Nani Atafika Salama: Freddie au Eddie?

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
12,865
2,000
Mjengwa kauliza swali tamu sana kule kwenye blogu yake http://mjengwa.blogspot.com/
Amesema hivi:

frededward.jpgWachukuliwe kwa gari wote wawili. Washushwe Magomeni Mwembechai kisha waambiwe; tembeeni kwa miguu bila walinzi wala wapambe. Mkatishe Tandale, Manzese Uzuri na mwisho mtokee Sinza Kijiweni. Naamini Fred angefaulu kukatisha na labda kuna wawili watatu njiani wangemwuliza maendeleo ya mashamba yake ya Kibaigwa na ng'ombe wake kule Kibaha. Vinginevyo, pamoja na kashfa zake za mashamba ya Kibaigwa, Mkopo wa milioni hamsini Nssf na safari ya Marekani iliyogharimu shilingi milioni mia tano, bado Fred angekanyaga Sinza Kijiweni akipiga miruzi na mikono mfukoni. Lakini, kwa joto hili la sasa la Richmond na hasira za wananchi, nahofia Edward safari yake ingeishia Tandale. Labda wanakijiji wenzangu mna mtazamo mwingine.
 

Pundit

JF-Expert Member
Feb 4, 2007
3,738
1,225
Huko watu hata hawamjui Freddie wala Eddie, akishaonwa suti sop sop anaonwa ulaji tu watu wanachukua vyao.Unafikiri amteja wanamjua hata former PM?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom