwa kwa ufupi hapo mwanzo mwa waraka huu. Mkurugenzi huyu amekuwa akitumia ushauri wa watu hawa wawili na kuacha kusikiliza ushauri unaotolewa na viongozi (wataalam) wengine waliopo kwenye Menejimenti/wafanyakazi wenye uzoefu wa kutosha, tena wakiwamo ambao wana uzoefu wa kitaalam uliobobea katika majukumu ya msingi ya Tume kwa muda mrefu. Katika kusikiliza ushauri wa “akili ndogo” Mkurugenzi huyu amekuwa akihamisha hamisha wafanyakazi pasipo kuzingatia ufanisi wa majukumu ya Tume. Mkurugenzi huyu tangu ameletwa hapa kwenye Tume ameshahamisha wafanyakazi zaidi ya 12 na kufukuza wafanyakazi watatu na kuhamisha nje ya Tume wafanyakazi watatu bila kuzingatia mahitaji halisi ya Tume katika kuboresha utendaji kazi kwa ufanisi. Aidha itakumbukwa kuwa kumekuwa na upungufu wa wafanyakazi wataalam makao makuu kwa muda mrefu kulingana na ripoti mbalimbali za Tume. Hamisha hamisha hii ambayo imefanyika kama adhabu kwa walengwa ukiifuatilia utakuta kuwa washauri wakuu wa hamisha hii ni wale wale “akili ndogo”. Kwa mujibu wa kifungu cha sita (6) cha sheria namba 7 ya nguvu za atomiki ya mwaka 2003, Tume ina majukumu (functions)takribani 5 yenye vipengele vingi hasa lile jukumu la kwanza, lakini kimsingi ni kipengele kidogo kimoja cha jukumu namba moja lenye vipengele 24 kinachopewa kipaumbele katika hivyo 24 ambacho ni udhibiti wa vyanzo vya mionzi katika vyakula vinavyoingia na kutoka nchini. Jukumu hili kimsingi halina umuhimu kuzidi majukumu mengine, kusababisha kupeleka wasimamizi kwenye mipaka kwa kiwango kilichofanyika mpaka sasa. Katika hamisha hamisha hii isiyokuwa na tija, Tume imejikuta ikiwahamishia mipakani wanasayansi (wataalam) waliobobea, wengine wakiwa na shahada za uzamifu (PhD) kwenda kutekeleza majukumu ambayo hata mtu mwenye Stashahada (Diploma) angeweza kuyatekeleza kwa ufanisi. Wataalamu hawa wangetumika kufanya tafiti na kutumia vizuri maabara za Tume ambazo zimepatiwa vifaa vya kutosha wangewezesha utendaji wa Tume kuwa wa kiwango cha juu sana kuliko kuwatumia kama wakusanya mapato mipakani. Mifano ya wafanyakazi waliohamishiwa mipakani huku utaalam wao ukihitajika zaidi kwenye majukumu mengine makubwa ya Tume pamoja na viwango vyao vya elimu kwenye mabano ni pamoja na:

1. Justine Ngaile (PhD in Nuclear Physics) ambaye ana uzoefu wa miaka zaidi ya 20 aliyehamishiwa mpaka wa Namanga

2. Ebenezer Kimaro (MSc Physics) uzoefu wa zaidi ya miaka 15 aliyekuwa amehamishiwa mpaka wa Sirari na baadae kuhamishiwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kile kilichoitwa kuwa ni kutokana na umuhimu wa kazi wizarani.

3. Lazaro Meza (MSc ) uzoefu wa zaidi ya miaka 10 aliyehamishiwa mpaka wa Tunduma

4. Mungubariki Nyaki (MSc Physics) uzoefu zaidi ya miaka 10 aliyehamishiwa bandari ya Tanga

5. Sadiki Mutabuzi (MSc. Eng) mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 7 aliyehamishiwa mpaka wa Holili, lakini aliacha kazi kutokana na kutokubaliana na uhamisho huu

6. Christina Nyakyi (MSc in Electronic and Telecommunication) uzoefu wa zaidi ya miaka 7 aliyehamishiwa mpaka wa Tarakea

7. Hilal Hussein (MSc) uzoefu zaidi ya miaka 6 aliyehamishiwa mpaka wa Horohoro

8. Leonid Nkuba (MSc in Physics) uzoefu zaidi ya miaka 5 aliyehamishiwa mpaka wa Mtukula

9. Tunu Kaijage (Postgraduate Diploma in Radiation Protection) uzoefu zaidi ya miaka 5 aliyehamishiwa mpaka wa Sirari

10. Erasto Kayumbe (MSc IT) uzoefu zaidi ya miaka 3 aliyehamishiwa mpaka wa Holili

11. Goodchance Mboya (BSc) mwenye uzoefu wa miaka zaidi ya 10 katika utaalam wa Dosimetry aliyehamishiwa Mtwara

12. Mchibya Matulanya (MSc ) mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 5 aliyehamishiwa Mtwara

13. Miguta Ngulimi (…) mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 5 aliyehamishiwa Songea

14. Edwin Konzo (BSc) mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 7 aliyehamishiwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kilichosemekana kuwa ni kutokana na umuhimu wa kazi Wizarani hapo.

15. Wilson Kitara (….) ambaye ana uzoefu wa miaka 5 aliyeajiriwa kama Nuclear Instrumentation technician amehamishiwa kituo cha mpaka wa Rusumo

16. Fadhili Msumali (….) mwenye uzoefu wa miaka 5 ambaye aliajiriwa kama Nuclear Instrumentation technician aliyehamishiwa kituo cha Namanga

17. Innocent Mapendo (MBA+CPA(T)) mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 7 aliyeajiriwa kama Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Ndani (Chief Internal Auditor) alihamishiwa ofisi ya Kanda Zanzibar kama mhasibu wa kawaida. Uhamisho huu ulikuwa ni kama adhabu kutokana na kuonekana kuingilia maslahi ya hawa watu wawili (Mwanasheria na DFA).

18. Alex Muhulo (Msc) uzoefu wa zaidi ya miaka 10 aliyehamishiwa katika ofisi ya Dar es Salaam

19. Wilson Ngoye (Msc in medical radiograph) uzoefu wa zaidi ya miaka 10 aliyehamishiwa ofisi ya Dar es Salaam

20. Amasi Aloyce (Msc) uzoefu wa zaidi ya miaka 5 aliyehamishiwa katika ofisi ya Dar es Salaam

21. Atumain Makoba (Msc Physics) ambaye aliajiriwa kwa taratibu za Tume ya Utumishi wa umma ofis ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma kutoka Manispaa ya Temeke kama Mtaalamu wa Fizikia ya Mionzi daraja la I, baada ya muda wake wa matazamio (Probation period) ya Mwaka mmoja pamoja na maendeleo mazuri aliyokuwa akionyesha katika ufanyaji kazi Kaimu Mkurugenzi Mkuu alimrudisha kwa mwajiri wake wa awali bila sababu za msingi eti alikuwa hamtaki kumuona akiwa mfanyakazi wa TAEC.

Wasimamizi wa Tume mnaweza kuona kuwa hamisha hamisha hii ambayo imefanyika ndani ya kipindi cha mwaka mmoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyu ambaye hajafikisha hata miaka miwili (2) ndani ya Tume, ikifuatiliwa kwa karibu itagundulika kuwa hazikufanyika katika muktadha wa kuimarisha utendaji kazi wa Tume, zaidi ya kuendelea kuzorotesha utekelezaji wa majukumu ya msingi ya Tume. Kwa sababu nyingi ya hamisho hizi zilifanyika katika kuwakomoa wahusika aidha kutokana na misimamo yao katika kusimamia maslahi ya wafanyakazi na maslahi ya Tume kwa ujumla wake. Hivyo basi, Mkurugenzi Mkuu anaposema utendaji wa Tume umeshuka inabidi na yeye ajitathmini kama kweli anafaa kuendelea kuongoza Taasisi hii muhimu katika nchi. Hivi alitegemea utendaji na ufanisi katika Tume baada ya kuhamisha wataalamu wote hawa waliosomeshwa kwa fedha za walipa kodi wa nchi hii? Halafu leo hii Mkurugenzi mkuu huyu huyu analalamika kuwa Tume haina wafanyakazi wa kutosha, wakati kuna wafanyakazi wenye uzoefu wa kutosha anawahamishia Wizarani bila hata ya kuombwa na Wizara husika kwa madai ya kwenda kuongeza ufanisi wizarani. Leo hii baada ya kufanya madudu kwa muda wote aliokabidhiwa Tume anatafuta mchawi aliyemloga wakati wachawi anao hapa hapa wamemzunguka. Inabidi ajitafakari na kujitathmini kama kweli ana uwezo wa kuvaa viatu vya kuongoza Taasisi hii muhimu kwa maendeleao ya Taifa. Wasimamizi wa Tume hii liangalieni hili kwa makini na kulichunguza ukweli wake. Maana hawa watu wawili waliitajwa hapo juu yaani Allen Kitutu na Naiman Mchomvu wana mpango wa makusudi wa kuiua hii Tume kwa maslahi yao binafsi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom