Nani anawatetea watoto wakiwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani anawatetea watoto wakiwa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Fundi Mchundo, Feb 25, 2008.

 1. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #1
  Feb 25, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Najua wengi mmeisoma hii habari. Hivi kweli vitendo hivi vinaweza kuendelea kufanyika with impunity? Hao mawakili wetu mashujaa kwa nini wasiichukue kesi hii pro bono na kumgeuza huyu Suzan kuwa Rosa Parks wa haki za watoto wakiwa? Hivi hakuna sheria inayolinda haki zao na kumsimamia msimamizi wa mirathi ili asiwadhulumu watoto wa marehemu? Watu kama hawa wanatakiwa watolewe mfano ili wengine wote wenye uchu wa fisi wa namna yake waogope kufanya hivyo. Hatuwezi kama jamii kukaa na kutingisha kichwa tuu wakati unyama kama huu unatendeka. Ni wajibu wetu kudai kuwa hawa waliokuwa wanyonge (watoto yatima, wajane, wazee, wenye ulemavu n.k.) walindwe na sheria.
   
 2. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #2
  Feb 25, 2008
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Mchundo
  Hata mimi nimeisoma..good that you have brought it up!

  Mimi personally yalishapata kunifika kufiwa na dada na shemeji in 1990s na waliacha watoto wawili wadogo- basi kwa vile mila zinasema Mdogo wa Kiume Marehemu awe Msimamizi wa mali za Marehemu.. basi tukashughulika kweli tukafanikiwa kupata kama laki 8 pesa ya mirathi ilyokuwa ktk Account ya Marehemu dada kwa cheque ambayo iliandikwa kwa huyu shemeji ili kulipia malipo ya shule ya hawa watoto!

  Hutaamini.. shemeji yule alipotea na zile pesa na watoto wa dada tumewachukuwa na kuwasomesha hadi sasa! Naskia alijapatikana miezi mitatu akioomba msamaha kwa wazazi..sema hatukuwa na mda wa kumpeleka mahakamani kwa yule hakimu aliyesimamia mirathi!

  Haya mambo ya aibu ktk nchi na taratibu za sheria zetu. Mimi nashauri mzazi akifariki mali ipigwe mnada iweke ktk Account ya Elimu Watoto kama CRDB .. na hakimu ndo awe signatory kulipia shule za watoto wa marehemu! Hili swala kuwaachia ndugu wenye njaa naona ni usumbufu mtupu wakati mwingine baadae!

  Mimi sii Mwanasheria..ila mtu wa sheria aweza kutoa mwanga zaidi

  Mzalendohalisi
   
 3. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #3
  Feb 25, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145

  Pole sana kwa yaliyowakuta. Mimi naona imefika wakati social workers wetu waanze kuwajibika. Msimamizi wa mirathi awajibike kutoa ripoti kwao kila mwaka hadi hapo watoto wanapofikia umri wa kujitegemea. Nakala ya ripoti hii na ile ya ufuatiliaji wa hao social workers ikabidhiwe kwa mahakama iliyohusika katika kuamua mirathi. Msimamizi atakapoonekana anakwenda kinyume cha mahitaji na manufaa ya wafiwa, hawa social workers watoe taarifa katika vyombo husika na hatua za kisheria zichukuliwe ambazo hazitaishia kwenye kumnyang'anya usimamizi. Pale social worker atakapoonekana ku'collude' na msimamizi wa mirathi na yeye achukuliwe hatua za kisheria. Watoto wafiwa wachague mtu ambae wanaoona ataweza kuwatendea haki zaidi ya huyu msimamizi wa mirathi. Huyu nae ataweza kushitaki kwa social worker au mahakama kama ataona kuna tatizo lolote. Najua hii inaweza kufanyika katika sehemu chache nchini mwetu lakini ni lazima tuanze mahali.
   
 4. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #4
  Mar 3, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145

  Kutoka the Guardian.
  Naona kuna watu wamesikia. Ningependekeza huyu binti afanywe mfano katika siku ya wanawake jumamosi. Hao wakina Kato wasingoje waletewe Suzan, wamfuatilie. Kama nilivyopendekeza, awe Rosa Park wa hii ishu na wao wawe wakina Thurgood Marshall. Hi lazima watu kama hawa wakina Magina washikishwe adabu irrespective ya kuwa wazazi waliacha will au la! Tusiishie kutoa machozi ya mamba, tufanye kweli.
  Aluta Continua!
   
Loading...