Nani anastahili tuzo ya Nobel katika marais 6 tuliowahi kuwa nao Tanzania?

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,997
2,000
Baba wa Taifa tu wengine hawastahili tuzo ya aina yoyote ile.
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,997
2,000
Huyu si Mtanzania alishaukana miaka mingi na kuchukua uraia wa UK. Anaingia nchini kwa kutumia visa kama mgeni.

Bwana Douglas tutarajie mapambio na hongera nyingi sana kutoka kwa politicians kwa hili hapa...kama yuko nje watajipanga airport kumpokea (unafik na ubinafsi) hata kama hawakumjua wala kusoma kazi zake kabla....I said we should not focus on a political arena katika Nobel Price....

Viva Tanzania Hongera sana kwake.

Katuheshimisha kuliko.

View attachment 1967184

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Ng'wanamangilingili

JF-Expert Member
Aug 22, 2015
3,734
2,000
Huyu si Mtanzania alishaukana miaka mingi na kuchukua uraia wa UK. Anaingia nchini kwa kutumia visa kama mgeni.
Subiri utaona tu watakavyokurupuka. Huonagi hata wachezaji michezo or anybody that shines wenye uraia wa mbele walioikana bongo wanavyowasilolimisha Kwa lazima kuwa ni wakwetu wana asili yetu kwa ivo tuwapongeze tu.

NB uraia pacha is a thing

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
  • Love
Reactions: BAK

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,997
2,000
Wameshakurupuka Mkuu sijui Wizara ya utamaduni imeshamtumia hongera kama Mtanzania sasa Wabongo wanawaambia mpeni zawadi ya uDC kitu ambacho hawawezi kufanya maana inahusu kubadili katiba na katiba huwa hawataki kuigusa kwenye mambo wao HAWAFAIDIKI ila kama wanafaidika basi hawakawii kufanya mabadiliko.

Viongozi wa Tanzania wengi ni makima

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Douglas Majwala

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
1,124
2,000
Tanzania hakuna kiongozi anayefaa kutunukiwa tuzo ya Nobel kwani wana mengi ya kusontewa kidole kuliko kuenziwa.

Nyerere ndiye aliyeweka msingi mbovu ambao ndio umesababisha hii nchi kuwa masikini hadi leo kwa kuleta mfumo mbovu wa ujamaa akiifanya Tanzania kuwa maabara ya kujaribishia itikadi za kigeni.

Alifuta mfumo wa vyama vingi na kuleta mfumo wa udikteta wa chama kimoja na kuweka sheria ya kuweka watu kizuizini bila ya kuwafikisha mahakamani. Akatuingiza kwenye vita vya kijinga na Uganda kwa ajili ya rafiki yake Obote.

Nimechoka kwa sasa, nitawachambua hao wengine baadaye.
Siyo kwamba vita vya Kagera vilisababishwa na uvamizi wa Nduli na siyo urafiki wa Mwl na Obote:-

1) 1971 Nduli alishambulia mji wa Mwanza. Mwl akawa mvumilivu hakujibu, Nduli akaona kwamba Mwl hamuwezi, akatangaza kwamba baada ya Mwanza sasa anaingia hadi Dar es Salaam.
2) 1979 akavamia Kagera, akapiga, na kusogeza mpaka wa Uganda ndani ya Tz. Ungekuwa Mwl tuelimishe ungechukuwa hatua gani labda?
OIP.ZQc6Ab1hOh9wW_AfFx6OwwHaFj
OIP.ixUYOG2aipOcECaL7opGXgHaDt

Taswira zote kwa hisani ya google.
 
dos.2020

JF-Expert Member
Feb 17, 2009
5,380
2,000
Nobel hutolewa kwa mtu aliye hai tu. Leo hii Nyerere ana vigezo vya kuipata lakini anakosa sifa kwa vile hayuko hai. Mawazo ya Nyerere ya wakati huo yalikuwa hayakubaili nchi za Magharabi; lakini leo hii yanakubalika wakati yeye mwenyewe hayupo kuyazungumzia. Hasa hili swala la uhuru na kujitegemea!

nyerere alikua kiongozi wa ovyo mno, mawazo yake gani yanayokubalika? Ujamaa? au huu muungano unaoelekea kukata pumzi?
 
Douglas Majwala

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
1,124
2,000
Mkapa (Big Ben)

Honours
Order
Country
Year
Order of the Golden Heart of Kenya (Chief)Kenya
2005​
Order of Mwalimu Julius Kambarage NyerereTanzania
2011​

Awards

2007: Jane Goodall Global Leadership Award

Honorary degrees

University
Country
Degree
Year
Sōka UniversityJapanHonorary degree
1998​
Morehouse CollegeUnited StatesHonorary degree
1999​
Open University of TanzaniaTanzaniaHonorary degree
2003​
National University of LesothoLesothoDoctor of Law
2005​
Kenyatta UniversityKenyaDoctor of Education
2005​
University of Dar es SalaamTanzaniaHonorary degree
2006​
Newcastle UniversityUnited KingdomDoctor of Civil Law
2007​
University of Cape CoastGhanaDoctor of Letters
2008​
Makerere UniversityUgandaDoctor of Law
2009​
Big Ben hakuchagua kuitwa kwa salutation ya Dr licha ya kuzipewa tuzo hizo takriban 5. Sijui ni kwanini?

Mwl JK Nyerere
1633718937436.png

Mwl hakuchagua kuitwa kwa salutation ya Dr licha kuipewa tuzo hiyo. Sijui ni kwanini?

Rejea zote mbili kwa hisani ya Wikipedia.
 
Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
2,059
2,000
Tuzo ya kimataifa ya Nobel iliyoanzishwa na Bw Alfred Bernhard Nobel, Mswidi mbobezi wa kemia, uhandisi, mvumbuzi, mjasiriamali na mdiakonia (matendo ya huruma (philanthropist)) imetoa tuzo hiyo kwa Wanafizikia watatu kwa mpigo.

Swali:
Katika safu ya marais 6 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unadhani nani kati yao angeweza kustahili tuzo hiyo maarufu?

Kwa sababu zipi?

Kwanini imeshindikana?

Afrika Kusini wana Laureate 3, Liberia 2, DR Congo 1, Ethiopia 1, Kenya 1, Tanzania tumekwama wapi na juhudi zote nzuri za #AMANI YA NCHI, #ULINZI WA AMANI YA DUNIA, #UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA, #MIUNDOMBINU BORA, #MUUNGANO WA PEKEE DUNIANI, #OAU, #KUANZISHWA KWA NON ALIGNED MOVEMENT, #SOUTH SOUTH COMMISSION, #SADC, #EAC, na mengine mengi mazuri kimataifa. Ni Mwl. Nyerere ndiye aliingiza China kwenye kundi la mataifa yenye kura ya turufu katika Umoja wa Mataifa. Aidha alikuwa mmoja wa washauri wa Malkia wa Uingereza lakini hata tuzo ya heshima ya juu Uingereza ya "Sir" hakuwahi kuipewa. Naomba nikope maneno ya Paulo Mtume aliyeuliza hivi "Enyi Wagalatia mmerogwa na nani? Wagalatia.3:1"

Yote hayo na mengine mengi mazuri ya Tz bado Kamati ya Nobel haizioni tu?

Angalizo:
Changia mawazo yako kwa kutuonyesha hekima na busara zako ili tufaidike na maarifa yako, usichangie jazba za kuonyesha kejeli, dharau na matusi, utakuwa umetunyima maarifa yako.
MWENYE NCHI YAKE MBONA ANAJULIKANA KIPENZI MZALENDO wa KWELI KAFA MASIKINI KWA AJILI YA WATU WAKE hakujilimbikizia Mali hakuna na Hisa wala Majumba ya kifahari
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
12,234
2,000
nyerere alikua kiongozi wa ovyo mno, mawazo yake gani yanayokubalika? Ujamaa? au huu muungano unaoelekea kukata pumzi?
Huenda hujui kuwa uhuru wa kusini mwa Afrika ulisababishwa na mawazo ya Nyerere. Peace prize haifuati mawazo ya itikidi bali impact kwa maisha ya watu wengi, na kikawaida hutolewa baada ya muda mrefu kuona impact ya mawazo hayo. Ni wachache miaka ya hivi karibuni walioipata baada ya kip[indi kifupi: Malala,Obama na Al-Gore lakini hutolewa si chini ya miaka kumi.

Unaweza kumchukia kuwa hakuwa kiongozi mzuri kwa mawazo yako, lakini kum,be alikuwa na impact kubwa katika kuleta amani kwa watu wengi kusini mwa afrika
 
Imeloa

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
8,610
2,000
Siyo kwamba vita vya Kagera vilisababishwa na uvamizi wa Nduli na siyo urafiki wa Mwl na Obote:-

1) 1971 Nduli alishambulia mji wa Mwanza. Mwl akawa mvumilivu hakujibu, Nduli akaona kwamba Mwl hamuwezi, akatangaza kwamba baada ya Mwanza sasa anaingia hadi Dar es Salaam.
2) 1979 akavamia Kagera, akapiga, na kusogeza mpaka wa Uganda ndani ya Tz. Ungekuwa Mwl tuelimishe ungechukuwa hatua gani labda?
OIP.ZQc6Ab1hOh9wW_AfFx6OwwHaFj
OIP.ixUYOG2aipOcECaL7opGXgHaDt

Taswira zote kwa hisani ya google.
Baada ya Amin kunyakua madaraka nchini Uganda mwaka 1971, kulikuwa kukitokea "frequent border incursions" kwenye mpaka wa Tanzania na Uganda zikifanywa na majeshi ya Obote yaliyokimbilia Tanzania mara tu baada ya Obote kupinduliwa na Amin, majeshi hayo ya Obote yalikuwa pale Tabora.

Hili lilikuwa likifanyika kwa siri sana na hata mwaka 1978 kabla ya vita pia hayo majeshi ya Obote yalifanya tena uvamizi nchini Uganda na kisha kukimbia na kurejea tena Tanzania. Kimsingi, Amin alikuwa sahihi kwani yeye alichokuwa anafanya ilikuwa ni kujaribu kukomesha uvamizi wa mara kwa mara ktk ardhi yake.

Huu ndio ukweli ambao umekuwa ukifichwa sana na tawala mbalimbali za Tanzania japo ndio chimbuko la vita vyenyewe
 
MTK

JF-Expert Member
Apr 19, 2012
8,689
2,000
Tuzo ya kimataifa ya Nobel iliyoanzishwa na Bw Alfred Bernhard Nobel, Mswidi mbobezi wa kemia, uhandisi, mvumbuzi, mjasiriamali na mdiakonia (matendo ya huruma (philanthropist)) imetoa tuzo hiyo kwa Wanafizikia watatu kwa mpigo.

Swali:
Katika safu ya marais 6 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unadhani nani kati yao angeweza kustahili tuzo hiyo maarufu?

Kwa sababu zipi?

Kwanini imeshindikana?

Afrika Kusini wana Laureate 3, Liberia 2, DR Congo 1, Ethiopia 1, Kenya 1, Tanzania tumekwama wapi na juhudi zote nzuri za #AMANI YA NCHI, #ULINZI WA AMANI YA DUNIA, #UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA, #MIUNDOMBINU BORA, #MUUNGANO WA PEKEE DUNIANI, #OAU, #KUANZISHWA KWA NON ALIGNED MOVEMENT, #SOUTH SOUTH COMMISSION, #SADC, #EAC, na mengine mengi mazuri kimataifa. Ni Mwl. Nyerere ndiye aliingiza China kwenye kundi la mataifa yenye kura ya turufu katika Umoja wa Mataifa. Aidha alikuwa mmoja wa washauri wa Malkia wa Uingereza lakini hata tuzo ya heshima ya juu Uingereza ya "Sir" hakuwahi kuipewa. Naomba nikope maneno ya Paulo Mtume aliyeuliza hivi "Enyi Wagalatia mmerogwa na nani? Wagalatia.3:1"

Yote hayo na mengine mengi mazuri ya Tz bado Kamati ya Nobel haizioni tu?

Angalizo:
Changia mawazo yako kwa kutuonyesha hekima na busara zako ili tufaidike na maarifa yako, usichangie jazba za kuonyesha kejeli, dharau na matusi, utakuwa umetunyima maarifa yako.
Afrika na hizi sera za figisufigisu, rushwa, ufisadi, Utawala mbofumbofu haiwezi kutoa mshindi halali wa tuzo ya Nobel, hata kidogo! Angalia walikurupuka kumpa Waziri mkuu wa Ethiopia Ahmed Abiy tuzo ya Nobel angalia Hana hata miaka 5 madarakani huyo anaendesha mauaji ya kumbari Kule Tigray, kaskazini mwa Ethiopia, anajua raia wake mwenyewe kama Mwendakuzimu!
Afrika akili na hulka zetu ni kama ngozi ya Tako tu!
 
Andie

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
633
1,000
Anastahili Hangaya na sababu zake itakua:- "tuzo zote barani Africa wamekua wanapewa wanaume tu, wanawake wameonewa ni zamu ya wanawake yeye ni mwanamke, anachangiwa mbegu tu kila kitu anafanya mwenyewe haki sawa 50/50 ni wanawake wanastahili tuzo"

Yani haijalishi kama hawana uwezo wao wanadai nafasi kwa kigezo cha jinsia.

Ila sema mama ni feminist hatari.

Tuzo ya kimataifa ya Nobel iliyoanzishwa na Bw Alfred Bernhard Nobel, Mswidi mbobezi wa kemia, uhandisi, mvumbuzi, mjasiriamali na mdiakonia (matendo ya huruma (philanthropist)) imetoa tuzo hiyo kwa Wanafizikia watatu kwa mpigo.

Swali:
Katika safu ya marais 6 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unadhani nani kati yao angeweza kustahili tuzo hiyo maarufu?

Kwa sababu zipi?

Kwanini imeshindikana?

Afrika Kusini wana Laureate 3, Liberia 2, DR Congo 1, Ethiopia 1, Kenya 1, Tanzania tumekwama wapi na juhudi zote nzuri za #AMANI YA NCHI, #ULINZI WA AMANI YA DUNIA, #UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA, #MIUNDOMBINU BORA, #MUUNGANO WA PEKEE DUNIANI, #OAU, #KUANZISHWA KWA NON ALIGNED MOVEMENT, #SOUTH SOUTH COMMISSION, #SADC, #EAC, na mengine mengi mazuri kimataifa. Ni Mwl. Nyerere ndiye aliingiza China kwenye kundi la mataifa yenye kura ya turufu katika Umoja wa Mataifa. Aidha alikuwa mmoja wa washauri wa Malkia wa Uingereza lakini hata tuzo ya heshima ya juu Uingereza ya "Sir" hakuwahi kuipewa. Naomba nikope maneno ya Paulo Mtume aliyeuliza hivi "Enyi Wagalatia mmerogwa na nani? Wagalatia.3:1"

Yote hayo na mengine mengi mazuri ya Tz bado Kamati ya Nobel haizioni tu?

Angalizo:
Changia mawazo yako kwa kutuonyesha hekima na busara zako ili tufaidike na maarifa yako, usichangie jazba za kuonyesha kejeli, dharau na matusi, utakuwa umetunyima maarifa yako.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom