Nani anatoka Marekani kuja kutibiwa Tanzania?

Juzi wakati Rais Samia alipotembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete [siyo ule moyo wa Kikwete uliopo ndani ya kidari chake], alisema kuwa alifarijika kusikia kwamba miongoni mwa wagonjwa wanaoenda hapo kutibiwa, wanatoka nchi za jirani na hata Marekani.

Hapo kwenye Marekani alisema kwa mshangao na msisitizo.

Haya hapa kwenye video maneno aliyoyasema. Anzia dakika ya 12:49 hadi 13:10.

Isije wakawa wamemlisha matango pori huyo mama!

Nani atoke Marekani aje Tanzania kutibiwa ugonjwa wa moyo?

Labda ni awe au wawe Wamarekani ambao tayari walikuwepo Tanzania [kwa sababu yoyote ile] halafu wakapatwa na matatizo ya moyo ndo wakapelekwa hapo kupata matibabu.

Ila mtu atoke Marekani na matatizo yake ya moyo aje Tanzania kwa ajili ya kupata matibabu hapo kwenye hiyo taasisi?

Ngumu kuamini….
Ngoja tuwasubiri nyie diaspora labda mtakua wa kwanza
 
Na kiumbe ambae anatoka marekani akaja tibiwa tanzania anakuwa ana matatizo ya akili. Tanzania hii ninayoijua unapeleka mgonjwa unaambiwa dr ambae atamshughulikia mgongwa wako hayupo tusubiri aje?

Bora enzi za JPM nidhamu ya kazi ilikuwepo ma dr muda wote wako kazini, hata mgonjwa akizidiwa dr anakuwepo sio zama hizi ma dr lazima wapigiwe simu.

Juzi mtoto wa wifi yangu alimeza mbegu ya tunda fulani (silijui kwa kiswahili) hilo tunda ni tamu kwa juu ukila utamu ukaisha ndani kunabaki kama ile mbegu ya mparachichi sasa hiyo ndo aliimeza kwa sababu lina ukubwa kama ya yai dogo hakuweza kuimeza ikabana juu kama puani hivi. Mtoto ana 1.3yrs

Mtoto kimbiza dispensary wakasema hawamuwezi, kimbiza hospital nyingine huko ndo walikutana na vituko. Huyo sijui ni ness sijui dr ni mmama wala hakumgusa mtoto. Anauliza kameza nini? Wakataja hilo tunda kwa kiluga chetu wala hakujali alibaki amekaa anauliza hilo ni tunda gani? hakuwaambia chochote.

Mtoto ashavimba pua uso damu zinatoka wakampeleka hospital nyingine ma dr chap wakaanza kazi baada ya muda akapiga chafya kikatoka.

Ati kwa upuuzi kama huu mtu anatoka marekani aje tibiwa tz? Kweli hii dunia ina mambo mengi.
Yaani wewe na wifi yako muache.kuwa busy na simu muwe mnaangalia watoto.
 
Juzi wakati Rais Samia alipotembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete [siyo ule moyo wa Kikwete uliopo ndani ya kidari chake], alisema kuwa alifarijika kusikia kwamba miongoni mwa wagonjwa wanaoenda hapo kutibiwa, wanatoka nchi za jirani na hata Marekani.

Hapo kwenye Marekani alisema kwa mshangao na msisitizo.

Haya hapa kwenye video maneno aliyoyasema. Anzia dakika ya 12:49 hadi 13:10.

Isije wakawa wamemlisha matango pori huyo mama!

Nani atoke Marekani aje Tanzania kutibiwa ugonjwa wa moyo?

Labda ni awe au wawe Wamarekani ambao tayari walikuwepo Tanzania [kwa sababu yoyote ile] halafu wakapatwa na matatizo ya moyo ndo wakapelekwa hapo kupata matibabu.

Ila mtu atoke Marekani na matatizo yake ya moyo aje Tanzania kwa ajili ya kupata matibabu hapo kwenye hiyo taasisi?

Ngumu kuamini….
Mkuu wewe ni CCM Baby,tena Team Magufuli Baby,na slogan yenu ni Tanzania kuwa Dana kantre,si ajabu Tanzania imetajirika kushinda US

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
 
Yaani mbeba maboksi [kama mimi ] ambaye hana insurance [mimi sina health insurance ], na ana matatizo ya moyo, anarudi bongo kuja kupata matibabu hapo kwenye taasisi ya Kikwete?

Bongo huhitaji insurance kupata matibabu? Au ni bei rahisi kupata matibabu hata kama huna insurance?
Tanzania ni Tajiri kuliko US, "in Mataga's voice"......

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
 
Tunaweza kushangaa lakini pengine wapo.... Mkuu wa hii taasisi amehudumu miaka mingi US na mpaka sasa ni visiting lecturer vyuo kadhaa huko US. Inawezekana mtu aliyeshindwa gharama akaona kuliko kufia USA acha nikajaribu bahati huko Africa. Na kama alipata msaada, anakuwa balozi. Anyways, Rais anajua mengi kuliko wengine hapa
 
Back
Top Bottom