October man
JF-Expert Member
- Nov 23, 2017
- 3,635
- 4,997
Huu uzi unanuka umasikini.Unaweza kuwa na pesa alafu ukawa na kisukari au shinikizo la damu, vyakula vizuri kama burger, keki, pizza utakula kwa macho.
Viatu vikali utashindwa kuvaa ukiogopa kuchubuka na kupata vidonda mguu ukatwe,utashinda na yebo yebo kutwa nzima mpaka ofisini.
Ukiumwa na chochote Malaria, Ukimwi nk mate yanakuwa machungu, hamu ya kula inapotea hata biriani utaliona chungu.
Ukiendekeza kubana na kutafuta hela ukajisahau utaishia kupata vidonda vya tumbo.
Ishu hapa sio kutokula, tatizo ni kula ili mradi umekula siku ipite au kutokula kabisa usave hela utajirike.
Chanzo cha magonjwa mengi kama kisukari na shinikizo la damu ni kuishi maisha yasio na mpangilio katika ulaji, unakula ili mradi umekula unathamini pesa kuliko afya.
Kwa maisha hayo, matokeo yake wengi wetu hujikuta tumeshapata magonjwa hayo wakati pesa ndio zimeingia, unaishia kusikitika huwezi kuzitumia.
Linda afya yako kwenye harakati zako za kutafuta pesa. Afya ndio kila kitu.