Nani anastahili kukuita Mpenzi, darling, sweetheart

...it's 'Weird' pale mtu miaka nenda rudi alikuwa anakuita Darling, mkishaachana tu anakuita "lijanaume!" :D

We unasema kuachana,wengine wakigombana tu utasikia jina lako halisi badala ya la kimahaba kama ilivyokuwa mazoea yenu ya vionjo.
Well mwanamke kukuita lijanaume labda akiwa anaongea na watu ila hawezi kufanya straight kwa mwanaume hivyo!..Hisia yangu
 
Asante BJ,
Je nje ya hapo mtu akikuita darling na wakati hamna uhusiano?

Nje ya uhusiano, unaweza kuwa umezoeana sana na mtu mwingine akakuita hivyo(inategemea na kiwango cha mazoea kwakweli).Mara nyingi kama hujazoeana na mtu hata kama unamfahamu lazima ushangae imekuwaje.
Pia kwa sisi wanawake,binafsi na rafiki zangu kwenye mawasiliano huwa tunatumia sana kuitana majina kama hayo. Mfano wewe WoS,naweza kuwa huru kukuaddress 'mpenzi au darling' ni kawaida kwa ladies.
Halafu pia wazazi kutumia kwa watoto,kwenye darling unaongezea daughter/son(mara chache na inategemea na watu wanavyoishi).
 
lakini ikumbukwe kuwa katika kiswahili tuna majina yetu hutumika kuonesha kiasi gani unampenda na kumsamini mke au mpenzi kwa tafsiri nyingine (kumjali)kimapenzi kwa mfano tokea mababu wamekuwa na kawaida ya kuwaita wake zao au wapenzi wao neno Bibie kwa huku kwetu naimani ni sawa na hilo neno la kingilishi sweetheart ,lakini basi vile vile Neno Bibie kwa baadhi ya watu hapa Ni matusi makubwa kuna mama mmoja aliwahi kuitwa bibie kwa vile alivyopendeza kivazi chake na uzuri wake lakini alikasirika na kusema ametukanwa .
 
Nje ya uhusiano, unaweza kuwa umezoeana sana na mtu mwingine akakuita hivyo(inategemea na kiwango cha mazoea kwakweli).Mara nyingi kama hujazoeana na mtu hata kama unamfahamu lazima ushangae imekuwaje.
Pia kwa sisi wanawake,binafsi na rafiki zangu kwenye mawasiliano huwa tunatumia sana kuitana majina kama hayo. Mfano wewe WoS,naweza kuwa huru kukuaddress 'mpenzi au darling' ni kawaida kwa ladies.
Halafu pia wazazi kutumia kwa watoto,kwenye darling unaongezea daughter/son(mara chache na inategemea na watu wanavyoishi).

...hivi nikitamka, 'BJ you are such a darling'utanishangaa, wakati huo nikisubiria mkong'oto toka kwa mpwa?
 
Kutokana na kitu fulani ambacho tutakuwa tumeongelea au kimekufurahisha,hiyo ni njia mojawapo ya kusifia au kuexpress fikra zako hivyo sitokushangaa. Unless umeamua tu kuiandika,ha ha
 
...ndio maana yake :)
 
Hakuna ubaya wowote watu wa jinsia tofauti kuitana haya majina, kwa utamaduni wa TZ watu wataona ajabu iwapo mwanamke na mwanaume wataitana honey, sweet, little boy, babe, dear nk. iwapo hao watu hawana mapenzi ya kimwili kati yao. Sehemu za ughaibuni kuitana haya majina kati ya jinsia mbili tofauti inaoneka sawa tu, maana inaashiria upendo.
 
Hey honey bunch...how was your day?
 
Yanaleta maswali kama yepi? Unaweza kutoa mfano au mifano na muktadha (context) wa jinsi matumizi hayo yanavyoweza kuleta maswali...Thanks

huku makazini tunaona mambo mengi sana, utakuta mume wa mtu anamwita mke wa mtu sweetie, darling n.k, sasa kama ni mkeo unasikia anaitwa sweetie na mshkaji kwakua wako close tu kiurafiki na kikazi, hapo utamuelewa mshkaji kweli, si patakua hapatoshi hapo mywife wako kuitwa sweetie?
 
Its funny..mtu unapokuwa kwenye receiving end ndipo panakuwa hapatoshi LOL!
Hizi ndizo changamoto za maisha ya kisasa ndani ya utandawazi.Utandawazi umetuletea/umetukusanyia kila kitu na kutubwagia pwaa! Bahati mbaya sana hakuna package ya ku mitigate maafa/maumivu/matokeo yasiyotarajiwa yatokanayo na utandawazi huo.

Inatokea mara nyingi watu wanajikuta kwenye cross-fire bila kutarajia, mahusiano yanaharibika bila kutarajia, watu wanakosa amani...sasa tufanyeje?
 
Hakuna ubaya wowote watu wa jinsia tofauti kuitana haya majina, kwa utamaduni wa TZ watu wataona ajabu iwapo mwanamke na mwanaume wataitana honey, sweet, little boy, babe, dear nk. iwapo hao watu hawana mapenzi ya kimwili kati yao. Sehemu za ughaibuni kuitana haya majina kati ya jinsia mbili tofauti inaoneka sawa tu, maana inaashiria upendo.

kwa tamaduni za kitanzania, itakuwa ajabu iwapo mwanamke na mwanaume wataitana ...asali-roho, ...mtoto, ....la 'azizi, ...mpenzi, ...bibie, ...mamsapu, ...bwan'kaka nk? au ni tafsiri tu; moja "kidhungu", ingine kiswahili?
 
Neno dear naaminini halina maana ya mpenzi katika lugha yetu. huwa linatumika rasmi katika barua. Dear sir/madam maana yake nini kiswahili
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom