Nani anishawishi nipende kulipa kodi Tanzania'

REMSA

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
2,577
1,225
1.Watoto wangu ninasomesha English medium nalipa ada kubwa,hii ni kwa sababu shule
za serikali ni duni'

2.Ninaishi Segerea maeneo ya Mandela,barabara ni mbovu labda kuliko zote hapa mjini,
mvua ikinyesha usiku hatuna uhakika wa kwenda kazini,ikinyesha mchana hatuna uhakika
wa kurudi majumbani.maana hata bodaboda haziwezi kwenda'

3.Maji nanua lita 3000 sh.30,000. kwa wiki,hivyo kwa mwezi natumia sh.120,000.maana hakuna maji
ya bomba wala visima.

4.Hatuna usafiri wa uhakika kwa sababu ya ubovu wa barabara ila bodaboda.

5.Mbunge wetu ni Makongoro Mahanga,tangu alivyokuja kuomba tumpe kura hatujawahi kumuona
tena mpaka leo.

Katika mazingira haya ni kweli naweza shawishika kulipa kodi kwa hiari na kupenda,nakatwa Payee
kwa sababu sina jinsi lakini sioni umuhimu wake,nalazimishwa niikopeshe serikali hela ya kununua
EFD kwenye biashara ili serikali ikusanye kodi ambayo sioni umuhimu wake.Ki ukweli naumia sana ndani
mwangu ktk mazingira haya nani ananishawishi kwamba Slogan ya "LIPA KODI KWA MAENDELEO" ni sahihi'
 

rodrick alexander

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
8,268
2,000
unafungua biashara ambayo unahitaji umeme lakini hupati umeme hapohapo unalipia frem ya biashara kodi kwa mwaka,unalipa wafanyakazi,leseni inalipiwa ni kweli hata mimi huwezi kunishawishi nilipe kodi
 

Mokoyo

JF-Expert Member
Mar 2, 2010
15,172
2,000
Kulipa kodi Tanzania inaumiza sana moyo, binafsi ninapoweza kukwepa nakwepa
 

lyinga

JF-Expert Member
Nov 18, 2013
2,498
0
Elimu ya uraia inahitajika sana hapa kwetu tanzania wanatumia umbumbu tuliokuwa nao kuzidi kutuharibu kisaikolojia hembu tujiulize anasimama rais au waziri na hawa watawala wengine wanajinadi tutajenga barabara au wamejenga barabara, dhule za kata sijui wamechimba visima wakati vitu vyoote hivyo ni haki na nilazima viwepo tena vyenye ubora kwavile kila kicha cha mtanzania kinalipa kodi, mfano ukinunua chochote tayari kuna kodi utakuwa umelipia hapo, ukitumia usafiri hapo kuna kodi umelipia chamuhimu ni elimu ya uraia isambazwe nchini kote hawa viongozi waache kutuibia wananchi
 

IDUNDA

JF-Expert Member
Oct 31, 2013
457
0
sheria ndiyo itakushawishi na kukulazimisha ulipe kodi. itafika kipindi hautakuwa na jinsi ila kulipa tu kwasababu usipofanya hivyo utawekwa lupango.
 

REMSA

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
2,577
1,225
sheria ndiyo itakushawishi na kukulazimisha ulipe kodi. itafika kipindi hautakuwa na jinsi ila kulipa tu kwasababu usipofanya hivyo utawekwa lupango.

Kwa sababu ya kutumia sheria na mabavu ndio inawafanya watu wengi wanakwepa kulipa kodi,si kweli
kwamba kodi inayolipwa ndio inayostahili kulipwa Tanzania,hii ni kwa sababu watu hawaoni umuhimu wa
kulipa kodi kwa sababu hawana msaada nayo ila ni kwa maslahi ya wachache.Unaposema sheria itanibana
je nikimuuzia kitu mtu nisimpe risiti nitakuwa nimelipa kodi?'
 

Belo

JF-Expert Member
Jun 11, 2007
12,625
2,000
Kulipa kodi ni mojawapo ya vitu nisivyovipenda kungekuwa na option ya kukwepa nisingelipa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom