Nani anayakumbuka ya Mugabe uwanja wa Uhuru kuapishwa kwa Ras Kikwete!

nzagambadume

JF-Expert Member
Apr 9, 2018
2,430
5,769
Nani kasahau shangwe alilopigiwa Robert Mugabe 2005 kwenye sherehe za kuapishwa Rais kikwete kwenye uwanja wa shamba la bibi?ilikuwa ni balaa,kwa mujibu wa ufahamu wetu wakati huo ilikuwa ni kwamba Mugabe ni mkombozi wa weusi wa zimbabwe anapambana na mabeberu na kachukua mashamba yao kawapa wanyonge na kwamba yanayosemwa na IMF na world bank ni propaganda tu za mabeberu.

Nakumbuka mwaka 2004 nikiwa katika harakati za ku hustle huko enfield north london nilipata temporary job moja ya catering kupitia Reed employment kwenda kuhudumia katika mbio za farasi ziitwazo Royal ascot

Kwenye van tulikuwa waafrika watupu ikaja topic ya mugabe katika mazungumzo mimi nikawa kimbelembele kumsifia,aisee gari ilkuwa nusu ni wazimbabwe wakitaka wanigawane kwa hasira hadi dereva mturuki akasimamisha gari na kutaka kunishusha nakumbuka niliomba radhi na kuongezea neno la kiarabu kiswahili TAFADHALI akaishia tu kucheka tukaendelea na safari kwenda mzigoni lakini tulipofika mama mmoja wa kizimbabwe akanisihi nisiamini propaganda za Mugabe na kuniambia hali ya raia ilikuwa mbaya waliokuwa wanafaidika ni wapambe wake tu

MORAL OF THIS STORY IS:nimeshangaa sana kuona wa ccm wakipigia kelele clip eti magufuli kashangaliwa South africa anakubalika,For God sake kila Rais aliyeshuka alishangiliwa hadi dikteta museveni alipigiwa shangwe,kama ni shangwe basi makofi aliyopigiwa kikwete kwa hotuba yake kali siku ya kuaga mwili wa mandela yalikuwa na maana kubwa zaidi

KAMA 2005 TULIMSHANGILIA MUGABE tukidhani anapambana na mabeberu kumbe nyumbani kumeoza wapambe wake wakitajirika na maskini hali kuwa mbaya cha kushangaza ma dikteta wakishangiliwa huko nje ni nini?

Hakuna mtu mjanja kama Kagame kwa kutumia baadhi ya waandishi kutengeneza imgae yake kimataifa ,kwa huyu wetu ni rahisi sana mtu aliyeko malawi aus south africa kusoma kwamba Rais wa Tanzania anatunishiana misuli na wazungu wa madini wakaona ni mzalendo kumbe hawajui hali halisi ya raia mtaani na hela zinavyopigwa kibabe plus haki za kiraia kuminywa,kama majirani tu kenya walibabaika na zile mbwembwe za kusafisha soko,kutembea kwa miguu kwenda BOT ,kubana matumizi kwa kuzuia sherehe hadi wakaanza kuomba akatawale kwao sembuse hao wa kusini?

NYONGEZA:mika hiyo ya 2005 hadi msanii wa bongo fleva Crazy GK alitoa nyimbo inaitwa simba wa afrika eti Mugabe naye akasifiwa huko ndani ni simba wa Afrika

AMA KWA HAKIKA USILOLIJUA NI USIKU WA GIZA.
 
Inaonekana hili tukio limewauma sana sana mpaka mnaleta stori za Alfu lela ulela.
Ushauri:sumu ya panya inauzwa shilingi 200 tu nyote mnakaribishwa.
tunawaelimisha sisi ni anti virus, viruses zikileta ujinga tunaziangamiza na kufanya fumigation. It is war against fake news.
 
tunawaelimisha sisi ni anti virus, viruses zikileta ujinga tunaziangamiza na kufanya fumigation. It is war against fake news.
Mkuu wewe unacheza na kichapo cha Mungu, huyo Kikwete mnaejifanya kumsifia sasa hivi si mlimchukia mkamchafua kweli mpaka Mungu akakasrika akaamua kutoa adhabu ya maana mpaka saa hizi watu wanaomba po!

Acheni malalamikolalamiko ya kukufuru mwisho wa siku tutakuja kuletewa mtu ambae atataka tuwe tunalala kuanzia saa tisa hakuna kuzurula mtu nje, Mungu hua hapend malalamiko yasiyokua na tija.

Hata Kikwete mwenyewe sasa hivi atakua anatucheka kweli, tulijifanya hatutaki mbichi hizi sasa tumeletewa mbivu, na tukijifanya kuendelea kulalamika tutakuja kuletewa zilizoiva mpaka zimeoza.
 
mliomba wewe na nani? huko kolomije au CHATU CITY? au ndo nyie mnaomba bashite awe rais 2025?
cemetery.PNG
 
Mkuu wewe unacheza na kichapo cha Mungu, huyo Kikwete mnaejifanya kumsifia sasa hivi si mlimchukia mkamchafua kweli mpaka Mungu akakasrika akaamua kutoa adhabu ya maana mpaka saa hizi watu wanaomba po!

Acheni malalamikolalamiko ya kukufuru mwisho wa siku tutakuja kuletewa mtu ambae atataka tuwe tunalala kuanzia saa tisa hakuna kuzurula mtu nje, Mungu hua hapend malalamiko yasiyokua na tija.

Hata Kikwete mwenyewe sasa hivi atakua anatucheka kweli, tulijifanya hatutaki mbichi hizi sasa tumeletewa mbivu, na tukijifanya kuendelea kulalamika tutakuja kuletewa zilizoiva mpaka zimeoza.
Wasukuma wacheni kelele leteni pesa katika mzunguko c mwazimaliza nyinyi tuu
 
Sawa khursa, vipi waliwa wewe?

Nadhani lengo sio kuumizwa

Tatizo ni kuilewa dhana halisi ya nini kilikuwa kusudio na lengo la ushangiliaji

Lejea historia na nafasi ya Tanzania katika ukombozi kusini mwa Africa

Rejea historia hiyo walivo SA ....hifadhiwa Morogoro wakafanya harakati zao zote

Rejea Heshima aliyoijengea Tanzania mwalimu Nyerere nk

Nakuhakishia yeyote angetuwakilisha pale angeshangiliwa kwa nguvu zote.....jina Tanzania

Tanzania, neno hili ndio asili ya zile shangwe

Julius malema kunawakati alitusifia sana Tanzania hususani Hayati Mwl. Nyegere
 
....watu sema hawafuatiliagi mambo ya huko nje. Mugabe huyu huyu kila alipokuwa akitembelea SA wakati ule baada ya land grabbing wasauzi walikuwa wakimpa mapokezi ya kifalme kule na kumwita shujaa dhidi ya mabeberu.
 
Hivi waafrika kusini wanajua madhira wanayopata wakulima wa korosho, hivi wanajua kuwa kuna maelfu ya vijana wamemaliza vyuo vikuu lakini hawana ajira (wakiwemo afya na elimu).
Hao waafrika kusini wanajua jinsi uchumi wa nchi ulivyokufa, biashara zinafungwa, nguvu ya manunuzi imeshuka.
Waafrika kusini wanajua jinsi wapinzani wanavyonyanyaswa, uhuru wa habari unavyokiukwa.
Waafrika kusini wanajua watumishi wa umma hawajaongezwa mishahara toka mwaka 2015.
 
Waambie hata alipokua pale United Nations akitoa speech alipigiwa shangwe la kufa mtu
 
Hata viongozi wa upinzani huwa wanashangiliwa na wapenzi wao kwa kuonekana ni wakombozi... Kumbe nao....
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom