NANI ANAYETAKIWA KUFANYA KAZI ZA MWENYEKITI WA MTAA ENDAPO HAYUPO AU ANAUMWA?

Adolph Sendeu

JF-Expert Member
Apr 21, 2009
269
250
Naomba kuuliza maswali kama ifuatavyo
1. Endapo mweyekiti wa mtaa anaumwa au amesafiri
a) ni nani anatakiwa kufanya kazi zake na anapatikanaje na kwa sharia au kanuni ipi?
b) Mhuri wa mwenyekiti anatakiwa auache au ukae kwa nani
c) Nani ataongoza vikao vya halmashauri ya mtaa
d) Je akidi ya kikao cha halmashauri ya mtaa ni wajumbe wangapi
e) Je halmashauri ya mtaa ya wajumbe 6, kwa maana ya mwenyekiti na wajumbe wake 5, wajume 2 wakihama mtaa, je halmashauri hiyo ina hadi ya kuendelea kuwa halmashauri

2. katika kikao cha mtaa/mkutano wa mtaa, wajumbe wa mkutanao ni wajumbe 6 wa halmashauri ya mtaa na wananchi wenye umri wa Zaidi ya miaka 18 waakazi wa mtaa husika. endepo mwenyekiti hayupo, mwenyekiti wa kuongoza kikao husika huteuliwa toka wajumbe wa mkutano. Je sharia inasemaje hapo? atateoliwa toka wajumba wale 5 wa halmashauru au toka wajumbe wote waliohudhuria katika kikao?
 
Top Bottom