Nani anatoka Marekani kuja kutibiwa Tanzania?

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
89,734
2,000
Juzi wakati Rais Samia alipotembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete [siyo ule moyo wa Kikwete 🤣 uliopo ndani ya kidari chake], alisema kuwa alifarijika kusikia kwamba miongoni mwa wagonjwa wanaoenda hapo kutibiwa, wanatoka nchi za jirani na hata Marekani.

Hapo kwenye Marekani alisema kwa mshangao na msisitizo.

Haya hapa kwenye video maneno aliyoyasema. Anzia dakika ya 12:49 hadi 13:10.


Isije wakawa wamemlisha matango pori huyo mama!

Nani atoke Marekani aje Tanzania kutibiwa ugonjwa wa moyo?

Labda ni awe au wawe Wamarekani ambao tayari walikuwepo Tanzania [kwa sababu yoyote ile] halafu wakapatwa na matatizo ya moyo ndo wakapelekwa hapo kupata matibabu.

Ila mtu atoke Marekani na matatizo yake ya moyo aje Tanzania kwa ajili ya kupata matibabu hapo kwenye hiyo taasisi?

Ngumu kuamini….
 

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
89,734
2,000
Mkuu kuna diaspora ndugu wanweza kuamua kupunguza gharama
Yaani mbeba maboksi [kama mimi 😉] ambaye hana insurance [mimi sina health insurance 😉], na ana matatizo ya moyo, anarudi bongo kuja kupata matibabu hapo kwenye taasisi ya Kikwete?

Bongo huhitaji insurance kupata matibabu? Au ni bei rahisi kupata matibabu hata kama huna insurance?
 

Jp Omuga

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
4,508
2,000
Yaani mbeba maboksi [kama mimi 😉] ambaye hana insurance [mimi sina health insurance 😉], na ana matatizo ya moyo, anarudi bongo kuja kupata matibabu hapo kwenye taasisi ya Kikwete?

Bongo huhitaji insurance kupata matibabu? Au ni bei rahisi kupata matibabu hata kama huna insurance?
Mkuu kuliko ufie huko tusafirishe wapo ndugu watapenda uje huku. Najua kutibiwa umaanishi kupona!
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
6,580
2,000
Inawezekana kutibiwa imekuwa kama kuonja ladha ya chakula hotelini, sawa Marekani wanatibu moyo, lakini jamaa ametaka kutibiwa huku aone itakuwaje.
 

Bambushka

JF-Expert Member
Jan 9, 2020
2,656
2,000
Mmmh labda amemaanisha, watalii wanaojikuta wanaugua wanajua shida ni moyo, huwa wanaenda hapo.

Gharama ya usafiri tu, mmmh marafiki wa Prof Janabi?? Anayetudanganya tusile chakula cha sherehe!

Everyday is Saturday............................... :cool:
 

Majestic wolf

JF-Expert Member
Feb 10, 2015
1,249
2,000
Labda ni awe au wawe Wamarekani ambao tayari walikuwepo Tanzania [kwa sababu yoyote ile] halafu wakapatwa na matatizo ya moyo ndo wakapelekwa hapo kupata matibabu.

Hichi ndio sahihi. Kuna raia wakipatwa na shida wakiwa TZ, sio kwamba walifunga safari kutoka US kuja huko

Ngumu kuamini….[/QUOTE]
 

luckyline

JF-Expert Member
Aug 29, 2014
12,246
2,000
Na kiumbe ambae anatoka marekani akaja tibiwa tanzania anakuwa ana matatizo ya akili. Tanzania hii ninayoijua unapeleka mgonjwa unaambiwa dr ambae atamshughulikia mgongwa wako hayupo tusubiri aje?

Bora enzi za JPM nidhamu ya kazi ilikuwepo ma dr muda wote wako kazini, hata mgonjwa akizidiwa dr anakuwepo sio zama hizi ma dr lazima wapigiwe simu.

Juzi mtoto wa wifi yangu alimeza mbegu ya tunda fulani (silijui kwa kiswahili) hilo tunda ni tamu kwa juu ukila utamu ukaisha ndani kunabaki kama ile mbegu ya mparachichi sasa hiyo ndo aliimeza kwa sababu lina ukubwa kama ya yai dogo hakuweza kuimeza ikabana juu kama puani hivi. Mtoto ana 1.3yrs

Mtoto kimbiza dispensary wakasema hawamuwezi, kimbiza hospital nyingine huko ndo walikutana na vituko. Huyo sijui ni ness sijui dr ni mmama wala hakumgusa mtoto. Anauliza kameza nini? Wakataja hilo tunda kwa kiluga chetu wala hakujali alibaki amekaa anauliza hilo ni tunda gani? hakuwaambia chochote.

Mtoto ashavimba pua uso damu zinatoka wakampeleka hospital nyingine ma dr chap wakaanza kazi baada ya muda akapiga chafya kikatoka.

Ati kwa upuuzi kama huu mtu anatoka marekani aje tibiwa tz? Kweli hii dunia ina mambo mengi.
 

Kong Chi

Senior Member
Mar 15, 2021
100
225
Yaani mbeba maboksi [kama mimi 😉] ambaye hana insurance [mimi sina health insurance 😉], na ana matatizo ya moyo, anarudi bongo kuja kupata matibabu hapo kwenye taasisi ya Kikwete?

Bongo huhitaji insurance kupata matibabu? Au ni bei rahisi kupata matibabu hata kama huna insurance?
Hivi wewe ngabu mpaka leo unalia huna insurance? Mwanangu kamaliza high school soon atakuwa boss wako usipoangalia, tangu kina koba miaka hiyo wanakutukana bado unabeba box. Umekosea wapi ngabu?
 

Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
4,705
2,000
Pengine watu kutoka huko marekani wanakuja kwa shughuli zao ikiwemo utalii au wanadiplomasia ndio wakafika kutibiwa hapo afu punga mmja anasema wametoka Marekani.

Hii nchi ifike mahara kuwe na watu waliosoma na kuelewa sio kukariri na pia menejimenti za hawa wakubwa ziwe za kuajiriwa sio lazima mtu awe daktari Ili kuleta Uwajibikaji

Hata kama unatafuta sifa Rais sio mjinga kama wao ,huko Duniani anakujua vizuri sana kuliko wao.

Eti hospital yenyewe haina accredation ya WHO na ina upungufu wa majengo na wataalamu eti ndio watu watoke US kuja kutibiwa huku Bongo?

Hao hao ndio waliomba msaada wa bil.2 kwa Rais mbona wasiende kukopa bank?
 

Pslmp

JF-Expert Member
Mar 18, 2021
1,521
2,000
Mmarekani aletwe kuja kutibiwa Bongo?

kwanza hizo mashine saidizi za kufanyia operation zinatokea wapi vile😛
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom