Nani atakasimishwa madaraka ya Urais endapo Rais atakuwa kasafiri?

Chura

JF-Expert Member
Sep 22, 2009
1,345
2,296
Wasalamu wana bodi wajuvi, wajuaji, wastaarabu bila kuwashau wale wa lolote sawa.
Leo ntatoa desa kidogo kuhusu mtiririko wa ukasimisishwaji madaraka ya Urais(presidential line of succession au hierarchy of presidency) kwa JMT.

Mataifa ya wenzetu kama US wao kutokana na muvi zao na kuwa wawazi sana inaelewaka kwamba anaanza Rais, Makamu, Spika halafu Waziri.

Hivi karibuni tumeshuhudia viongozi wakuu watatu kwa pamoja wakiwa nje ya nchi. Rais akiwa UK, Makamu Us na PM Japan, hivyo kuzua soga na mambo ya vijiweni kuhusu nani huweza kushika madaraka ya kuongoza serikali endapo Rais na Makamu wa Rais hawapo kwa maana wakiwa nje ya Jamhuri kwa Majukumu mengine.

Kwa kulianza hili desa tutaangalia viongozi wa Tanzania wakoje.

Kwa mujibu wa muongozo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwenye itifaki ya viongozi, umewataja viongozi wa kitaifa katika dhana mbili:

(1) Wa kisiasa - Hawa wanaweza wakawa wakuu kimjengo lakini hawana mamlaka yoyote kwa Tanzania, mfano Makamu wa Rais Zanzibar.

(2) Wa kimamlaka - Hawa wanakuwa wakuu kimjengo na wana mamlaka kwenye Jamhuri mfano Rais wa JMT.

Muongozo huu pia huongoza viongozi wa kitaifa katika kuingia kwenye tukio kwa maana ya nani kati yao ni wa kwanza kuingia na wa mwisho kuingia.

Vivyo hivyo muongozo huo unaongoza nani wa mwisho kuingia, nani akae wapi na nani asikae wapi sambamba na kutoka kwao kwa maana ya nani
anatangulia kutoka na nani ni wa mwisho kutoka.

Viongozi wa kitaifa ni hawa wafuatao:

MJENGO WA UKUU WA VIONGOZI TZ KISIASA

Rais wa JMT >Makamu Rais JMT >Rais wa ZnZ >Waziri Mkuu JMT > Makamu wa Kwanza Rais ZnZ(kama yupo lakini kutokana na katiba yao 2010)> Makamu wa pili wa Rais ZnZ > Spika wa bunge la JMT > Jaji Mkuu JMT

Kwa mtiririko hapo juu usije ukachanganya, mtiririko huo ni wa wakuu kisiasa na siyo kimamlaka japo wapo ambao ukuu wao unabaki vile katika dhana zote mbili mfano Rais wa JMT.

MJENGO WA UKUU WA VIONGOZI TZ KIMAMLAKA

Rais wa JMT > Makamu wa Rais JMT > WM wa JMT > Spika wa bunge JMT > Jaji Mkuu JMT>Waziri aliyekaa madarakani mda mrefu kuliko wote (mfano Mkuchika labda😂)

Wanabodi kwenye mjengo wa pili ndipo hasa kilipo kiini cha desa letu, mtiririko wa kukasimishwa madaraka ndani ya JMT huzingatia ukuu wa kimamlaka wa kiongozi husika na siyo wa kisiasa. Iko hivi kisiasa Rais Mwinyi wa Zenji ni Mkuu kwa Dr. Tulia maana hata kwenye hafla kiitifaki ataanza kuingia Tulia kabla ya Mwinyi. Ndiyo, hii ni kwa sababu politically Mwinyi is senior to Tulia, ila kimamlaka Tulia ana mamlaka makubwa kuliko Mwinyi unajua kwanini? Swali lifuatalo linajibu hili.

Nani huweza kukaimu madaraka ya Rais endapo Rais hayupo katika Jamhuri?

Wanabodi katiba inaeleza kama wengi tunavyofahamu kuwa endapo Rais wa Jamhuri ya
Muungano yupo kwenye majukumu mengine nje ya Jamhuri ni Makamu wa Rais ndito hukaimu kiti chake.

Je, baada ya Makamu au kama Rais na Makamu wa Rais wote hawapo ni yupi kati ya viongozi wa kitaifa huweza kukasimiwa mamlaka kwa muda ambao viongozi hao hawapo?

Kabla sijajibu swali hili ngoja niweke kitu kimoja sawa, katika kipindi kama hiki cha ukuaji mkubwa wa teknolojia Rais kuwa nje ya mipaka hakumuondolei uwezo wa yeye kuwajibika kama mkuu wa nchi. Hivyo majukumu mengine yote huyatimiza hata akiwa majuu na ndiyo sababu majuzi Rais Samia alifanya uteuzi wa viongozi moja kwa moja kutoka London.

Kwa hoja hii hakuna ukaimishwaji wa madaraka Rais akiwa nje ya mipaka isipokua pale tu Rais hawezi kutekeleza majukumu yake sababu ya ugonjwa, upungufu wa akili ama kifo.

Kwa mujibu wa ibara ya 37 ya Katiba ya Jamhuri ya
Muungano, inasema:

(3) Endapo Rais atakuwa hayupo katika Jamhuri ya
Muungano au atashindwa kutekeleza majukumu yake
kwa sababu nyingine yoyote, kazi na shughuli za Rais
zitatekelezwa na mmojawapo wa wafuatao kwa
kufuata mpangilio ufuatao, yaani-

(a) Makamu wa Rais au kama nafasi yake iwazi au kama yeye hayupo au ni mgonjwa basi;

(b) Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano.

Waziri Mkuu atadumu katika mamlaka hayo mpaka pale mmoja kati ya Rais au Makamu wa Rais atakaporejea naye ataacha kuhudumu katika mamlaka ya Rais na kurejea kwenye nafasi yake ya Uwaziri Mkuu kama iliyvoainishwa kwenye ibara ya 37.

Wanabodi mnaona sasa katiba imejiweka wazi kwamba Rais>Makamu>Waziri mkuu ikaishia hapo je, ikitokea wote hawapo inakuaje? Ukiwa makini utagundua kwamba katiba imetaja ukasimishwaji kwa kufuata mjengo wa ukuu kimamlaka na sio kisiasa na ndiyo maana baada ya Makamu wa Rais akaja Waziri Mkuu na sio Rais wa Zanzibar.

Maana yake ni kwamba Mjengo wa Ukuu kimamlaka ndiyo unaotupa mnyororo wa nani anafuata baada ya nani maana yake kama Rais, Makamu na Waziri Mkuu wote hawapo basi mamlaka yataenda moja kwa moja kwa Spika, na kama pia Spika hayupo basi moja kwa moja Rais anakua Jaji Mkuu na kama naye hayupo basi Waziri aliyekaa madarakani mda mrefu kuliko wote ndiyo anakaimishwa kuwa Rais.

Hii ndiyo sababu awali niliwaambia kwamba Tulia kimamlaka ni Mkuu kwa Mwinyi au kwa lugha nyingine Waziri wa Baraza la Mawaziri la JMT ana mamlaka makubwa kuliko Rais wa Zanzibar, yaani hata ikitokea (God forbid) Samia, Mpango, Majaliwa na viongozi wote wa JMH wamelipuka kwenye ndege hakuna namna Mwinyi anaweza kuwa Rais wa JMT hata kwa dawa.

Wanabodi kwa sasa iko hivi;

Samia>Dr. Mpango>Majaliwa>Dr. Tulia>Pro. Ibrahim.

Kwa leo ni hayo tu.

Wenu,
Chura wa Tuvitu Vitu🐸
 
Kwa Tanzania, Spika na Jaji Mkuu hawawezi kushikilia madaraka ya -Rais. Kila Mhimili unajitegemea. Kwa ninavyojua, kama Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu kwa pamoja hawapo nchini, basi Serikali itakuwa chini ya "Waziri Mwandamizi" Serikalini.
 
Umesema kwa unavyojua sio? Sasa soma katiba tena
 
dah umeeleweka kwahyo mwigulu si ndio waziri wa mda mrefu 😀 maara pap wa juu wote hawapo
 
Asante sana kwa kutoa ufafanuzi unaoeleweka
 
Back
Top Bottom