Nani anastahili lawama pavement za jiji la Dar kugeuzwa sehemu ya biashara?

O-man

JF-Expert Member
Nov 17, 2011
323
65
Imekuwa jambo la kawaida kuona watu wakiyumba kwa umahiri barabarani wakipishana au kukwepa magari. Sababu kuu ni kwamba sehemu iliyotengwa kwa ajili yao imehodhiwa na wafanyabiashara. Manunguniko hutokea endapo patatokea ajali au msongamano na mtu akaibiwa.
Kwenye makutano ya mtaa wa Swahili na Mkunguni kuna tawi jipya la Peoples Bank of Zanzibar. Hapa eneo la watembea kwa miguu limetekwa lote na hiyo benki. Hapo mahali upo msongamano mkubwa wa watu, magari ya mizigo na Daladala. Mtaa mwingine wenye tatizo sugu ni Sikukukuu kati ya mtaa wa Rufiji na Twiga. Hapa kuna mtu ana magari mengi sana kiasi cha kukifanya kipande hiki cha barabara kupitika kwa taabu sana. Kwa muda mrefu utakuta magari yake yameegeshwa mawili mawili kana kwamba hakuna mwenye haki zaidi yake. Ikumbukwe kwamba barabara hii iliboreshwa kwa kiwango cha lami ili kupunguza msongamano mta wa Msimbazi kwa magari yanayounganisha na Br. ya Morogoro kuelekea Magomeni.
Mtaa mwingine ni Swahili kuanzia mtaa wa Mafia hadi kwenye mataa ya Fire, eneo la watembea kwa miguu limetoweka mpaka miferejini.
Wale walio katika mamlaka wananufaika vipi na kadhia hii. Au mpaka itokee ajali ya kutisha ndiyo wafunguke? Ukija eneo la soko la Kariakoo maajabu yanaogezeka. Watembea kwa miguu wanaongozana magari. Segemu za barabara zimetekwa 'wapanga chini'.
 
Unawapigia mbuzi gitaa. Viongozi wetu wameamua kujenga mazingira ya kuchukiana ili tumalizane sisi wakati wao wakitumaliza. Ni Tanzania pekee ambapo watu wanaweza kufanyia biashara barabarani. Serikali haiwezi kuwagusa kwa vile watadai iwatimue wahindi waliovamia biashara hata wengine wakiishi kinyemela na viongozi kukosa pesa. Hivyo wanafanya umobutu ambapo kila kamanyola atajua jinsi ya kujilipa mshahara mradi amlinde.
 
Back
Top Bottom