Nimekuwa nikijiuliza mara nyingi ni nani hasa anayepaswa kusimamia uendeshwaji wa mashule na elimu hapa Tanzania?
Shule nyingi ni za kata ambazo ndio huhudumia wananchi walio wengi.Lakini kumekuwa hakuna walimu wa kutosha na hata vifaa vya kufundisha pengine hata chaki tu. hata sasa wengi wankwenda kufanya mitihani ya kumaliza shule, ytutegemee nini?
Zipo taasisi nyingi tu ambazo zinakusanya michango kutoka sehemu mbalimbali mf.Mfuko wa kuchangia elimu, hata WAMA n.k ambazo lengo lao eti ni kuinua hali ya elimu Tanzania. Lakini sielewi ni elimu gani inayoendelezwa hapa, au elimu za matumbo yao.
Wapo pia matajiri na wafanyabiashara wanaojidai kuchangia maendeleo ya elimu; lakini nao wanaoenda kuchangia sehemu ambapo wanaweza kulamba mkono.Mfano gazeti la the guardian 18 linamwonyesha mengi akiwa katika sherehe ya kuwaaga wanafunzi wazo hill sekondari, watoto wanaahidiwa milioni moja moja na ma-compyuta, katika shule zenye uwezo-wenyewe wanaiita international(au english medium).
Maswali yangu ni:
1. Ni nani hasa anayesimamia shule zetu za walalahoi, kuanzia primary hadi sekondari ambazo zina watoto wa watanzania weeeengi sana.
2. Kwa nini viongozi wakubwa na wafanyabiashara wanapenda kwenda kwenye shule za matajiri ambazo mimi naamini zinawanyonya tu watanzania wenzetu wanaoenda kusomesha watoto wao huko.
3. Kwa nini wasiajiriwe na kufundishwa walimu wengi wenye sifa wakalpiwa vizuri,katika mashule yetu haya ya kata??tukapunguza watoto wetu kusafiri umbali mrefu kwenda kutafuta shule 'nzuri'
4.Hii michango inayokusanywa kila pembe kuhusiana na elimu inainua elimu ipi na vipi?
5.Ni vipi serikali inasimamia unedeshwaji wa mashule haya yanayojiita ya international, kwani kumekuwa na wimbi la kujipangia bei/karo wanavyotaka tu wao.Ugumu upo wapi kwa serikali kubadili mitaala ya elimu iwe inafundishwa kiingreza tupu-kama ndicho wanachoona bora?
6.Nini mpango wa serikali kuboresha elimu kuanzia chini hadi juu?
7. Kiongozi anayesubiri kualikwa kwenye mashule ya wenye hela anatusaidiaje?
8. Tutegemee nini kwa matokeo ya mitihani ya la saba la form4 kwa mashule yetu yalee??? aaaah Tanzania!!!!