Nani anayekabidhiwa fedha ya Dowans? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani anayekabidhiwa fedha ya Dowans?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jan 2, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jan 2, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,799
  Likes Received: 83,172
  Trophy Points: 280
  Nani anayekabidhiwa fedha ya Dowans?


  [​IMG]
  Na Saed Kubenea - Imechapwa 22 December 2010

  [​IMG][​IMG] Gumzo la Wiki


  [​IMG]


  WAZIRI Mkuu wa Jamhuri, Mizengo Pinda amejitwisha zigo lisilobebeka. Litamuangusha. Ameahidi kulipa mabilioni ya shilingi kwa kampuni ya kufua umeme wa dharula, Dowans Holding Tanzania Limited.

  Akizungumza na waandishi wa habari Ijumaa iliyopita, ikulu jijini Dar es Salaam, Pinda alinukuliwa akisema, “…Nchi hii inaendeshwa kwa utawala wa sheria. Tutakata rufaa, lakini tukishindwa, basi itabidi tulipe…”

  Pinda, hata hivyo, amenukuliwa akisema, hukumu hiyo ni matokeo ya genge la watu wachache wanaofahamika; ambao wameamua kutafuna rasilimali za taifa bila huruma.

  Tarehe 15 Novemba 2010, Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara (ICC), iliagiza serikali kuilipa kampuni ya Dowans fidia ya Sh.185 bilioni kutokana na kile kilichoitwa, “Kukiuka masharti ya mkataba.”

  Kampuni ya Dowans ilipata kazi hiyo baada ya kurithi mkataba wa kufua umeme kutoka kwa dada yake – Richmond Development Company (RDC), ambayo ilibainika baadaye kuwa haikuwa na hadhi, sifa wala uwezo wa kupewa kazi iliyoomba.

  Sasa kabla ya Pinda kuagiza watendaji wa serikali kulipa mabilioni hayo ya shilingi na kugeuza taifa hili kuwa kichaka cha wajanja wachache kuvuna wasichopanda, kwanza ni lazima aeleze: Nani aliyefikisha serikali hapa ilipo katika sakata hili?

  Pili, hicho ambacho waziri mkuu anaita, “genge la watu wanaofahamika,” ni akina nani? Nani anayewalinda serikalini na kwa maslahi yapi hadi yeye anashikwa na kigugumizi cha kusema, “Basi, tutalipa…?”
  Tatu, kabla ya hundi ya malipo kuandikwa, waziri mkuu aeleze nani anayekabidhiwa fedha hizo?
  Mpaka sasa, serikali haijataja mmiliki wa Dowans na wala haijataja mahali anakoishi?

  Haya ni muhimu yajulikane mapema kwa sababu, aliyetajwa kuwa “mmiliki” wa Dowans Holding Tanzania Limited, Bregedia Jenerali Sulaiman Mohammed Yahya Al Adawi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) amekana, mara mbili, kumiliki kampuni hii.

  Naye mfanyabiashara na mbunge wa Igunga, Rostam Aziz ambaye aliwahi kunukuliwa akisema, “Mimi nawafahamu Dowans, si Richmond,” hajataja hadharani mmiliki wa Dowans nchini.

  Nako ndani ya Bunge, si serikali wala Kamati Teule ya Bunge iliyotaja mmiliki wa Dowans.

  Badala yake, Kamati Teule iliyoongozwa na mbunge wa Kyera, Dk. Harrison Mwakyembe iliishia kusema, “Richmond ni mradi wa mkubwa…”
  Hadi sasa huyo mkubwa hajulikani ni nani. Je, uhusiano wake na hicho ambacho waziri mkuu anaita “genge la watu linalofahamika,” ni upi?

  Jingine ambalo Pinda anapaswa kulifahamu ni hili: Mwenye uwezo wa kulisema hili kwa ufasaha na akatosheleza majibu ya wananchi, ni Rais Jakaya Kikwete na aliyekuwa waziri wake mkuu, Edward Lowassa.

  Kikwete ndiye aliyeongoza kikao cha Baraza la mawaziri kilichopitisha maamuzi ya kuipa kazi Richmond ambayo haikuwa na uwezo wa kufanya kazi iliyoomba.
  Mara kadhaa, Kikwete amekiri kwamba alikuwa anafuatilia kwa karibu shughuli za Richmond. Kuna wakati alisema aliwahi kumuagiza waziri wake kutoilipa kampuni hiyo kwa vile tayari ilidhihirika kuwa ni kampuni ya kitapeli.

  Kigugumizi cha rais kushindwa kuchukulia hatua watuhumiwa wakuu wa Richmond na dada yake Dowans, kunazidi kusisitiza kuwa “Richmond ni kampuni ya wakubwa.”

  Kamati Teule ilipendekeza kwa mamlaka za juu za uteuzi kuwaondoa kazini Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru), Edward Hoseah, aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali, Johnson Mwanyika na aliyekuwa katibu mkuu wizara ya nishati na madini, Athur Mwakapugi.

  Bunge lilitaka pia hatua za kisheria zichukuliwe kwa wote ambao walionekana wazi kutenda jinai.

  Ndani ya Bunge, Hoseah alituhumiwa kuibeba Richmond. Kamati Teule ilisema Hoseah aliaibisha serikali kwa kusema, “Mkataba ulikuwa halali na hakuna harufu ya rushwa ndani yake.”

  Hadi sasa, Hoseah hajajiuzulu, wala rais Kikwete hajamfuta kazi. Badala yake rais alimteua kwenye kamati yake ya kufuatilia walioiba Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
  Johnson Mwanyika kama ilivyokuwa kwa Hoseah, naye alibaki katika nafasi yake hadi alipotimiza muda wake wa kustaafu. Naye aliingizwa kamati ya rais ya kufuatilia mafisadi waliokwapua mabilioni ya shilingi BoT.

  Kosa la Mwanyika ni kushindwa kushauri serikali; kuzembea katika usimamizi wa mkataba; na kushindwa kuangalia maslahi ya umma katika mkataba.
  Kimsingi uzembe wa Mwanyika, iwapo hakutenda hayo kwa maelekezo ya juu, ndiyo yaliosababisha serikali kulipa fedha hizo.

  Naye Lowassa alitajwa kuwa ndiye aliyekuwa akiagiza, kushinikiza na ndiye aliyeibeba Richmond na kuifikisha hapo ilipofika.

  Mathalani, baadhi ya nyaraka zinaonyesha aliyekuwa waziri wa Nishati na Madini, Dk. Ibrahim Msabaha, alibakia kama karani wa kutekeleza maagizo ya Lowassa.

  Akitii kile alichoita maagizo ya Lowassa, 21 Juni 2006, Dk. Msabaha aliandikia Mwakapugi akisema, “…Andaa barua kwa mwenyekiti wa bodi ya Tanesco kumuagiza aingie mkataba na Richmond haraka iwezekanavyo. Nakuletea nakala ya kibali kutoka ofisi ya Mhe. Waziri Mkuu kwa kumbukumbu za wizara.”

  Lakini kama haya ndiyo maagizo ya Dk. Msabaha kwa Mwakapugi, nani aliyeagiza Lowassa kuipa kazi Richmond? Maana kwa vyovyote vile, Lowassa hawezi kutenda haya peke yake.

  Ni Msabaha anayedaiwa kuandika katika baadhi ya nyaraka kuwa “suala la kushughulikia mashine za umeme wa kukodi limekwisha kushughulikiwa na waziri mkuu Lowassa?”

  Je, kwa nini Lowassa ajipe kazi hii wakati kazi ya kutafuta mashine hizo ilikuwa ya kitaalamu na Lowassa si mtaalamu wa masuala ya umeme?
  Aidha, kama hayo ndiyo maagizo ya Lowassa kwa Dk. Msabaha, kwa nini waziri Msabaha aliyatekeleza wakati alijua wazi kuwa tayari kuna walakini wa uhalali na uwezo wa Richmond?
  Mashaka ya uwezo wa Richmond kumudu kufanya kazi yanadokezwa na kauli ya Lowassa katika barua yake ya 21 Septemba 2006 kwenda kwa Dk. Msabaha.
  Lowassa katika barua hiyo anasema, “…Yapo maneno mengi sana yanasemwa kuhusu uwezo wa Richmond kuagiza Gas Turbines... Inawezekana hivi vikawa ni vita vya kibiashara… Ni vizuri ukajiridhisha kwamba kampuni hii itaweza kutekeleza kazi hiyo…”

  Kujitosa kwa Lowassa katika sakata la Richmond/Dowans halipo kwenye kuagiza Dk. Msabaha na Timu ya Majadilino ya Serikali (GNT) pekee.
  Barua ya Msabaha ya 17 Juni 2006, siku sita kabla ya mkataba wa Richmond kusainiwa, inaonyesha alivyoelezwa jinsi majadiliano yalivyokwenda hatua kwa hatua kati ya GNT na Richmond na jinsi utekelezaji wa mkataba utakavyokuwa.
  Lowassa alijulisha yote aliyoyatenda kwa rais Kikwete. Je, Kikwete alichukua hatua gani mpaka sasa wanataka kulipa “kikundi hiki kidogo cha watu” mabilioni ya shilingi?

  Lakini kuna jingine: Baada ya serikali kujiridhisha kuwa Richmond haiwezi kutekeleza mkataba wake iliyofunga na Tanesco 23 Juni 2006, baadhi ya vigogo serikalini walishinikiza kampuni hiyo kuhuisha mkataba wake kwa Dowans.

  Je, nani aliyemtuma Nazir Karamagi kufanya kazi hiyo na kwa faida ya nani wakati ambapo mkataba kati ya Tanesco na Richmond ulikuwa tayari umevunjika? Ni vema Pinda ataje aliyemtuma Karamagi.

  Kwa inavyoonekana, Karamagi hakuwa peke yake. Je, alishirikiana na nani? Nani alimuagiza? Rais Kikwete, Lowassa au alitenda hayo kwa shinikizo la Rostam Aziz?

  Jingine ambalo linahitaji ufafanuzi ni hili: Wakati Richmond inaomba kazi iliyopewa, haikuwa na fedha za kuendesha mradi. Huo ndiyo msingi wa kutaka serikali iidhamini kwa kufungua LC – dhamana.

  Kamati Teule ya Bunge imethibitisha; Karamagi aliyesimamia uhamisho wa mkataba naye amekiri pia, kwamba Richmond haikuwa na uwezo, ujuzi wala fedha za kufanya kazi iliyoomba.

  Sasa kwa nini serikali inataka kulipa watu ambao hawakuwa na fedha?
  Ni lazima Pinda afahamu kuwa huwezi kuitenganisha Richmond na Dowans. Hii ni kampuni inayomilikiwa na watu walewale, lakini walioamua kuzitambulisha kwa majina mawili tofauti.

  Ushahidi wa hilo ni jinsi Richmond ilivyoruhusiwa kuhuishaji mkataba wake.
  Hakuna mahali popote panapoonyesha Richmond iliwahi kutangaza tenda ya kutafuta mbia; badala yake yote yaliyofanyika yalitendeka kwa siri na yakishirikisha baadhi ya viongozi serikalini.

  Kwa mfano, kwa nini Karamagi alihamisha mkataba wa Richmond kwenda Dowans, wakati tayari kampuni hiyo ilishindwa kazi; mvua tayari zilishaanza kunyesha na mabwawa kujaa?

  Hoja kuu ambayo Pinda na wenzake wanasimamia katika kuhahalalisha malipo ya Dowans, ni “serikali hii inafuata misingi ya sheria.”
  Lakini serikali inayofuata misingi ya sheria, haijalipa fidia wananchi wake hata baada ya kushinda kesi mahakamani.

  Tokea mwaka 1986 wananchi wa kijiji cha Kitondoloni, wilayani Kisarawe mkoani Pwani, walihamishwa ili kupisha kilichoitwa “shughuli za jeshi.”
  Kupitia waziri wa fedha wa wakati huo, Kighoma Malima, serikali ilikubali kuwalipa stahiki zao, lakini hadi leo hii ahadi ya serikali haijatekelezwa.
  Hata baada ya hukumu ya Jaji Khamisi Msumi ya 18 Novemba 1996, iliyowapa haki yao ya kufidiwa, bado serikali haijawalipa Ally Mwang’omba na wenzake 143 katika kesi Na. 144 ya mwaka 1996.

  Ni serikali hii, ambayo Pinda anasema inafuata utawala wa sheria iliyogoma kulipa wafanyakazi zaidi ya 40 wa lililokuwa Shirika la Bima la Taifa (NIC) waliosimamishwa kazi tokea mwaka 1998.

  Kesi ya watumishi hawa ambayo hata baadhi ya wafanyakazi wa serikali waliipachika jina la “kesi ya kuchonga,” ilichukua miaka 11 na ilifutwa mapema mwaka huu kwa kile serikali ilichoita, “Hakuna tena sababu ya kuendelea na shauri” hilo.

  Katika kipindi chote hicho, wafanyakazi hawa walikuwa wanalipwa nusu mshahara. Baadhi yao wamefariki. Lakini serikali imegoma kulipa hata vizuka.
  Wapo ambao watoto wao wameshindwa kwenda shule kwa kuwa wazazi wao hawana tena kipato na Pinda na serikali yake imegoma kuwalipa.

  Orodha ya kesi ambazo zimeamuliwa mahakamani, lakini serikali haijalipa wanaostahili, ni nyingi na nzito hata kuliko Dowans.
  Tokea mwaka 1989 serikali imeshindwa kumlipa mfanyabiashara Devram P. Valambhia. Hata pale iliposhindwa katika mahakama ya rufaa kwa zaidi ya mara 10 bado serikali iliendelea kugoma kulipa fedha hizo hadi akaaga dunia akiwa masikini na dhaifu.

  Kama haya yalifanyika kwa Valambia, kwa nini serikali isiyafanye kwa Dowans? Au ni kweli kwamba Dowans ni ya vigogo ambao wanadai wameiweka serikali kiganjani?


  Tutafakari Watanzania....
   
 2. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #2
  Jan 2, 2011
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  At times, you have to swallow the bitter pill to proudly accept Tanzanian as your nationality! :((
   
 3. m

  mzambia JF-Expert Member

  #3
  Jan 2, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  mh son of peasant naye yumo?
   
 4. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #4
  Jan 2, 2011
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mh!!!!
   
 5. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #5
  Jan 2, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,315
  Likes Received: 5,609
  Trophy Points: 280
  Kamata watu 6 tuu nchi itaenda hakuna fisadi tena hapa tz....kamata hao tu..RA,EL,JK,Chenge,Mkono,Jeetu na Shivacom pamoja na Manji!!!waliobakia wote wataacha unafiki na ufisadi!!!

  Pia wanasheria wote waliofungua makampuni fake kwenye ofisi zao...futa vibali na tia ndani wote...IMMA na Malegesi!na REX
   
 6. nyondoloja

  nyondoloja Senior Member

  #6
  Jan 2, 2011
  Joined: Nov 10, 2010
  Messages: 190
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  inasikitisha sana uhaba madawa hs,vifaamashureni,miundombinumibovu,umeme ndousiseme
   
 7. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #7
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  wazee wa afrika mashariki watazipokea?
   
 8. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #8
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Baba wa Taifa alitaifisha mashamba, mabenki na majumba (Msajili wa majumba) Idd amini aliwatimua wahindi wote, hivi tusipowalipa dowans tukawalipa wazee wetu wa E.A.C. wanaogoma nani atatufuata kutudai deni la kutunga la dowans ambao wamekuja na vi briefcase tu wakatukuta tuna mito mingi, mabwawa na maziwa mengi kuliko nchi yoyote Africa na mabara yote lakini umeme juu. Jamani hata maji ya mtera, nyumba ya MUNGU, Hale ni yetu bado tunadaiwa? kweli kamba sasa kali iko siku tutatoa hukumu za ki-China (kifo kwa wahujumu) hata kama wametoka madarakani kwa mafisadi hawa
   
 9. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #9
  Jan 2, 2011
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  There should be an end to all these. That day will come.

  Hakuna marefu yasiyo na mwisho.
   
 10. F

  Fenento JF-Expert Member

  #10
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 320
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Haya masuala ya Ufisadi yanatumaliza sisi watanzania wa hali ya chini. Ebu wasomi na wanaharakati tujaribu kuyasema hayamambo kwa watanzania ambao wapo vijijini hawaambiliki na ccm yao.Tumechoka
   
 11. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #11
  Jan 2, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hivi tusipolipa hiyo fidia nini kitatokea
   
 12. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #12
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Rostam Hazizi ndiye atakayelipwa. Kulingana na taarifa zinazotoka na uamuzi wa hivi majuzi;mnamo tarehe 28/1/2006 Rostamari alipewa 'power of attorney" na Dowans, ambayo pia ilinakiliwa CRDB ambapo iliko akaunti ya kampuni hiyo.
   
 13. M

  MAMA B Member

  #13
  Jan 2, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  TUNAHITAJI JESHI LIONGOZE HII NCHI.........:angry: WATU WANAOTAKA AMANI MATENDO YAO YATAKUWA YANAONYESHA KWELI NI WA AMAN........ ILA KUNA MTU ANAONGEA MDOMON TU ANATAKA AMAN LAKINAI VITENDO VINAONYESHA NI WA SHARI......CCM ANGALIEN MNAYOYAFANYA MAANA MWISHO JESHI LITACHUKUA MWELEKEO ATA KAMA HATUTAKI
   
 14. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #14
  Jan 2, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,799
  Likes Received: 83,172
  Trophy Points: 280
  Kampuni inaingia nchini kwa kuidanganya serikali kwamba ina utaalamu wa kufua umeme na makao makuu yao yako Houston, TEXAS. Hawana hata dollar 1 au shilingi moja ya kununulia mitambo. Serikali inawapa dhamana na hivyo kupata mkopo mkubwa toka benki ya biashara na kufanikiwa kuagiza mitambo inayohitajika. Mitambo inawasili lakini jamaa hawana utaalamu wowote wa kufua umeme na wanashindwa kuzalisha hata tone moja la umeme. TANESCO inaamua kuvunja mkataba baada ya ile dhana ya Wataaalamu wa TANESCO na kuishauri Serikali kutoingia kwenye mkataba na kampuni hii kutokana na ukweli kwamba haijawahi kufua umeme sehemu yoyote ile duniani kuwa kweli

  Katika hali ya kutatanisha inaibuka kampuni nyingine inayoitwa Dowans ambayo wamiliki wake hawajulikani na kurithi utapeli ambazo uliokuwa unafanywa na Richmond wa kupokea malipo toka TANESCO pamoja na kuwa kazi waliopewa iliwashinda. Dowans wanataka kuichukua mitambo yao kwenda kuiuza nchi za nje, lakini TANESCO wanasema tumewalipa wale Richmond mapesa mengi sana bila kufanya kazi yoyote hivyo wanastahili kwanza kutulipa pesa zetu kisha ndiyo tuwaruhusu kuchukua mitambo yenu.

  Dowans kwa kujua wameshashtukia ndani ya Tanzania wanaenda kufungua kesi nje ya nchi na hatimaye hukumu kutolewa ya kuitaka TANESCO iwalipe fidia matapeli wa Richmond/Dowans ambao mpaka sasa hawajulikani ni akina nani shilingi 185bn wengine wanadai ni 90bn.

  Hii inawezekana katika nchi ambayo tunaweza kuita kichwa cha mwendawazimu au Tanzania ambapo kampuni inaingia nchini bila hata senti tano, kuidanganya Serikali, kushindwa kufanya kazi waliyokabidhiwa baada ya kupewa mkataba, wamiliki wa kampuni hiyo hawajulikani na sasa inakaribia kulipwa kitita cha hali ya juu na TANESCO kitu ambach kinaweza kabisa kuifilisi TANESO na kushindwa kufanya kazi zake kwa miaka mingi ijayo au hata kufa kabisa.

  Mungu ibariki Tanzania
   
 15. T

  Topical JF-Expert Member

  #15
  Jan 2, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Sijawahi kumuelewa Pinda, I am sorry...

  Naona kama Harmless/Powerless/

  Anafanya kazi kama hataki, kalazimishwa, bored, anyway
   
 16. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #16
  Jan 2, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Mwaka 2005 walitumia EPA, This time wanatumia DOWANS, huu ni mkakati mahsusi wa wahujumu uchumi ndani ya CCM kuchota pesa za wananchi kwa ajili ya kuhakikisha wanaweka mtu atakayeendeleza na kulinda maslahi yao katika uchaguzi wa 2015. Samuel Sitta alipiga kelele kishapewa tahadhari anyamaze kwa masilahi ya chama. Ukiona watu waliopewa dhamana ya kuwa custodians wa mali zetu wanakubali mwizi kuingia na kuiba ujue kuwa huko vichakani wana mgao wao.

  Wajanja wa Dowans wameingia mkataba na watawala kuwa walipwe na percentage fulani iingie kwenye Chama cha mapinduzi kwa ajili ya uchaguzi wa 2015. Huo ndiyo ukweli wenyewe na asiyekuwa na masikio basi. We uliona wapi baada ya mtu kuhukumiwa kunyongwa anatamka kuwa atakata rufaa ila akishindwa atakubali tu kunyongwa japo hana hatia?, mtu huyu ni dhahiri amechoka kuishi na amefurahishwa na hukumu ya kifo. A fighter always going for the winning strategy not losing strategy, on DOWANS our custodians are for losing strategy that's why the've lost.

  Let them say, Tanzania didn't had patriotic leaders, let them say their hardship is the result of our cowardness and failure to safegurad their resources. They will hunt all of those who advocated for their failure, trace their siblings and bring back their resources and punish the culprits, that's what our sons and daughters are going to do in the future.
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #17
  Jan 2, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,799
  Likes Received: 83,172
  Trophy Points: 280
  Thank you Mkuu!

   
 18. N

  Nonda JF-Expert Member

  #18
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  mkuu,
  Kosa moja kubwa ambalo mwalimu alilifanya ni hilo la ku-politise Majeshi yote nchini.. wakuu wa jeshi, "usalama wa taifa" na wakuu wa polisi ni wanasiasa zaidi.

  Wao wanatumika kuuilinda CCM au wajanja wachache wanaoongoza CCM.
  Mkuu CCM wameweza kutuchakachua waTZ sote, including hao wanajeshi...

  Kwa Mwalimu ilikuwa ni mbinu ya kuzuia uwezekano wa kupinduliwa lakini kwetu sisi, leo ndio limekuwa ni jinamizi. They side with CCM na kuuacha umma unadidimia katika ufukara na umasikini.
   
 19. N

  Nonda JF-Expert Member

  #19
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Mtu mwenye "power of attoney" ameshajitokeza au vipi? Ndiye atakayelipwa hiyo kodi anayokamuliwa mlalahoi.
  Wanamkamua mlalahoi mpaka atie akili, aache ukondoo. na bei za umeme, vyakula,usafiri juu, ampaka fahamu na akili zirudi.
   
 20. M

  Matata Member

  #20
  Jan 3, 2011
  Joined: Mar 28, 2006
  Messages: 23
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 5
  It is just matter of time, hawa viongozi na familia zao kuna siku watafikishwa mahakamini na mali zao zitataifishwa. Tumeona nchi kama Chile na Arigentina vingozi wao walioiba na kuhujumu uchumi wa nchi zao wamefikishwa mahakani wakiwa na miaka zaidi 80. Wengi walifungwa, wengine walihukumiwa vifo na mali zao na familia zao zilitaifishwa, kwa hiyo genge la Kikwete na Mkapa linasubiri muda ufike. It is matter of time.
   
Loading...