Nani ataitetea Tanganyika kwenye Tume ya Katiba. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani ataitetea Tanganyika kwenye Tume ya Katiba.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EasyFit, Apr 9, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  Apr 9, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Sheria ya marekebisho ya katiba mpya inapendekeza kamati ya tume iwe na majina 30, 15 toka pande zote mbili.
  Inavyoonekana Zanzibar kama nchi inawakilishwa na wajumbe 15, Serikali ya Jamhuri ya Muungano inawakilishwa na wajumbe 15. Lakini sioni nani ataiwakilisha nchi ya kufikirika Tanganyika, Tunaomba angalau majina mengine 15 yaiwakilishe ili jumla iwe 45.

  Nawasilisha.
   
 2. lidoda

  lidoda JF-Expert Member

  #2
  Apr 9, 2012
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 634
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 80
  Ndio maana nasema ingepitishwa kura ya maoni kuangalia kama Watanznia tunapenda Muungano au la. Na kama tunapenda Muungano basi hamna kuangalia wangapi wametoka bara na wangapi wametoka visiwani, uwezo tu ingekuwa ni kigezo. Na kama tutataka serikali tatu basi kila nchi yaani ya Tanganyika na ya Zanzibar zote ziandae katiba na baadae tukubaliane mambo yepi yaingie ktk katiba moja. Sasa hao wajumbe wa Bara wanawawakilisha akina nani?
  basi kwanza zitengenezwe katiba mbilTanganyika kwanza iwe na katiba yake, halafu ZNZ iwe na katika yake h
   
 3. O

  Ongeauchoke Senior Member

  #3
  Apr 9, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 150
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Zanzibar mwaka jana waliyakataa mapendekezo ya marekebisho ya Katiba. Hilo lilikuwa jambo la msingi sana. Zanzibar wana Katiba yao hivi hiyo Tume inakwenda kuandaa mapendekezo ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Zanzibar na nchi isiyojulikana!Nchi ya Tanganyika haipo mimi ningefikiri kwanza tutengeneze Katiba ya Tanganyika halafu ndipo tuwe na Katiba ya Muungano kama tunafikiria hivyo lakini wajumbe wa Tume hiyo kwa mfano Prof. Kabudi alisika akisema kuwa maswala ya Muungano yasijadiliwe kweli tuna wasomi wa namna hii halafu ndio hao wako kweye Tume tunategemea kupata kitu hapo?
   
 4. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #4
  Apr 9, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hapa kuna tatizo kubwa sana, Sasa sijui tutajadili na ile katiba ya Zenji, au tuirudishe katiba ya tanganyika kwanza au ... Yaani sielewi hiki kimzungumkuti.
   
 5. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #5
  Apr 9, 2012
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,423
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Nadhani Muungano utamfuata Nyerere si mda mrefu...maana yeyeye pekee ndio anajua maana halisi ya huo muungano wake. Kadiri kizazi kinavyobadilika logic hasa ya muungano huu inazidi kuchanganya.
   
 6. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #6
  Apr 9, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hivi kweli unaweza kutengeneze katiba ya Jamhuri ya Muungano bila kujadili muungano?
   
 7. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #7
  Apr 9, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Hili nalo neno, kamati itakapokuwa inajadili mambo yanayotakiwa yaingizwe kwenye muungano wenzetu Zanzibar wataleta katiba yao na mambo yao sisi wadanganyika tutapeleka nini mezani na nani atatusemea. Kama ni hawa 15 kina Kabudi wanajua ni kitu gani watanganyika tunahitaji au watategemea maoni ambayo hata wazanzibari watakuwa wanatoa?
   
 8. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #8
  Apr 9, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Masikini yatima (Msukule) huu sijui utazumziwa na nani?
   
 9. K

  KALABASH JF-Expert Member

  #9
  Apr 9, 2012
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 465
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35

  Mkuu EasyFit sikupati kabisa. Unasema wajumbe 15 wanaiwakilisha Zanzibar kama nchi na wengine 15 wanaiwakilisha Jamhuri ya Muungano ambamo Zanzibar pia imo ndani. Kwa maana hiyo Zanzibar ina wawakilishi 30 katika hiyo tume ya katiba! What a contradiction! Sijui ni vichwa vya aina gani vilitengeneza na kupitisha hii sheria
   
 10. J

  JokaKuu Platinum Member

  #10
  Apr 9, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,152
  Trophy Points: 280
  ..Zanzibar wameshajiandaa kuondokana na muundo wa sasa wa muungano.

  ..tena sasa hivi hata serikali 3 hawataki kuzisikia tena. wanataka kwenda kwenye arrangement kama ya east african community.

  ..msimamo wao ni mkali sana na sidhani kama Warioba,Dr.Salim,na Prof.Kabudi, wataweza kuwayumbisha.

  .
   
 11. S

  Stoudemire JF-Expert Member

  #11
  Apr 9, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 840
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Idadi sio ishu as long as wanatambua wajibu wao.
   
 12. P

  Paul S.S Verified User

  #12
  Apr 9, 2012
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Ni ukweli usiomithilika kwamba
  Asilimia karibu 90 hatujui wala kuueleza muundo huu wa muungano tulionao
  Na walioshikilia mpini hawataki ujadiliwe
  Nahisi mchakato huu wa katiba utalazimisha sasa muungano ujadiliwe na ueleweke
   
 13. nsangaman

  nsangaman JF-Expert Member

  #13
  Apr 9, 2012
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 276
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kuwepo na Serikali ya Tanganyika
   
 14. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #14
  Apr 9, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Wazanzibar tutaitetea tanganyika kwa kushawishi irudi katika katiba kwa jina lake la awali sio kama sasa inavyoitwa tanzania.
  so toeni shaka tutawatetea kwa manufaa yenu. Ikumbukwe jambo lolote halitapitishwa ikiwa halitapata baraka ya 2/3 ya kura za wazanzibar kwa hiyo hii ni nafasi ya watanganyika kuonyesha heshima kwetu ili tuwatetee.
   
 15. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #15
  Apr 9, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Na tuemwaambia wajumbe, wakipindisha lolote katika tuliowatuma itakuwa ndio mwisho wa wao kuishi zanzibar.
  Inshort kuna makundi manne yanayoendelea na kazi sasa ya kuhamasisha na yote yana baraka za serikali na hakuna kundi katika hilo linalounga mkono kuipunguzia nchi huru ya zanzibar mamlaka yake.
   
 16. T

  Topical JF-Expert Member

  #16
  Apr 9, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Grave mistake..kwa mujibu wa sheria hii wakikataa muundo wa serikali current constitution will prevail..(kitu ambacho wazenj wanajua wametegwa hapo..

  Wazanzibar wanataka Muungano wa serikali tatu..wewe ndio hujui unataka nini?

  Kkama unajua hutaki kuiwajibisha serikali yako au unataka usaidiwe na wazenj pathetic..
   
 17. s

  sweke 34 JF-Expert Member

  #17
  Apr 9, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 694
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ah vyovyote itakavyokuwa whether wanataka serikali tatu au arrangement nyingine kwangu mimi chokochoko yeyote ya kuvunja muungano naiita a blessing in disguise...!
   
 18. J

  JokaKuu Platinum Member

  #18
  Apr 9, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,152
  Trophy Points: 280
  Topical,

  ..hizo serikali 3 labda watafanya kama njia ya mpito kuelekea huko walikodhamiria.

  ..kuwa mkweli, hivi unadhani muundo wa serikali 3 utakidhi matakwa na matarajio ya wa-Zanzibari?

  ..bila ya uwakilishi UN, mabalozi wao wenyewe, uanachama ktk vyombo vya kimataifa vya fedha, mamlaka za mapato na forodha, uanachama FIFA,etc etc, mnafikiri wa-Zanzibari wataridhika kweli??

  ..halafu ukishawapa vyote hivyo, serikali ya muungano[Federal Government] itakuwa na majukumu gani??

  ..mtafanya kazi kubwa sana "kuwasomesha" wa-Zanzibar wakubali kuendelea na muungano, lakini naona mmechelewa.
   
 19. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #19
  Apr 9, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Whatever the case what i need is my beloved Tanganyika back.
   
 20. S

  Sirikali Member

  #20
  Apr 9, 2012
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 84
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 15
  JIBU HILI HAPA:

  Labda niwakumbushe mbinu za jk wakati wa kampeni kuingia ikulu:
  1. alikuwa ana kikundi cha kigaidi LAMU, kazi yake anaijua jk mwenyewe
  2. alikuwa na kikundi misikitini tz ambazo vingeongoza mapigano incase angetoswa urais

  Unga na hii:
  1. mr clean alipigwa biti na mzee kinje,"jk hasipochaguliwa lazima damu imwagike"
  2. mr clean akiwa kwenye mkutano, file la uchafu wa jk linaingia mezani, mr clean kwa kuhofu biti la kinje anawaambia wasaidizi wake "hakuna kujadili file la jk, hata kama lina uchafu, kila mtu ni mchafu".

  Mtakumbuka mr clean alisema mbele ya wana habari, nimefanya maamuzi mazito kwaajili ya hii nchi, lakini naogopa kufa, inatosha.

  Hiyo tume ipo kuandaa mazingira ya urais anayependwa na jk( mzenj au mtanganyika pure muslim).

  Wengi mnachekelea vita kati ya kambi ya mwakyembe, sitta na lowassa, lakini hamjui ndio wakristu mnajimaliza wenyewe, hapo waislamu na jk wanapata credit , hadi ifike 2015 wakristu mnakuwa hamna mtu msafi na mwenye sifa wa kuwa rais, imekula kwenu for next ten years.

  Hapo ndipo chadema itakaposhinda baada ya christian kushtuka na kugawa kura zao kwa chadema, bcoz hamtakuwa na mtu wenu kutoka ccm.

  Kwa sasa mna mtu, mtoto wa mkulima, lakini yeye ni usalama hana msaada kwenu, hawezi kwenda against na jk. Hivi unadhani LEMA angekuwa position ya mtoto wa mkulima angekubali jk afanye use.n.g.e anaoufanya sasa hivi?

  FUNGUKAAAAAAA
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...