Nani anaweza kuukosoa Ubepari wa Tanzania kama ulivyokosolewa Ujamaa?


Hii adithi bwana! Huyo jirani wa Myahudi aliyefanyiwa hivyo na Myahudi ni nani? Na amini si Mpalestina.
Hapana sii hivyo mkuu wangu ni hadithi ya Utajiri na mifumo yake. Ya kwanza wakati wa Ujamaa wetu, umeona jinsi tulivvyobakia na rasilimali kibao tukashindwa hata kuzichimba wala muda wa kujifunza kuzichima tukilinda kila siku.. Haya Mabepari nao unawaona jinsi wanavyokimbizana kutafuta mananasi dunia nzima wasialikane isipokuwa kuwekeana mikwara kina Barrick, na Myahudi yeye katika Ubepari wake atakupa asilimia ndogo ya pato zima maadam hutanung'unika lakini utajiri mzima kauchukua yeye na mara zote mjanja yeye kuliko wote waliotangulia.. Hii ndio siri ya mafanikio yao.
 
Hapana sii hivyo mkuu wangu ni hadithi ya Utajiri na mifumo yake. Ya kwanza wakati wa Ujamaa wetu, umeona jinsi tulivvyobakia na rasilimali kibao tukashindwa hata kuzichimba wala muda wa kujifunza kuzichima tukilinda kila siku.. Haya Mabepari nao unawaona jinsi wanavyokimbizana kutafuta mananasi dunia nzima wasialikane isipokuwa kuwekeana mikwara\ kina Barrick na Myahudi yeye katika Ubepari wake atakupa asilimia ndogo ya pato zima maadam hutanung'unika lakini utajiri mzima kauchukua yeyey kuliko wote waliotangulia.. Na hii ndio siri ya mafanikio yao.
Katika mataifa yote duniani, lipi lina pato kubwa kwa kila mwananchi, ukizingatia pia lipi lina gap ndogo kati ya tajiri na masikini.
Israel ni taifa linalopewa msaada(kifedha) na USA kwanini umeona ni taifa la kuungwa mkono kiuchumi?
 
Wakuu blaming capitalism kwa matatizo yaliyotokea America..., nadhani ni sawa na kulaumu bunduki kwa kuua watu badala ya mpiga bunduki; to underline what am saying angalia hii extract ya Ron Paul kutoka kwenye kitabu chake cha Pillars of Prosperity...

Capitalism should not be condemned, since we haven't had capitalism. A system of capitalism presumes sound money, not fiat money manipulated by a central bank. Capitalism cherishes voluntary contracts and interest rates that are determined by savings, not credit creation by a central bank. It's not capitalism when the system is plagued with incomprehensible rules regarding mergers, acquisitions, and stock sales, along with wage controls, price controls, protectionism, corporate subsidies, international management of trade, complex and punishing corporate taxes, privileged government contracts to the military-industrial complex, and a foreign policy controlled by corporate interests and overseas investments. Add to this centralized federal mismanagement of farming, education, medicine, insurance, banking and welfare. This is not capitalism!


To condemn free-market capitalism because of anything going on today makes no sense. There is no evidence that capitalism exists today. We are deeply involved in an interventionist-planned economy that allows major benefits to accrue to the politically connected of both political spectrums. One may condemn the fraud and the urrent system, but it must be called by its proper names — Keynesian inflationism, interventionism, and corporatism.

Okay I know unaweza uka-raise the same case about Tanzania socialism (ujamaa) kwamba kilichotokea hakikuwa the intended outcome.., lakini ukweli ni kwamba on paper it was great lakini practically sababu ya tamaa na watu kubweteka ujamaa unaleta stagnatation, pili history tells us UK walijaribu wakashindwa vibaya sana hata Thatcher akaja kusweep away huo uozo, pia kwa historia ya mbongo na usimamizi wa serikali zetu kila kitu kikiwa state owned kitakufa within no time (hakuna accountability).., profit driven bring competition and quality...

Na tukiongelea kwamba Ubepari umefail USA kwanini tusiseme pia ambacho hakijafail China ni nini ? au Ujamaa ume-succeed wapi?..., Things might work well on paper lakini only time can tell and am sure everyone know what time has told us about Ujamaa na Ubepari
 
Wakuu blaming capitalism kwa matatizo yaliyotokea America..., nadhani ni sawa na kulaumu bunduki kwa kuua watu badala ya mpiga bunduki; to underline what am saying angalia hii extract ya Ron Paul kutoka kwenye kitabu chake cha Pillars of Prosperity...


Okay I know unaweza uka-raise the same case about Tanzania socialism (ujamaa) kwamba kilichotokea hakikuwa the intended outcome.., lakini ukweli ni kwamba on paper it was great lakini practically sababu ya tamaa na watu kubweteka ujamaa unaleta stagnatation, pili history tells us UK walijaribu wakashindwa vibaya sana hata Thatcher akaja kusweep away huo uozo, pia kwa historia ya mbongo na usimamizi wa serikali zetu kila kitu kikiwa state owned kitakufa within no time (hakuna accountability).., profit driven bring competition and quality...

Na tukiongelea kwamba Ubepari umefail USA kwanini tusiseme pia ambacho hakijafail China ni nini ? au Ujamaa ume-succeed wapi?..., Things might work well on paper lakini only time can tell and am sure everyone know what time has told us about Ujamaa na Ubepari
How do u categorize NORDIC countries?... to me that's how socialism should be.
 
Labda niulize hivi: Je Ubepari kama mfumo wa uchumi unaweza kukua na kuwa na mafanikio ya kweli kwa watu wengi mahali ambapo pana usawa, haki, umoja na utu? Siyo kweli kwamba ubepari ulizaliwa kutoka katika dhulma na uvunjaji wa haki (utumwa, Ukoloni, n.k) na sasa mambo ya kupigania "usawa duniani" yanakuwa kikwako kikubwa sana cha ubepari? Yawezekana kitu kinachoitwa "corporate social responsibility" ni mbinu ya ubepari kujipa sura ya ujamaa?

Mwanakijiji Ubebari ni aina ya falsafa inayofaa kwa ajili ya mahusiano ya nje siyo kwa ajili ya siasa za ndani na mahusiano ya ndani ya nchni naomba uamini hivyo na hivyo ndivyo walivyokuwa wanafanya na ndivyo wananvyofanya hadi leo wao magwiji wa Ubebari.

Wao wanavyofanya siku zote na labda nasi kama tungelikuwa makini tungeiga, ni kuwa Ubebari unafuatwa na kuwekewa vigezo pale wanapojadiliana na nchni za nje katika foreign economy, ila pale wanapo panga mambo ya ndani na jinsi ya kujenga msingi wa biashara ndani ya nchni wanafuata siasa za Ujamaa, siyo tu kama social responsibility lakini pia hizo nchni zote wameng'amua na kuweka bayana mambo makuu ambayo ndiyo misingi ya Taifa yao kiitikadi na kiuchumi na kuakikisha kuwa inalindwa na Umma kwa nguvu zote, ni kama sisi tulipobaini tokea awali baada ya uhuru na list maadui wetu wakuu na nguzo kuu za uchumi wetu ina maana kuwa serikali ilipaswa kubaki na kazi za kulinda na kuchagiza nguzo zetu kuu za uchumi na pia kusimami kwa hali na mali vita dhidi ya maadui wetu wakuu bila kuja itikadi yoyote na mkataba wowote unaofungwa na nchni yetu.


Kama tulisema Kilimo ndio uti wa mgongo wetu basi serikali ilipaswa kuweka mkazo katika kilimo na kukiboresha zaidi na zaidi na hata kuweka ruzuku ya kutosha na wataalam wakutosha bila kujali nani ni rafiki yetu, na kila sera inayotungwa Tanzania ilipaswa kuwa na uhusiano wa kuendeleza kilimo basi, na hii inawezekana kabisa. Leo hii hakuna kipaumbele nchni ambayo haina kipaumbele ambacho kinalindwa na kuheshimiwa haiwezi kusonga mbele bali inakuwa kama ngazi tu kwa mataifa mengine. Kama maaduli wetu wakuu walikuwa Ujinga, maradhi na Umaskini basi mambo yetu ya ndani yote na serikali yetu ilipaswa kusimamia hayo bila kulega na kuhakikisha elimu, afya na mitaji ya ndani inapatikani bila kuteteleka na hayo yasinge tufanya tushindwe kujadiliana na US au UK au nchni yoyote na kuwaambia sisi ni wabepari!

Last time ulikuwa unaongelea swala la UDA hapa, wao hao magwiji wa Ubepari wana amini kuwa usafirishaji wa watu kwenda makazini ni msingi imara ya kukuza uchumi na uwezo wa watu wao, hivyo katika hizo nchni zote serikali ndio inasimamia usafiri wa mijini na kuhakikisha ni ya uhakika na wanatoa ruzuku na hata pengeni wanatoa bure, unaigia ndani ya basi bure unaenda kazi. Central London Mabasi yote bure, Ujerumani train unalipia lakini hakuna anayezunguka kuakagua ticket mara moja moja kwa kushtukiza tu kila moja ina staili yake ilimradi hiyo huduma inatolewa kwa kiwango ambacho wao wanaridhika kuwa inasukuma uchumi wao. Je sisi ni kitu gani hapa ndani ya nchni kina lindwa na kusimamiwa kwa ajili ya maendeleo yetu leo!?
 
How do u categorize NORDIC countries?... to me that's how socialism should be.

Okay kwahiyo tumetoka kwenye Ujamaa (ambao unakubaliana na mimi kwamba uliacha a lot to be desired)....

Nordic countries wanafuata social democracy ambapo ingawa means of production ni private owned lakini state inatoa huduma za walfare ambazo pesa inazipata kutokana na kodi; pili advantage yao udogo wa nchi unakuwa easily managed...

Pia mkuu kumbuka kwamba kwa maliasili zetu hakuna sababu kwanini tuwe masikini hata tungefata mfumo usioeleweka kama wa Gadaffi still ingebidi tuwe tajiri; kinachofaa Tanzania ni kuhakikisha mali zetu haziibiwi na zinamnufaisha mwananchi..., nchi ingebidi itoe welfare ya nguvu as we can afford it from our natural resources...
 
Hapana sii hivyo mkuu wangu ni hadithi ya Utajiri na mifumo yake. Ya kwanza wakati wa Ujamaa wetu, umeona jinsi tulivvyobakia na rasilimali kibao tukashindwa hata kuzichimba wala muda wa kujifunza kuzichima tukilinda kila siku.. Haya Mabepari nao unawaona jinsi wanavyokimbizana kutafuta mananasi dunia nzima wasialikane isipokuwa kuwekeana mikwara kina Barrick, na Myahudi yeye katika Ubepari wake atakupa asilimia ndogo ya pato zima maadam hutanung'unika lakini utajiri mzima kauchukua yeye na mara zote mjanja yeye kuliko wote waliotangulia.. Hii ndio siri ya mafanikio yao.

Mkuu nakupata sana na nina kubaliana nawe, lakini bado tungeweza kuchimba hata kama sisi ni wa bepari au wajamaa, lengo kuu la mwalimu wakati hule ilikuwa ni vitu viwili, kwanza kuhakikisha kuwa angalau tunaweza kuchimba wakati tunauelewa na kuifaidi hiyo rasilimali na ikiwezekana labda tunge chimba wenyewe, lakini la pili ambalo watu wengi hawalijuli ilikuwa ni iwapo tungeweza kujengaka kiakili na kifikra kuwa kunaweza kuendelea na kuishi bila kutegemea madini peke yake.

Mwalimu aliamini katika historia kuwa nchni ambazo wananchni wao wamejengwa na kuamini kuishi kwa kutegemea mali asili za kurithi na kuchimba
wanakuwa wavivu kiakili na hata kutofikiria njia zingine mbadala na pengine hata uelekea katika kupigania hizo rasilimali kama hamna mpango maalum wa kuzitumia kwa maslahi ya Taifa, wakati ule wakiangalia mifano ya nchni zilizoweka turufu yao juu ya mafuta, kongo na madini na hata Angola ya wakina savimbi.
 
Wakuu blaming capitalism kwa matatizo yaliyotokea America..., nadhani ni sawa na kulaumu bunduki kwa kuua watu badala ya mpiga bunduki;

Utamlaumu vipi mpiga bunduki kama hakukuwa na bunduki in the first place. Huwezi kutenganisha hivyo viwili kwani bunduki ikikaa peke yake haiui na mtu akikaa bila bunduki anaweza kutumia kisu na madhara yakawa ni yale yale. Mfumo wa Ubepari umejengwa na watu kama bunduki zinavyojengwa na watu, however unlike bunduki ubepari unahusisha maamuzi ya watu kila siku.


kila kitu kikiwa state owned kitakufa within no time (hakuna accountability).., profit driven bring competition and quality...

Hakuna mtu anayetaka kila "kitu" kiwe state owned. Tunachouliza ni vipi viwe state owned na vipi viachiwe binafsi? Ni nchi gani ya kibepari ambayo haina 'state owned properties"? Hakuna. Zote zinazo na zinatofautiana tu kwa kina. Tumeonesha huku mapebari wanamiliki hadi mabasi ya abiria!


Na tukiongelea kwamba Ubepari umefail USA kwanini tusiseme pia ambacho hakijafail China ni nini ?

China hawafuati Ubepari kama wa Marekani. No sir. Wanachojenga China, Vietnam na sitoshangaa hata Cuba muda si mrefu ndio njia ambayo hata sisi tungeweza kuiendea. Maana tunaambia ubepari unaendana na demokrasia, well Vietnam na China zinapiga maendeleo ya haraka bila demokrasia ya vyama vingi na wanabadilishana madaraka vizuri tu (it works for them).

au Ujamaa ume-succeed wapi?..., Things might work well on paper lakini only time can tell and am sure everyone know what time has told us about Ujamaa na Ubepari

China, Vietnam n.k na ungeweza kusucceed hata Tanzania kama tungekuwa na watu ambao wangeweza kuanisha njia sahihi ya kukutanisha mifumo ya ubepari na ujamaa katika mazingira kama ya kwetu. Ubepari nao ukiangalia unaonekana vizuri kwenye paper lakini ukweli ambao tunaushuhudia sasa hivi ni kuwa probably haufanyi vizuri sana in a long run kwa sababu hauendani na masuala ya haki, usawa, na utu. Ubepari unapingana na vitu hivyo na hauwezi kusimama vitu hivi vikisimama. Ujamaa on the other hand unaendana na vitu hivyo vitatu.
 
Ukomunist ulishindwa ulishindwa kwa sababu inherently unaviza nafsi ya mtu, unamfanya mtu awe treated kama mashine bila kuona matunda halisi na mafanikio ya kazi yake. State ndo inachukua mafanikio ya mtu binafsi. Mungu alituumba akatuwekea uwezo wa kuji-express, kwa hiyo mtu anaponyang'anywa huo uwezo anakuwa amefungwa kutumia uwezo wake to the fullest. Communism was likely to fail by all means.

Ubepari, tofauti na ukomunist, unatoa hiyo fulsa kwa kiwango kikubwa. Tatizo la ubepari ambao umejengwa kwenye msingi wa ubinafsi (km ulivyosema) ni huo ubinafsi wenyewe. Watu wanakuwa wabinafsi kiasi kwamba wanachojali ni kutengeneza pesa tu. Watu wanakuwa tayari kuvunja maadili yoyote ya utu ili watengeneze pesa. Anguko la uchumi wa USA ambalo liliasisiwa Wall Street, ni huo ubinafsi na uroho wa kutengeneza pesa.
Na hao wanaodai serikali ijitoe kwenye kila kitu nadhani wanataka ku-create chaos tu.

Mawazo yangu: A branded system works better than both communism and capitalism. Angalia Scandnavian countries, mostly zina karibu kila kitu bora kuliko hata hao magwiji wa ubepari. Afya bora, elimu bora, maisha bora, wananchi ni happier, uchumi hauyumbi kama mabepari etc.

Kuhusu Tanzania: Kama ujamaa ulikuwa haujajaribiwa, basi na ubepari haujajaribiwa; kilichopo sasa hivi ni ANARCHY ya kiuchumi.

 
Hujaona Upebari wa Tanzania
1. hakuna uhuru wa mwananchi
2. vyombo vyingi vinanguvu zaidi ya wananchi angalia Bakwata
3. Wenye Pesa ndio watakoongonza nchi hii kama una itiakadi pekee haupiti hata kwenye vikao vya shina
4. unafiki na upendeleo umezidi, Angalia hakuna haki ya mnyonge angalau wakati wa Ujamaa alikuwa na Ardhi sasa hivi Ardhi iko kwa Mabosile
 
Wakati wa kuvunjika kwa nchi za kijamaa ni ujamaa uliolaumiwa kwa matatizo ya kiuchumi ya nchi hizo. Wasomi wa Kimagharibi na wale wa nchi za kijamaa wenye mrengo wa kimagharibi walibebesha lawama mfumo wa ujamaa kuwa "umeshindwa" kuleta matumaini kwa wake. Ujamaa ulikosolewa kama ni mfumo wa njozi "utopia" wenyewe walisema. Nyerere aliwahi hata kuulizwa ni kwa namna gani "ujamaa ulishindwa" na yeye alijibu kuwa "utashindwa vipi wakati haujajalibiwa"?

Mwanakijji.......good analysis. Makuunga mkono katika tathmini hii. Naamini unachoamini.
 
Soby,
Mkuu wangu nilichoongelea mimi ni Ubepari mktk ngazi ya watu maana ukienda kitaifa ni mapana ya ubepari lakini maudhui yake hayatofautiani na yale ya watu binafsi. Israel kama Taifa wana mchanganyiko wa yote kwa sababu yapo mengi ya kijamaa na yale ya Kibepari nadhani swala kubwa tunalozungumzia ni Ubepari ktk hali ambayo serikali haimiliki njia za kuzalisha uchumi. Kwa hiyo tunapozungumzia Ujamaa tutazame njia za kuzalisha uchumi kuwa mikononi mwa serikali au Ubepari ambao njia hizi huwa mikononi mwa wananchi, na lengo na kuu la itikadi hizi ni kuhakikisha mavuno bora ambayo kila mwananchi anafaidika, hilo kwanza.

Halafu, wana falsafa wamekaa na kuunda msingi ya kuwezesha njia hizi zipate kufanikiwa na hapo ndipo tunakuta kutokubaliana ktk uundwaji wa sera na vipaumbele kiasi kwamba within Ujamaa utakuta makundi na within Ubepari utayakuta makundi yakitofautiana ktk utunzi wa policies..Leo hii tunaolaumu Ujamaa wa Nyerere sii kwa sababu ya nia la lengo la Ujamaa, isipokuwa sera zake kufikia malengo hazikuweza kushabihiana na watu na mazingira tulokuwepo hivyo failure ilikuwa matokeo ya kile tulichokipanda.

Na ukija ktk Ubepari unakuta pia tofauti za kisera ktk uzalishaji na sii who owns it, hivyo kukuta sera zinazopingana wakiwa lengo moja la kuboresha maisha ya wananchi.. hapa ndipo tunakuta bureaucratic politics za where you sit is where you belong ( vyama na Upinzani).. lakini pamoja na yote hayo kikubwa ni kwamba none of us can predict the outcome and bet on it! - hakuna, isipokuwa tunatumia akili zetu kutazama uwezekano mkubwa upo wapi sii tu ktk kupata ushirikiano ktk uzalshaji bali hata ktk kupata mavuno bora ambayo yatawafikia wananchi wote na kuboresha maisha yao.

Binafsi, huamini kwamba itikadi ni elimu ya kuelewa mazingira uliyopo na kutafuta njia mbadala zinazowawezesha wananchi kufanikiwa zaidi kimaisha ktk ulimwengu wao wa biashara..Yapo maswala yanayotakiwa kufuata Ujamaa na yapo yanayotakiwa kuwa ya Kibepari maadam tutazingatia mila na desturi za wahusika zinalingana na mazingira waliyopo. Ni kusema kwamba ktk mifumo yote ya kiitikadi huwezi kupanda mahindi wakati wa masika! au kupanda juu ya magugu ukategemea kuvuna pia hata ukapanda wakati muafaka lakini mvua zikanyesha wakati miche ya mahindi inaota maua na ikaharibika haiwezi kuwa matokeo ya kimfumo, iwe Ujamaa au Ubepari hatuwezi kupima mafanikio ya mfumo au failure ya mfumo isipokuwa sera zilizowekwa kukabiliana na matukio kama hayo na ktk mazingira gani.

Sababu kubwa ya kuweka mifano hiyo hapo juu ilikuwa uonyesha kwamba tunaweza sana kufanikiwa iwe ktk Ujamaa au Ubepari ikiwa sisi binadamu tutaweza kuondokana na ignorance, greed na selfishness lakini kwa vile ni moja ya mapungufu ya kibinadamu, wasomi wengi duniani wameumiza vichwa wameshindwa kabisa kupata mfumo mbadala kupambana na hisia hizi za kibinadamu. Na kama umenisoma vizuri hapo juu utakuta ya kwamba kila mrengo, mfumo na sera zinazojengwa huwa zimegubikwa na wingu kubwa la kuelewa kwa undani hisia za kibinadamu. Na hata sayansi haiwezi kutupatia ufumbuzi ktk hisia hizi.. hivyo matokeo ya kuanguka kwa uchumi mimi naamini kabisa hautokani na mifumo isipokuwa udhaifu wa binadamu..

Ya firauni ndiyo haya...kama utapata muda soma vitabu vya Ujamaa utaona wakilaani Ubepari ni ktk misingi iliyojaa ignorance, greed and selfish hali Mabepari nao waliona Ujamaa umejaa Wajinga, wabinafsi na walafi!..wote wananyoosheana vidole kwa makosa sawa kabisa! - Pia labda tutazame mifano yetu nyumbani sisi maskini huwaona matajiri Wabinafsi, walafi na wajinga wakati matajiri nao huwaona masikini vivyo hivyo. Hivyo we all carry Ujinga, Ulafi na Ubinafsi na sielewi nafuu imesimama wapi isipokuwa nachoweza kusema ni kwamba nia zetu sote ktk mirengo yote ni safi kabisa isipokuwa ni njia (sera) zipi hasa zinaweza ku deliver fruits na kile tunachopanda ndio ngoma mpyaaaa!. Tutaweza vipi kujenga policies ambazo zitazingatia zaidi mapungufu haya ya kihisia badala ya kuunda policies zinazosukumwa na societal pressure. Ufisadi ni ktk mapungufu hayo niliyozungumzia hapo juu na hakika unatufilisi iwe ktk Ujamaa au Ubepari.
 
Je ubepari wa Tanzania msingi wake ni uzalishaji, innovation, intellectual properties, technology, property rights?
 
Je ubepari wa Tanzania msingi wake ni uzalishaji, innovation, intellectual properties, technology, property rights?
Mkuu wangu we are users end! sisi ni watumiaji tu hivyo Ubepari kwetu ni uwezo wa kuagiza mali kutoka nchi na sii uzalshaji.. Mfano mdogo tu, yamejengwa mahotel mengi ya kitalii sii na wananchi wazawa bali ya mageni ambao booking na sales (malipo) yanafanyika nje online.. Unategemea Ubepari huo utaweza kutunufaisha sisi kwa lipi kwenda kujirusha?
 
Are there intellectuals in Tanzania (I didn't say graduates!) ambao wanaweza kuangalia mfumo wetu wa kiuchumi na kutuelezea ni ubepari wa namna gani huu?
 
Utamlaumu vipi mpiga bunduki kama hakukuwa na bunduki in the first place. Huwezi kutenganisha hivyo viwili kwani bunduki ikikaa peke yake haiui na mtu akikaa bila bunduki anaweza kutumia kisu na madhara yakawa ni yale yale. Mfumo wa Ubepari umejengwa na watu kama bunduki zinavyojengwa na watu, however unlike bunduki ubepari unahusisha maamuzi ya watu kila siku.

Mkuu huwezi kulaumu bunduki ni sawa na kumpa mtu kutumia jembe kupigia misumari na nyundo kulimia alafu akalaumu hivi vitu havifanyi kazi.., kama bunduki ingetumika kwa kazi yake ya kuulia wanyama mwitu na kujilinda kusingekuwa na matatizo...; what am saying ni kwamba the mess which occured has nothing to do na ubepari unavyofanya kazi bali ni wizi na utapeli wa watu kutaka kunufaika, hedge funds corporations gambling with people's money (watu wanakopesha watu ambao wanajua kabisa kwamba hawawezi kulipa ) na tatizo halikuanzia marekani, bali '97 lilianzia Asia (Indonesia, Thailand, Korea and Malaysia) baada ya nchi na watu kukopa pesa ambazo hawawezi kuzilipa na kutumia pesa ambazo hazipo na kama unavyojua hii sasa ni global village tatizo lika-spread. (America walivyo-wabail out ikaleta a wrong message kwamba sisi tukifanya makosa government will bail us out.

Sasa swali linakuja is that Capitalism according to Friedrich von Hayek..., kwamba let the markets take care of itself bila intervention au ni keynes way kwamba state should intervene to correct the market.., na tumeona baada ya Marekani na England kufata Keynes way after the war ilikuwa ni short term cure ambayo haikuzuia inflation...; Kwahiyo has Hayek way failed (ambayo ni common sence kwamba spend what you have and no giveaways) na kila politician knows this ila tatizo la kuacha kusaidia watu kwenye shida inafanya hii issue hard to implement (ni kama wewe kwenye nyumba yako ukitumia pesa ambayo hauna nadhani mwisho wake unaujua..)

Hakuna mtu anayetaka kila "kitu" kiwe state owned. Tunachouliza ni vipi viwe state owned na vipi viachiwe binafsi? Ni nchi gani ya kibepari ambayo haina 'state owned properties"? Hakuna. Zote zinazo na zinatofautiana tu kwa kina. Tumeonesha huku mapebari wanamiliki hadi mabasi ya abiria!

We saw what happened tulipotaifisha mabasi yote after Uhuru (no accountability no nothing and things failed) hapa ni kuacha masoko yajiendeshe vizuri hata state haikatazwi kuanzisha biashara zake lakini let them compete with private entities if they can...!!; kwahiyo ubepari does not mean kwamba give away everything owned by the state to people lakini make sure kwamba vitu vina-run profitably, tatizo la state owned things vitu vinakuwa vinaendeshwa as a service na sio biashara bail out left, right and centre..., (lakini kama sisi ambao tuna natural resources, kama we can afford to give services and bail out unsucessful companies..) basi hakuna neno ila issue ya kwenda kukopa ili kufanya kampuni iendelee kufanya kazi kwa miaka mingine miwili zaidi nadhani unajua the outcomes...;

Alternative way ni kuacha private companies nyingi zitoe huduma na kufanya biashara, wapige kodi za nguvu hizo private corporations na pesa inayopatikana toa services kwa wananchi... (elimu; usafiri; afya n.k.) lakini kumbuka the money has to come from somewhere..

China hawafuati Ubepari kama wa Marekani. No sir. Wanachojenga China, Vietnam na sitoshangaa hata Cuba muda si mrefu ndio njia ambayo hata sisi tungeweza kuiendea. Maana tunaambia ubepari unaendana na demokrasia, well Vietnam na China zinapiga maendeleo ya haraka bila demokrasia ya vyama vingi na wanabadilishana madaraka vizuri tu (it works for them).

Sijasema China wanafuata Ubepari kama wa Marekani.. lakini swali wanafuata nini? (kuna wengine wanaita Capitalism with Chiniese Characteristics.) Alafu what is American Capitalism..? Is it Keynes (Government Intervation..) ? au Hayek Open Markets and No Government Intervation
(No Bailouts) au is it total mess ambayo its just greedy, people wants handouts, work less wants over the roof payments (where is the money going to come from hata kama wanafuata ujamaa..??).

Asia is taking over no matter what they are following sababu essentially ya cheap labour which causes cheaper products which competes more easily. What happened in Economic Crisis did not make any economical au any sense at all it was chaos na wengi waliona hilo tatizo kwamba soon or later litatokea lakini everyone was busy making a quick buck (at everyones expense but themselves)

China, Vietnam n.k na ungeweza kusucceed hata Tanzania kama tungekuwa na watu ambao wangeweza kuanisha njia sahihi ya kukutanisha mifumo ya ubepari na ujamaa katika mazingira kama ya kwetu. Ubepari nao ukiangalia unaonekana vizuri kwenye paper lakini ukweli ambao tunaushuhudia sasa hivi ni kuwa probably haufanyi vizuri sana in a long run kwa sababu hauendani na masuala ya haki, usawa, na utu. Ubepari unapingana na vitu hivyo na hauwezi kusimama vitu hivi vikisimama. Ujamaa on the other hand unaendana na vitu hivyo vitatu.

Mkuu Usawa (this can only happen theoretically) hakuna usawa na ukilazimisha hili kunakuwa na stagnation mtu anaona kwanini mimi nihangaike sana for the benefit ya kila mtu..., and what is haki (you eat what your earn, "utakula jasho lako..." au) Mkuu nchi ikiwa profitable unaweza ukawalima kodi wenye nazo kwa manufaa ya wasionazo, tunaweza tukawa na kampuni moja tu.., ikalima kwa mitambo ya kisasa na ikalisha east africa nzima.., Hayek Capitalism has not failed sababu haijawa implemented na haiwezi ikawa implemented sababu ya politicians wanaogopa kuchukua hard decisions.. (No Money No Spending..., Ni kubana mikanda tu, Pesa kama ipo basi itumie.)


Na ndio maana nikasema kuanzia mwanzo Tanzania hatujafail sababu tunatumia Ubepari au Ujamaa sababu ni kwamba its total chaos na hakuna accoutability at all ni bora liende... Hivi unajua maliasili za kanda ya ziwa tu zingeweza kulisha Tanzania nzima, na kutoka elimu na afya ya bure (kama zingekuwa well managed..?); na hili la kuomba misaada nje, kutumia pesa ambazo hatuna na kugawa maliasili zetu what is it.. (Ujamaa, Ubepari au Ujinga...?) We are just labelling Ujinga tunaofanya na lack of common sense giving it different names lakini in short what is happening is called Ujinga....

Conclusively ni kwamba Tanzania tunaweza kufanikiwa na kila mtu kuishi maisha mazuri whatever mfumo wa uchumi tutakaotumia sababu tuna mtaji wa kutosha..; tunachotakiwa kuwa nacho ni usimamizi mzuri wa mali zetu (state lazima isimamie) na kuacha mambo ya biashara yashindane yenyewe bila intervation.., kodi ikusanywe kwa faida ya mwananchi Social Democracy
 


Last time ulikuwa unaongelea swala la UDA hapa, wao hao magwiji wa Ubepari wana amini kuwa usafirishaji wa watu kwenda makazini ni msingi imara ya kukuza uchumi na uwezo wa watu wao, hivyo katika hizo nchni zote serikali ndio inasimamia usafiri wa mijini na kuhakikisha ni ya uhakika na wanatoa ruzuku na hata pengeni wanatoa bure, unaigia ndani ya basi bure unaenda kazi.

Mkuu hio ndio kazi ya government ni governing; na mara nyingi ikiingia kwenye biashara huo inaanguka kifo cha mende sababu ya lack of accountability na pesa ipo nyingi ya kuchota.., na kutoa ruzuku sio kwamba ni bure its through kodi za watu ndio they can afford alafu pia watu wanalipia although its cheap through day savers weekly and monthly wazee ndio bure na wanafunzi ni bei rahisi na hakuna mtu anaesema state hairuhiwi kuwa na magari inaweza pia ikawa na usafiri ambao ukacompete na watu binafsi mfano Birminghan UK kuna magari ya council (manispaa) centro buses (ambayo ni mabaya na chakavu) alafu kuna privately owned (TWM - Travel West Midlands) ambayo ni mazuri yana quality na ni efficient serikali inatoa ruzuku hizi basi ziende routes ambazo hazina faida pia mabasi haya yana stream nyingine ya income ambayo ni matangazo

Central London Mabasi yote bure, Ujerumani train unalipia lakini hakuna anayezunguka kuakagua ticket mara moja moja kwa kushtukiza tu kila moja ina staili yake ilimradi hiyo huduma inatolewa kwa kiwango ambacho wao wanaridhika kuwa inasukuma uchumi wao. Je sisi ni kitu gani hapa ndani ya nchni kina lindwa na kusimamiwa kwa ajili ya maendeleo yetu leo!?
Pia mabasi sio bure bali ni affordable na efficient na kutokukagua ticket ni culture ya wenzetu sio matapeli sana huku bongo ukifanya hivyo hakuna mtu atalipa (wizi umejaa..) na huduma inayotolewa its funded by taxes ambayo inapatikana pia from private entities, pia hata train UK kuna za state nadhani Centro / Metro etc (ambazo nadhani state ina hisa lakini sina uhakika..) lakini kuna private owned Virgin Trains ya Richard Bransom ambayo ni way better..., lakini zote zinacompete kwa faida ya raia
 
Mfumo wa kibepari umesababisha Tanzania ya sasa kuwa tegemezi kuliko kipindi cha Mwalimu, matatizo yanaonekana lakini kwakuwa ubepari ni part and parcel na ubinafsi (hence ubinafsishaji) kila mtu anajali nafsi yake, viongozi wanataka kuwa wafanyabiashara pia, na wafanyabiashara wanataka kuwa viongozi pia n.k., kwa kifupi siku hizi maslahi ya taifa yanawekwa nyuma!

Btw: Kinachotokea Tanzania ni rasharasha tu, sote twajua kuwa mfumo wa kibepari unazidi kupagaranyika kila kukicha; snowballing of USA debt, EU tayari imeshakuwa kimeo. Wakati huo huo IMF wameshatoa ripoti kuwa ikifika ikifika 2015 China itaipita USA kuwa the biggest economy, tunaona pia a re-surging economic Bear (Russia) and the BRICS n.k.. Kwani haya yote ni mazingaombwe????

Stats zinaonesha kuwa'Das Kapital' ya Karl Marx imekuwa best seller (kwanini?)....labda kuna siku akina Mkulo watajikumbusha kuperuzi!
 
Mkuu what caused the current economic disaster as well as the problems which started in late 2000...? Je ni Ubepari au ni gambles and greediness za mabenki as well as hedge funds corporations kutoa mikopo kwa watu ambao hawawezi kulipa as well as watu na nchi kutegemea bail-outs pale wanaposhindwa kulipa...?

Kilichotokea hakina uhusiano na ujamaa wala ubepari ni tamaa and lack of common sense..; whats needed is an hybrid of a system depending na situation ya nchi yenyewe (tumeshaona jinsi state ambavyo haiwezi kusimamia mali kutokana na kukosa uchungu...) kwahiyo corporations and private sectors wapo better suited with a state putting checks and balances kuona kwamba hakuna abuse yoyote..

Kwahiyo mkuu naungana mkono na wewe kwamba kila nchi inahitaji mfumo unaochukua mazuri yote (hybrid ) kulingana na nchi yenyewe mfano China.. (Capitalism with Chiniese Characteristics..) therefore we need whats works better for Tanzania lakini lets not take the current economic problems with sweeping comments kwamba Ubepari ume-fail... Lakini (History has taught us kwamba human greediness na umimi has made Ujamaa hard to be implemented).

After all we have got all the raw materials and natural resources maybe all we need is to make sure kwamba kabla huu mtaji haujaisha tuwe tumeutumia vema kupata infrasture za kutosha mpaka enterior ili mimi ambae nipo mjini sasa hivi niweze kunywa maziwa yaliyokamuliwa asubuhi na bibi aliyopo nyuma ya mlima kule Mtwara (win win situation...) ; we are at a foundation level which we need to go back to the basics and what has worked or not worked in Cuba does not necessarily mean wont work here...

Transparency na usimamizi wa maana ndicho kinachotakiwa hapa Tanzania...; whatever you might call it ujima; ubepari, ujamaa au Tanzania ubeujamaa

Mkuuu nimependa sana hoja yako umeiweka wazi tuuuu tena kwenye part ya Umimi na Urafifi uliopindukia kupita kiasi. Pamoja na kusema kila nchi ingeweza fuata mfumu wake na kujiletea maendeleo, Yet unakubaliana nami kuwa Tanzania tulikimbia sana in terms of Umimi na urafi kwani Ujamaaa ulikuwa yet unatufaaa kabisa pamoja hata kama mwalimu JK Nyerere alikuwa na mapungufu yake yet we where in the right track.

Na ndio hawa hawa viongozi walio kaata Azimio la Arusha na kuja na style yao so called ubepari yet Mwl.Nyerere alikuwa anaupinga esp Ubinafsishaji a.k.a Soko huria Mwl aliwapa mifano mingi sana ya kufanya ila walipuuzia tu eg alilia sana na viwanda vyetu viboreshwe vifufuliwe tungesonga mbele lakini tulijionyesha tu wachanga sana wakuto jua kuviendesha na uwezo wa kuviendesha tulikuwa nao ni tulijidekeza sana na ndio mpaka sasa twaendelea na hali hii.

Ubepari kwangu mie yet haunipi picha halisi ya kimaendeleo ni kuwa unajenga umimi sana na urafi uroho na ndio chanzo cha kuweka gap kubwa kwa walio nacho na wasio nacho


 
Duniani tunatanguliwa na mambo matatu makubwa sana..IGNORAMCE, GREED na SELFISHNESS haya unaweza kuayweka sehemu yoyote ya itikadi na elimu za falsafa bado yakatoka washindi..
Kushindwa kwa Ujamaa kulitokana na haya ingawa misingi ya Ujamaa ilikuwa kupiga vita maswala haya haya. Kwa mfano unapokataa kuagiza mali za wengine ukataka kuuza zako inaweza kabisa kutokana na ignorance, greed na selfishness..

Kuna Myahudi mmoja alinipa hadithi fupi ya mafanikio yao na akasema ya kwamba chukulia umekwenda shamba umekuta mananasi 12 yaliyoiva, kwa mjamaa atasema mananasi yote ni yake na hatataka mtu asiyehusika achukue hata moja! mwisho wa siku atabakia nayo ashindwe hata kuokoa moja kwa sababu atatumia muda na kazi kubwa kuyalinda bila kupoteza hata moja huku akifikiria jinsi ya kuyabeba yote (Huonekana - ignorant, greed and selfish). (kina Nyerere)

Bepari atajaribu kuakota kadri ya uwezo wake kabla mtu mwingne hajatokea lakini uwezo wake ni kuchukua mananasi manne tu hivyo atachukua hayo na kuondoka akafiche au kuyapelekea nyumbani kwake akirudi hukuta mengine manane yameisha chukuliwa (huonekana pia- ignorance, greed and selfish)

Myahudi on the other hand, wakikuta mananasi kumi atabeba manne kisha atawaita jirani kumsaidia kubeba yaliyobakia halafu wakifuka kwake atawapa kila mmoja wao nanasi moja, akabakiwa na mananasi 10...(again huonekana ignorant, greed na selfish) - Mshindi nani?


Mkuu naona umemaliza kila kitu. Ukweli ni kwamba hata tulifanya nini hata tukichagua chama gani kama kuna matatizo ya msingi ambayo tutayaacha tutakuwa tunapiga mark time. Ukiangalia Zambia ukweli ni kwamba MMD imeleta mabadiliko makubwa, lakini kulikuwa na element ya Nationalism kwenye uchaguzi huo, bila element hiyo inawezekana kuwa MMD wangebaki, na tunatakiwa kukumbuka kuwa kwenye chaguzi zetu nyingi hapa Afrika, si wengi wanachagua wagombea kutokana na issues zilizopo au kutokana na ajenda zao, bali wanachagua kutokana na kabila, au wanachagua kutokana na kudanganywa.

Kwa mfano hapa Tanzania ukiangalia manifesto ya CCM waliyoitumia kuomba ridhaa ya kutawala unaweza kuona ni nzuri sana, lakini manifesto inayotekelezwa ni opposite kabisa na manifesto waliyoombea uongozi. Kikwete alisema maisha bora kwa kila mtanzania, angalia kama ni kweli. Kwa kuwa wengi ni wanyonge(wajinga kama alivyosema Baregu) wanaamini wanachoambiwa kuliko wanachokiona na kuwachagua wanaotekeleza manifesto walizonazo akili mwao yote unaaona ayanacheza kwenye hayo IGNORANCE, GREED na SELFISHNESS. Kama unafuata ubepari na ukaongozwa na Greed matokeo yake ni kuwa na system ambayo ina ukomo, yaani kama tunavyoona sasa financial crisis kwenye ubepari.

Hakuna mtu anayeweza kuulamumu ubepari moja kwa moja, lakini tunaweza kulamu baadhi ya tabia za binadamu zinazoweza kuharibu system yoyote.
 
Back
Top Bottom