Nani anastaili kuwa rais wetu ajaye nchini ? Tutafakari sasa,siyo baadaye ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani anastaili kuwa rais wetu ajaye nchini ? Tutafakari sasa,siyo baadaye !

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by BAOBAO, Oct 21, 2012.

 1. BAOBAO

  BAOBAO JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2012
  Joined: Oct 12, 2012
  Messages: 1,766
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Naomba sote,tuwachambue kwa uwazi bila ushabiki;wale wote tunatarajia watakuwa ni wagombea urais kupitia vyama vyao kama kweli wanastahili kuwa rais kipindi kijacho.Wana JF, tunaweza kabisa kupitia jamvi hili, kuwasaidia watanzania wenzetu kumpata Rais anastahili kuwaongoza watu kwenye mabonde na milima iliyojaa maziwa na asali.Tuanze majina kama Lipumba,Ndugai,Slaa,Lowasa,na wengine wengi.
   
 2. KALYOVATIPI

  KALYOVATIPI JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,419
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  zzk ndo rais atakaye leta matumaini kwa watz wengi
   
 3. l

  lukme Senior Member

  #3
  Oct 21, 2012
  Joined: Apr 18, 2012
  Messages: 191
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Slaa mpango mzima
   
 4. kimbangu

  kimbangu Member

  #4
  Oct 21, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 66
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 25
  Edward ngoyai lowassa is the best ov ol n he must be sworn in 2015
   
 5. M

  Mgaya D.W JF-Expert Member

  #5
  Oct 21, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 966
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 60
  Rais ajaye awe na sifa zifuatazo;-
  • Awe raia watz.
  • Awe na umri ambao katiba yetu inamtaka awe nao.
  • Awe mwadilifu.
  • Awe mzalendo wa kweli na dhati ya moyo wake.
  • Awe mchapakazi na asiyechoshwa na matatizo ya watz.
  • Awe na hekima na busara asiyeyumba kwa jambo lisilo na maslahi kwa Taifa lake.
  • Awe anajua tulikotoka,tulipo na wapi kama watz tunahitaji kwenda.
  • Awe anachukizwa sana na kukerwa na wizi,rushwa,ufisadi na uvunjifu wa sheria,haki na taratibu s kwa maneno pekee bali kwa matendo yake.
  • Awe ni yule kwake amani,utilivu na mshikamano vilivyopo vitalindwa kwa gharama yoyote.
  • awe ni yule ambaye atathamini rasilimali za nchi hii kwa manufaa ya watz wa sasa na kizazi kijacho.
  • Awe ni yule kwake ubaguzi ni mwiko kwa namna yoyote ile.
  • Awe ni yule atakayesimamia sheria za nchi bila woga.
  • Awe ni yule ambaye ni msikivu na mtulivu wa nafsi na akili.
  • Awe ni yule mwenye kuweka maslahi ya watz mbele naye kama kiongozi afuate.
  • Awe ni yule ambaye watanzania watamwamini bila shaka wala kinyongo.
  Haya ni kwa mujibu wa mawazo yangu mimi,kwa kuwa umetupa nafasi ya kutoa maoni basi nadhani huu ni wakati muafaka kuanza kuwajua viongozi wetu kwa sifa hizo kwa kuanzia na itakapofika wakati wa uchaguzi tutakuwa na majawabu yenye kujitosheleza.Ni matumaini yangu kuwa wanajamvi wataendelea kumwaga mawazo yao kadili kila mmoja alivyojaliwa kuona ila binafsi singependa nifungwe na jina la mtu anaehisiwa kwa kuwa miaka mitatu ni mingi,watu hubadilika,watu hupoteza maisha,watu hubadili mawazo,wanaweza wasiteuliwe katika vyama vyao,singependa kusemea nani mwenye kufaa kwa sasa lets time tell.
   
 6. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #6
  Oct 21, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Dr Wilbroad Peter Slaa,hakunaga kama yeye.
   
 7. BAOBAO

  BAOBAO JF-Expert Member

  #7
  Oct 21, 2012
  Joined: Oct 12, 2012
  Messages: 1,766
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Elezea matumani atakayoleta Zitto Kabwe kwa watz na jinsi atakavyoyafanikisha baada kuvuka vikwazo vya umri nk !
   
 8. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #8
  Oct 21, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Atafahamika JULY 2015
   
 9. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #9
  Oct 21, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Mkuu BAOBAO, nimeipenda hii thread lakini sijui kwanini hapo juu kuna watu wa ajabu ajabu...

  Anyway, my opinion ni kuwa tusiweke tumaini kubwa kwa yeyote yule...hasa kwa madudu yanayoendelea kutokea ila tuhasishane katika maslahi ya taifa, na Rais ajaye
  (REGARDLESS of chama atachotokea)..asimamie, kuilinda, kuongoza kupitia misingi hiyo.

  Nasema hivi kwa sababu,kila Rais ajaye anaanza moja( akisahau kuna mwingine aliyepita aliyaanzisha kitu fulani..mfano mzuri huyu wa sasa(MH. JM Kikwete)..alitokea huko huko CCM) lakini hali ni mbaya kuliko,kwa kila leo.

  Tuangalie, sifa, mahitaji, uwezo wa Nchi kwanza kabla ya kuweka Matumaini makubwa ambayo mwishoni yasipotimizwa mambo fulani tunasema "ningejua"... kwa kuwa na Utaratibu/ formula kama vile (Katiba/Constitution) ambayo tunaweza kuongozwa nayo, kwani katika hiyo ndipo yunaweza kuwajibishana...hata Rais mwenyewe kuwajibishwa.

  Hadi pale atapotokea mwingine kutangaza nia ya kugombea(ambaye sijamuona bado), ninadhani Dr. Wilbroad Peter Slaa anaweza kufanya jambo fulani.
   
 10. BAOBAO

  BAOBAO JF-Expert Member

  #10
  Oct 22, 2012
  Joined: Oct 12, 2012
  Messages: 1,766
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Asante kiongozi,nimetaja majina hayo kama mfano wa wagombea urais watarajiwa kupitia vyama vyao;kwa lengo la kuwajadili kila anayekusudia kutangaza nia ya kugombea urais tangu sasa au anayewatumia wapambe wake kupima upepo wakugombea urais !
   
 11. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #11
  Oct 22, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Asha rose Migiro -2015 zamu ya wanawake
   
 12. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #12
  Oct 22, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  Yote uliyoyasema ni madogo sana . Awe ni yule atakaye weza ku create jobs na kupunguza idadi ya watu wanaolima kwa misuri ya mikono.

  awe ni yule atakaye kataa influence ya mataifa kiarabu kuchukia Irsael, marekani na Ulaya magharibi.
  awe ni yule atakaye ongoza nchi kama Bunge, Mahakam kuu na idara ya utwawala vitakuwa huru.
  awe ni yule atakaye kukubali kushindania uraisi wakati tume ya uchaguzi , na Takuru viko huru.
  awe ni yule atakaye kukubali kushoitakiwa mara akifanya vibaya au kukubali rushwa.

  Jobs creation ni muhimu sana kuliko wino kwa hakimu. Huwezi kujivunia kuwa raisi wa nchi kama idadi ya wapiga kura kubwa ni unemployed. Hivyo mataifa yanayosaidia kutoa soko la ajira ni USA, Israel na Ulaya magharibi. sasa ukiona raisi hataki urafiki na mataifa hayo, basi huyo si mwingine bali ni mtesa watu. Halafu lazima ujue Ulaya, na marekani, ziko vizuri sana kiuchumi, lakini mafanikio yao yote yameletwa na adhabu ya kifo kwa wahujumu uchumi. Halafu lazima tumpate raisi ambaye aliuchukia sana mfumo wa Ujama na kujigemea na lazima taje dhambi za ujama ana kujitegemea zilivyo watesa watanzania hadharani.

  Kama hatatokea mtu kugombea uraisi ambaye hajaona dhambi za ujamaa na kujitegemea katika kuimarisha elimu , kucreate jobs, na kuboresha maisha ya wananchi, huyo hafai kabisaaa kuwa raisi wetu. Ni yale yale ya kuchukia matajiri, kuridhika na elimu ya UPE,na kunyenyekea mataifa ya waarabu!Kuamini kuwa pesa si msingi wa maendereo!!!
   
 13. BAOBAO

  BAOBAO JF-Expert Member

  #13
  Oct 22, 2012
  Joined: Oct 12, 2012
  Messages: 1,766
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Kiongozi,tukisubiri mpaka julai 2015 tuwafahamu;tutavuna mabua na visivyo dhahabu,kutokana nguvu kubwa ya mgombea katika kufanya kampeni kupitia mtandao wake tangu sasa.Wapo walioanza kutangaza hadharani kugombea urais,kama Zitto Kabwe ambao tuwatafakarikama wanastahili kuwa rais ajaye nchini.Tusisubiri media itutengenezee rais !!!!!!!
   
 14. BAOBAO

  BAOBAO JF-Expert Member

  #14
  Oct 22, 2012
  Joined: Oct 12, 2012
  Messages: 1,766
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Kama unawaza zamu ya mwanamke kuwa rais, kuwa Anna Tibaijuka ! Tuwachambue wote wanaofikiriwa kuutaka urais.
   
 15. BAOBAO

  BAOBAO JF-Expert Member

  #15
  Oct 22, 2012
  Joined: Oct 12, 2012
  Messages: 1,766
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Big up!. Kiongozi Tango, kutoa mawazo ni sawa na mbio za vijiti.Mgaya alianza,nawe utapokewa kijiti cha kutoa mawazo na wengine !
   
 16. BAOBAO

  BAOBAO JF-Expert Member

  #16
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 12, 2012
  Messages: 1,766
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Tutumie nafasi hii kuwaleta javini hapa,watarajiwa kugombea na kuwa rais ajaye kupitia vyama vyao kisiasa na hata kuweka vigezo vya rais anayestahili kushika nchi,baada ya dr.Kikwete
   
 17. baba juniho

  baba juniho Member

  #17
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 22, 2012
  Messages: 71
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Da aisee ni ngumu mno, maana kumjua mtu ni vigumu, ahadi hewa ndo zao wote, kwa kuwa ndo hivyo tena wanasema siasa ni propaganda, ni sawa na wale wa kale waliodanganywa sufuria inazaa jama tangu lini chuma/bati kikazaa??? sikia kupata mtu afaaye ni kama bahati nasibu, mtu mzalendo na mkweli ndo siku zote chama/Vyama vinampiga vita je atagombeaje??? dawa ni kupata katiba itakayoruhusu hata wagombea binafsi labda tutapatwa wigo wa kufanya best choice naweza sema" if Probability lack best sample it's so hard to get best outcome" so kwa mda huu tujitahidi tena katiba mpya ndo imekuja wakati muafaka, basi na tuitumie ili tujiongezee nafasi ya kuchagua kilicho bora, ili chama kikimnyima mtu tunaeona anafaa isivuruge Sample yetu, mtu huyo aweze kuja kwenye kinyang'anyiro kwa njia ya mgombea binafsi.
  Ila kwa hali ya ss bado chaguo langu na ambalo naona litawapa tumaini watz ni Dk. Slaa pekee sijui wenzangu.
   
 18. Mbonica VJ

  Mbonica VJ Member

  #18
  Oct 24, 2012
  Joined: Sep 27, 2012
  Messages: 77
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  EDWARD NGONYAI IS THE BEST
  :focus::focus::focus::focus::focus::focus:
   
 19. r

  radius Member

  #19
  Oct 24, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na huyo ni Dr. J. M. Pombe
  waziri mkuu Mwakyembe, waziri wa ulinzi na mambo ya ndani Lowasa. ndivyo nionavyo inafaa.
   
 20. M

  Mgaya D.W JF-Expert Member

  #20
  Oct 24, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 966
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 60
  muda ukifika tutajua kama ni hao ama la!
   
Loading...