Nani anasema nyumba za shirika la nyumba ni za watu wa kima cha chini?

Experince ya National Housing niliipata wakati naanza maisha nikawa natafuta nyumba ya kupanga kwenye shirika hilo, nilipokwenda kwenye ofisi zao wakaniambia kwasasa hatuna nyumba lakini kama utaona kuna mtu anahama kwenye nyumba zetu njoo mara moja tuambie halafu tutakupatia! mpaka leo ni mwaka wa 10 sijapata kuona mtu amehama kwenye nyumba hizo na bado naishi kwenye nyumba za Tembe kama ID yangu inavyonekana hapo kushoto.
Lakini muhindi anatoka leo Bombay na anafikia upanga au kisutu,katikati ya mji nakufikia nyumba ya NHC!!shame on them!!
 
Ushauri kwa NHC (ingawa siyo kazi yao), wangeonyesha mfano wa mtu kakopa 82 million (kwa ajili ya Ubungo), makato yake kwa mwezi itakuwa kiasi gani say for 10yrs loan na 20 yrs loan. Both on the higher and lower side. Hii itasaidia kujua je ni affordable. Waache propaganda kuwa za Ubungo 50 % tayari zimeuzwa. Je za Dodoma wameuza ngapi pamoja na punguzo.
 
Tutofautiane kidogo wadau, kunafaida pia manake leo huna 82m na una 8.2m then unapata asset yenye value 82 na itakuwa ikiongezeka thamani.
Ukipangisha utakuwa unapata kodi itakayokusaidia kulipa mkopo.
Kujenga nyumba kwa pesa zako sio sifa na ukikopa ni rahisi zaidi, ila changamoto ni access to finance manake kkoo watu wananunua appartment kwa za ya ya dola 150,000.
Serikali haiwezi kukujengea bure, gadafi na karume alijaribu. Chemsha bongo angalia utapataje fursa kuliko kulalama wakati wengine wanapiga bao. Kuweni positive mtaweza tu, kama unapata na airtime ya kuchat wewe sio masikini labda unafikra za kimasikini.
 
Tutofautiane kidogo wadau, kunafaida pia manake leo huna 82m na una 8.2m then unapata asset yenye value 82 na itakuwa ikiongezeka thamani.
Ukipangisha utakuwa unapata kodi itakayokusaidia kulipa mkopo.
Kujenga nyumba kwa pesa zako sio sifa na ukikopa ni rahisi zaidi, ila changamoto ni access to finance manake kkoo watu wananunua appartment kwa za ya ya dola 150,000.
Serikali haiwezi kukujengea bure, gadafi na karume alijaribu. Chemsha bongo angalia utapataje fursa kuliko kulalama wakati wengine wanapiga bao. Kuweni positive mtaweza tu, kama unapata na airtime ya kuchat wewe sio masikini labda unafikra za kimasikini.

songambele,
sioni hoja uliyoandika hapa zaidi ya kupotosha mada kwani ni wazi huelewi utaratibu uliotumika na nhc. hio nyumba ya 82M hupewi mpaka uikamilishe hio fedha, na hio 8M ni kitangulizi tu. unakuja kutuchanganya tu na hizo usd150,000 tutazipata wapi sie??

hamna alieomba ajengewe nyumba bure, bali nyumba zijengwe na zipewe reasonable price ili wananchi wa kawaida nao wajaribu. Hamna mgeni kwenye ujenzi hapa?? wala hamna ombaomba hapa; ila nyumba ya 30M-50M ni kubwa na unapata vyumba vitatu. Tatizo labda wewe labda umepewa ya urithi ama umepata kwa fedha zisizo halali ndio maana huoni shida.
 
NHC mapumbavu tu....sijui hiyo business plan nani aliwaandikia....nani anunue ujinga huo?Niache kujenga nyumba yangu ya 30mil ikiwa full hadi garden napata.....majinga kweli haya,sometimes nashindwa kuyaelewa.....hata hao matajiri hawatanunua,wazipeleke wapi?labda uniambie kuna mchongo wa kuwapiga NHC hao baada ya kulipa 8mil then kuna jinsi ya kuwachomoka na apartment ukala na kikazi unachofanya ukapiga chini,makato hamna.....kama kuna uwezekano wa kuwapiga ndio nitakua interested,otherwise tupa kule upuuzi huo!



Mkuu, kwa taarifa zilizopo ni kwamba tayari zaidi ya asilimia 50 ya nyumba za ubungo wameshauza. Ni kweli watanzania wengi ni masikini, lakini usishangae utakaposikia kwamba walio omba kununua wamezidi idadi ya nyumba zilizopo.
 
Mkuu, kwa taarifa zilizopo ni kwamba tayari zaidi ya asilimia 50 ya nyumba za ubungo wameshauza. Ni kweli watanzania wengi ni masikini, lakini usishangae utakaposikia kwamba walio omba kununua wamezidi idadi ya nyumba zilizopo.
Mkuu kununua nyumba zote si tatizo maana watanzania kwa kukimbilia mambo sisi ndio wenyewe, shida inakuja wakati wa kulipa hapo ndipo kuna kazi na utasikia karibu zote ziko kwa madalali...
 
Kumbuka, Tanzania hii hata Waziri au Rais analipwa kima cha chini. Ni nani mwenye mshahara wa kima cha juu ambae yupo Serikalini au mtumishi wa umma? Ambae anaweza ku "afford" baada ya kutowa gharama zake zote za maisha, kujenga majengo tunayoyaona watu wanashindana kuyajenga? Mimi nakuambia hakuna.

Woooooote wizi. Hakuna mmoja mbora kati yao.
 
Leo kuna Watanzania ambao ni maofisa utawala tu, au Mameneja wa idara au wakurugenzi. Wana mali kuliko kodi walizolipa, tuanze kukamatana wachawi, ni nani ataebaki?
 
http://www.nhctz.com/images/NHC_STRATEGIC_Plan_Exec_Summary.pdf

Tusiwe wakali jamani! Read the above linked report and you will notice that it is clearly stated that in order for them to progress forward the upper and middle income class is the market that will allow them to do so.

"It might sound prudent to construct more houses to the low income group thanto the high and medium income groups. However, in a situation where NHC is
expected to operate commercially while utilizing funds from financial institutions
and banks, it is also expected to repay the loans in time. Houses constructed for
the low income group will not be able to sustain the needed funding arrangement.
Therefore, NHC intends to construct more houses for the high and middle income
groups so as to be to make profit and possibly subsidize the construction of a
minimum of 5000 houses for the low income group."

Do they still have a social responsibility towards the lower income class? absolutely! But it also makes sense that they are striving for sustainability first. As far as how well the new boss has done so far, let me tell you this my grandma lives in a NHC house and rent has gone up and they are way more diligent in collecting it and the house is actually looked after i.e. repairs and such. I know it might be a bit of a silly example but it still highlights improvement. BTW before you get on my case, my grandma had to wait until a someone died before she got the house.

As far as their mortgages are concerned, that's how mortgages work anywhere is the world. You end up paying at least double of what you initially borrowed, that's why banks are evil. The lack of a good credit system in TZ does not help either because in Western countries you are looking at interest rates below 5%, in TZ I'm not sure what the figure is but I know it's in the upper tens.

Hakuna cha ukali ni facts tu zitembee. Shirika hili si la kibiashara ni la kuhudumia umma kwa maendeleya watanzania na tanzania yenyewe kwa ujumla. Hizo nyumba wanazoziuza sasa hivi labda chini ya asilimia moja ya watanzania ndio wenye uwezo wa kuzikopea hela, achilia mbali kuzilipia moja kwa moja.
Sera unayoisema au mkakati huo wa kujenga nyumba za bei ghali kwanza hauna tija kwa mtanzania wa kawaida na ungeweza kufanywa na taasisi binafsi. Hata NSSF na PPF walijenga nyumba kubwa kuliko zao na wakaziuza kwa bei ndogo kuliko hizi za NHC. Ni mkakati mbovu kwa sababu wenye kipato cha kawaida na cha chini (ambao ndio wengi) wataendelea kusubiri kama vile shirika hili halipo.
Kwa nini asilimia kubwa iendelee kuwa na makazi mabovu wakati kuna shirika lao lililokarabatiwa. Kwa nn waendelee kusubiri wakati shirika hili ni tajiri, kwa maana ya mali (nyumba na viwanja) ambavyo vingetosha kudhamini mikopo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za bei nafuu? Kwa nini waTz waendelee kuangalia matajiri wachache wakikaa kwenye nyumba walizojengewa na shirika la umma wakati wao wakisubiri wajukuu zao ndo waje kukaa pazuri. Maana kwa sasa haiwezekani, bei ni kubwa na wameambiwa wasubiri wenye pesa wahudumiwe kwanza, zamu yao itakuja miaka 100 ijayo.
NHC watafute mikopo rahisi, waitumie serikali kupata mikopo isiyo na riba kutoka nchi kama china na watumie mikopo hyo kujenga nyumba za bei nafuu kwa ajili ya watanzania. NHC sio shirika linalotafuta faida kubwa, labda kama limebadilisha sera.
Tusitetee hata kidogo, waTz wenye kipato cha kawaida(ambao si matajiri wenye uwezo wa kununua nyumba za NHC), hawafaidiki hata kidogo na NHC ya sasa
 
Mnaoilaumu NHC mnakosea sana. Tangu lini NHC ikawajali wananchi? Ukitaka kujua nimaanishacho angalia wapangaji wake ambao karibu wote ni wahindi au watu wenye vyeo vya juu au jamaa wa wakubwa serikali na wafanyakazi wa NHC yenyewe. Ukitazama hata hiyo nyumba ya mil 82 wanayoongelea utakuwa wanaijenga si juu ya robo ya hiyo bei wanayotangaza. Mmesahau usanii wa Tanzania? Heri udundulize vijisenti vyako ujenge taratibu hata kama ni kwa miaka 15, in the end utakuwa nyumba yako isiyo na mkopo wala ulanguzi huu na wizi wa mchana kweupe. Saa nyingine NHC wanataka watumie gear ya kujenga nyumba za bei nafuu kupata viwanja sehemu nyeti washirikiane na wakubwa wajenge halafu wajifanye wameuziana wakati wamepora hivyo viwanja.
 
nyumba ya 82 vyumba viwili! huu ni wizi wa mchana ,Inamaana watanzania hawajui gharama za ujenzi ama!?

Bado hiyo miradi haijafanyiwa "due diligence" ovehead expenses ni kubwa sana ndiyo inayopelekea gharama ziwe juu. Ikifanyiwa uchunguzi unaweza kuona ni kama ile ya Twin Towers ya BOT. Obvious Mtu wa kipato cha chini asahau kabisa kumiliki nyumba kwa mpango huu wa NHC , na ni bora atafute njia nyingine au atafute Wataalam wa mambo ya kifedha wampe ushauri kwanza kuliko kuingia kichwa kichwa. NHC wako kibiashara na gharama zao za uendeshaji wa Shirika zinaingia kwenye gharama za hizo nyumba. Ni sawasawa na kuwalipia matumizi yao ambayo yanawezakuwa yanaongeza kiujanja kwa faida ya Wachache.
 
Kiukweli mradi huu utazinufaisha Benki zaidi kuliko Watanzania wengi, Najua kuwa ujenzi wa nyumba kwa sasa hivi ni gharama sana, Lakini NHC Ingeweza kufanya vizuri kwa kushirikisha mifuko ya Jamii kama NSSF au PPF. Kwa wale waliochanga pesa za kutosha uko wangeweza kufanya mikataba nafuu kwa dhamana za michango yao kwa interest ilio nafuu na wakaweza kumiliki nyumba hizi, na risk haiwi kubwa sana kuliko kwenye mabenki.Mfano NSSF Kwa mwanachama aliyechangia amount fulani ingeweza kumpa loan ya 5-8% KWA MIAKA 5-10. Kulipia nyumba kwa muda mrefu wa miaka 15 ni wizi wa wazi wazi, Na ni mzigo kwa mfanyakazi.
 
Experince ya National Housing niliipata wakati naanza maisha nikawa natafuta nyumba ya kupanga kwenye shirika hilo, nilipokwenda kwenye ofisi zao wakaniambia kwasasa hatuna nyumba lakini kama utaona kuna mtu anahama kwenye nyumba zetu njoo mara moja tuambie halafu tutakupatia! mpaka leo ni mwaka wa 10 sijapata kuona mtu amehama kwenye nyumba hizo na bado naishi kwenye nyumba za Tembe kama ID yangu inavyonekana hapo kushoto.

Were you serious on that move?
 
Lakini Anti-Fisadi...hiyo nyumba ya milioni 30-40 ya vyumba vitatu utaijenga wapi katika eneo lile la Ubungo ambapo kiwanja pekee si chini ya milioni 100? Mi hawa jamaa nawaelewa kwa upande huo zaidi..wanajenga maeneo ambayo yanafikika na yapo mjini kabisa,waingereza wanaita prime areas. kama ni kujenga nyumba ya milioni 30 chanika,sawa! ila mafuta ya gari au nauli za daladala kila siku hadi kufika mjini na kurudi...ulinzi n.k vyote vitafanya mwisho wa siku unatumia zaidi hata ya kile wanachosema NHC sasa hivi. Cheap is expensive....ni hayo tu
 
Hamna cha prime area wala nini. Kiwanja kile kimejengwa nyumba 80, ukigawa hiyo thamani ya kiwanja haiwezi kuwa hata milioni 5 kwa nyumba moja. Na kama wanathaminisha nyumba zao kwa market price faida ya kuwa na NHC ni ipi sasa??? wao wanatakiwa kurahisishia wananchi wa Tanzania kuwa na makazi bora kwa bei nafuu. Kutakuwa na tofauti gani sasa na wale wafanyabiashara binafsi wanaojenga apartments na kuzipangisha kwa dola upanga na mjini huko. This simply doesnt make sense, uwe na shirika la umma lenye sera kama za kampuni binafsi inayotafuta faida. SERA MBOVU
 
kweli kabisa,tusidanganyane na swala la prime area! Kuwa shirika la umma,ni kuangalia maslahi ya wananchi walio wengi;sasa hapo wameangalia nini? Bado n nyumba ya vyumba viwili tu ndani ya congested enviroment.

Ni mradi upi hawa waliufanikisha kwa maslahi ya wengi? Kama kule boko waliishiaga kununua wachache nyumba kumi kumi,kumebakia kukaa vichaka tu bila watu! Ukiuliza wenyewe wapo masaki,au nje ya nchi?? Kwaio sishangai hata leo wakisema ubungo zimeuzwa zote kwani bado utakuta mtu mmoja kanunua nyumba hata 5.

Tz ni ya ujanja ujanja tu
 
Niliwasiliana na mmoja wa afisa masoko wa NHC kujua zaidi bei az apartment za Ubungo... kwa maelezo yake..
Bei: 67 Mil Tz Shillings
Muundo wa nyumba: Vyumba 2 kulala.. Sebule na sehemu ya chakula..choo cha umma.. sehemu ya maegesho ya gari na sehemu ya udobi..ktakuwepo na shopping complex hapo..
Malipo ya awali: 10%
Dhamana: Barua ya NHC kukutambulisha kama mkopaji pale benki ili ukopeshe Mil 67 uwalipe NHC ..
Mradi ukishakamilika: hati ya umiliki inakbidhiwa kwa benki uliyokopa ili na wewe unailipa benki huo Mkopo+RIBA:crutch:.....!!!

BINAFSI... Sijaona thamani ya mkopo kwa bei ya Mil 67(riba sijalipa) kwa nyumba ya kabila hiyo... labda kama sijapewa maelezo sahihi...!!!
Naombeni ufahamu..

Kuna mtu anaweza toa ufafanuzi wa hoja za huyu mkuu. he/she has a big point!
 
Mbona nimefika eneo lenyewe mbona ni yale magorofa ya urafiki sioni majengo mapya????? Huo mrtadi ni upi????
 
Vipi hawatoi Mikopo ya football stadium nami nikope niendeleze soccer bongo viingilio bei poa
 
Back
Top Bottom