Nani atafuatia kufa?

MAMMAMIA

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
3,811
1,603
Dogo mmoja tangu alipozaliwa hadi umri wa miaka mitano hakuwa anaweza kusema.
Siku aliyoanza kusema, alitamka neno moja tu, "Bibi".
Siku ile ile, bibi yake akafariki. Sku ya pili akatamka "Mjomba". Mjomba naye akafiriki.
Siku ya tatu akatamka "Babu", babu akafariki punde baadaye.
Familia yote ikawa haina raha, kila mmoja akiwa na wasiwasi wa kutajwa katika orodha ya dogo. Nani atafuatia baadae, baba? mama? shangazi?.....
Siku ya nne asubuhi mapema dogo akatamka "Baba".
Duh! Baba akaingiwana simanzi. Akawaaga jamaa zake, akajilaza kitandani kusubiri saa yake, lakini muda si mrefu ikaletwa taarifa kuwa dereva wa familia amepata ajali na kufariki.

Dah, umenitisha sana. Mi mwanangu ana miaka mitatu na nusu bado hajui kuongea sasa na hii stori sijui itakuwaje! Mi naanza kumwombea kila atayemtaja akianza na mimi awe tajiri.

Tunaibiwa kiingilio hapa. Anyway, i will be back to view comment.

Cjui baba atasema afadhali kwani atakuwa kesha nusurika,katambua kuwa yy c baba halali lakini je hapakuchimbika????

khaaa! Kumbe hakuwa baba wa mtoto dereva alicheza fauro
Lakini hiyo ndio iliyomwokoa

Hatari amani inatoweka jabisa
Kama ni mimi ninasamehe usaliti, maisha kwanza!
Cjui baba atasema afadhali kwani atakuwa kesha nusurika,katambua kuwa yy c baba halali lakini je hapakuchimbika????
Ningetamani kujua uamuzi wake

ha haaa haaa..................so dingi alichakachuliwa na derevantaua raaaia
Ndio, dingi alichakachuliwa, lakini naamini alshukuru kimoyomoyo kuwa yeye sie baba wa dogo!

Khaaa!! dereva alipiga vyombo hapo!! ha ha ha kwa hiyo baba atafurahi kuwa amenusurika ila sasa suala la mtoto wa dereva ndo utata mtupu

BADO HAJANUSURIKA,SI BADO ANAENDELEA KUTAJA,ANAWEZA KUTAJA'baba mlezi'

Du pia inawezekana kuwa baba alipokana kwa kuwa hakuwemo kwenye hiyo ajali

Hapo sijakupata vizuri hao waliotajwa na dogo wakafariki walikuwa na udugu na dreva wa familia au aliyedhaniwa kuwa baba wa dogo kumbe sio?

Dogo mmoja tangu alipozaliwa hadi umri wa miaka mitano hakuwa anaweza kusema.
Siku aliyoanza kusema, alitamka neno moja tu, "Bibi".
Siku ile ile, bibi yake akafariki. Sku ya pili akatamka "Mjomba". Mjomba naye akafiriki.
Siku ya tatu akatamka "Babu", babu akafariki punde baadaye.
Familia yote ikawa haina raha, kila mmoja akiwa na wasiwasi wa kutajwa katika orodha ya dogo. Nani atafuatia baadae, baba? mama? shangazi?.....
Siku ya nne asubuhi mapema dogo akatamka "Baba".
Duh! Baba akaingiwana simanzi. Akawaaga jamaa zake, akajilaza kitandani kusubiri saa yake, lakini muda si mrefu ikaletwa taarifa kuwa dereva wa familia amepata ajali na kufariki.

Angekuwa wangu ningemchinja asije akamaliza ukoo bure. Heri afe yeye mmoja kuliko kuimaliza familia nzima, khaaaa!

Hapo sijakupata vizuri hao waliotajwa na dogo wakafariki walikuwa na udugu na dreva wa familia au aliyedhaniwa kuwa baba wa dogo kumbe sio?

Bora umenisaidia kuuliza swali mkuu maana hata mimi nilitaka kuuliza hlo swali...

Kwa kuwa haikutajwa kama waliokufa ni jamaa zake dogo toka familia ya baba yake hawa Bibi, Babu na Mjomba inaonesha walikuwa walikuwa na uhusiano na dogo kwa upande wa mama yake tu.

Hapo nimekusoma mkulu safi na wikiend njema

Back
Top Bottom