Nani anamlinda RCO Kilimanjaro Ng'anzi anaendelea na biashara za Magendo?


R.B

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Messages
6,294
Points
2,000
R.B

R.B

JF-Expert Member
Joined May 10, 2012
6,294 2,000
LA mgambo limelia wasomaji wangu natumaini nyote hamjambo na mnaendelea na majukumu yenu kama kawaida. Tunakutana tena Jumapili ya leo kujadiliana mambo mbalimbali ambayo yametokea ndani ya taifa letu.

Leo bila kupoteza wakati wasomaji, maada kuu inahusu Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Kilimanjaro (RCO), Radhaman Ng’anzi.

Kwa kipindi kirefu sasa jeshi la polisi limekuwa likipitia milima na mabonde kujiweka sawa mbele ya jamii.

Mtakubaliana na mimi kwamba wakati wa utawala wa aliyekuwa mkuu wa jeshi hilo, IGP mstaafu Omar Mahita, jeshi hilo liligeuka chaka la wezi, majambazi na wabambikaji kesi kwa watuhumiwa.

Nani nabisha hakukuwa na ujambazi wa kutisha! Kumbukeni jinsi majambazi walivyotamba mchana kweupe na kupora mamilioni ya fedha katika miji mikubwa kama Dar es Salaam, Arusha na Mwanza.

Kumbukeni namna ambavyo wananchi walikuwa wakibambikiziwa kesi za mauaji. Naweza kusema kwa wakati huu wimbi hilo limepungua kidogo.

Nani asiyetambua utawala wa Mahita, ulivyoshusha heshima ya polisi mitaani kwetu! Kama msomaji wangu unabisha rudisha kumbukumbu zako nyuma kuanzia miaka 2003 na 2006 mwanzoni.

Nani anabisha namna ambavyo, Mahita na wasaidizi wake wakuu wakati huo, walishindwa kuchukua hatua madhubuti za kukabiliana na hayo yote.

Nani anabisha jinsi majambazi walivyokuwa wakiteka mabasi na kusema ‘mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe’. Hayo yote, Mahita, Adadi Rajab (DCI), Lauren Tibasana walikuwa wanayaona!

Sasa baada ya kizazi cha Mahita kung’olewa, akaja kamanda asiyekuwa na makuu, IGP Said Mwema.

Moja ya kazi ya kwanza ambayo Mwema aliamua kukabiliana nayo ni ujambazi na kurudisha heshima ya jeshi hilo karibu na wananchi, kwa sababu hao ndiyo wadau wake wakubwa.

Moja ya kazi kubwa aliyoifanya, ni kuondoa uozo wa makamanda wa polisi wa mikoa ambao walikuwa vinara wa kushirikiana kwa namna moja au nyingine na majambazi.

Wengi wao tuliona wanahamishiwa ‘kijiweni’ yaani makao makuu Dar es Salaam.

Lakini kazi nyingine iliyofanywa na IGP Mwema ni kuanzisha polisi jamii na kuagiza makamanda wake kutoa namba zao za simu za kiganjani. Haya yote ni matunda makubwa.

Siwezi kusema kwamba IGP Mwema kamaliza uozo kwani kwenye utawala wake tumeshuhudia matukio makubwa ya mauaji na upigaji mabomu ambao sijawahi kuhushuhudia maishani mwangu.

Turudi kwenye mada, juu tukio la RCO Ng’anzi ambaye anadaiwa kuwa ni mmoja wa maofisa wa juu wa polisi anayeshirikiana na wafanyabiashara katika biashara ya magendo mkoani Kilimanjaro.

Siku ya kwanza niliposikia habari hizi sikushutuka sana kwa sababu mkoa wa Kilimanjaro umekuwa kama umelaaniwa kwa maofisa wa polisi kujihusisha na biashara ya magendo.

Itakumbikwa mwishoni mwa mwaka jana, aliyekuwa RCO wa Mkoa huo,Obadia Nselu aliondolewa wadhifa wake na kurejeshwa makao makuu baada ya kutuhumiwa kujihusisha na rushwa ya magendo ya sukari licha ya tuhuma hizo kuzikana.

Naye RCO Ng’anzi ameingia kwenye kashfa hii, safari hii akihusishwa na tuhuma za kuwalinda na kuwakumbatia wafanyabiashara wanaojihusisha na usafirishaji wa sukari kwenda Kenya kwa njia za magendo.

Lakini katika hali ya kustaajabisha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Robert Boaz anapoulizwa anaonekana kukwepa kuzungumzia tuhuma hizi.Iweje asijue kama msaidizi wake huyo anajihusisha na biashara hiyo haramu? Hapa inaonekana wazi analinda kitumbua kisiingie mchanga! Nawaambia ipo siku uozo wenu utajulikana.

Ni wazi RCO Ng’anzi, anaonekana kuwa kikwazo katika mapambano dhidi ya biashara ya magendo kutokana na kuwa na uhusiano wa karibu na wafanyabiashara hao. Nina taarifa kuwa mmoja wa wafanyabiashara hao anatoka Wilaya ya Mwanga.

Nina taarifa kuwa tuhuma dhidi ya RCO huyo imo kwenye taarifa ya siri ya kurasa tano iliyotumwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na wananchi wema ambao wamekuwa wakishuhudia magari yanavyovusha sukari kila kukicha.

Lakini mtandao wa RCO huyo umepanuka zaidi ambako inadaiwa anashirikiana vizuri na viongozi wa Wilaya ya Mwanga, akiwemo Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mwanga (OCD),OCD Rombo Msaidizi wa Mkuu wa Kituo cha Polisi Himo.

Wengine waliohusishwa kwenye mtandao huo ni maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutoka ofisi kuu ya mamlaka hiyo na wale walio katika Kituo cha Ushuru na Forodha katika mpaka wa Holili.

Hawa wamekuwa mabingwa wa kupitsha magari usiku na mchana ambayo yanavusha sukari kama yanavyotaka. Najiuliza, hivi RCO huyo na mtandao wake wamejitangazia ‘Jamhuri yao’?.

Haiwezekani hata kidogo askari aliyepata mafunzo mazuri na kuheshimu kazi yake, ageuke kuwa mfanyabishara ‘bubu’ kwa kupitia migongo ya watu wengine.

RCO gani huyu? Inaonekana wazi wafanyabiashra hao wanapokamatwa na polisi wadogo humpigia simu na kutoa amri ya kuachiwa! Kibaya zaidi inadaiwa huwatolea maneno makali polisi wa chini wakati wanapowatia mbaroni wafanyabiashara hawa. Jamani IGP Mwema huyo mtu hakufai. Taarifa hiyo imefichua kuwa wafanyabaishara hao wamekuwa na uhusiano wa karibu na RCO huyo na humpigia simu wanapokamatwa na askari wa ngazi ya chini. Inadaiwa amekuwa akiwakaripia askari hao na kuwaamuru waondoke mara moja katika maeneo yanakopita magari hayo.

Mwishoni mwa mwaka jana aliyekuwa mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Kilimanjaro (RCO),Obadia Nselu,aliondolewa wadhifa wake huo na kurejeshwa makao makuu ya jeshi la polisi baada ya kutuhumiwa kujihusisha na rushwa ya magendo ya sukari,licha ya tuhuma hizo kuzikana.

Polisi na TRA, wamekuwa kitu kimoja kupitisha magari mengi kwa siku. Inaelezwa karibu magari ya Fuso 12 hadi 15, yaliyobeba sukari yamekuwa yakivuka mpaka na kuingia Kenya. Hivi jamani nani kawaloga hawa polisi wetu? IGP Mwema nakuomba uuangalie vizuri mkoa wa Kilimanjaro.

Najiuliza hivi kweli RCO huyo njia hizi hazijui? Kutoka mji wa Himo kupitia barabara ya Lower Moshi hadi yalipo machimbo ya mchanga ya pozolana na kuingia Kenya sehemu inayojulikana kwa jina la Kwa Mandara, ikiwa ni mita chache kutoka Holili.Hili linahitaji majibu.

Njia nyingine ni kutoka katika mji huo wa Himo kupitia Marangu, Mwika, Mamsera, Ibukoni wilayani Rombo na kuingia katika Kijiji cha Munga kilichoko mpakani mwa Tanzania na Kenya ambako magari hayo hupata urahisi wa kuingia Kenya eneo linalofahamika na polisi wa Rombo, liitwalo Chumvini.

Katika Wilaya ya Mwanga, magari yaliyosheheni sukari ya magendo huanzia safari zake katika eneo la Njiapanda ya Himo, baada ya kupakia sukari Moshi mjini na kuelekea vijiji vya Kileo na Mnoa, kabla ya kuingia Kenya eneo maarufu la Madarasani au Kitobo. Hapo ndiyo makao makuu ya kusambaza sukari yetu kwa taifa zima la Kenya.

Baada ya maelezo hayo,naomba kutoa mapendekezo yangu.

Mosi, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro atumie madaraka yake kuhakikisha anamuita RCO huyo na kumhoji.

Pili, haiwezekani tukaendelea kufuga polisi ambao wanakiuka miiko ya kazi.Tunataka kusikia hatua za nidhamu zinachukuliwa haraka.

Tatu, namshauri IGP Mwema afanye uamuzi mgumu dhidi ya RCO huyo i kurejesha imani kwa wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro.

Nne,namshauri IGP Mwema afanye ziara za kushtukiza katika maeneo yanayolalamikiwa ajionee ‘ulaji’ wa watu wake na achukue hatua.

Tano, namshauri IGP Mwema asikubali polisi mmoja au wawili wachafue sifa ya jeshi hili ambalo sasa linaonekana kurudi karibu na wananchi.

Sita, najiuliza RCO huyo anapata wapi jeuri hii? Inawezekana kuna mkubwa nyuma yake anamfanye asishutuke.

Leo namalizia kwa kuuliza, hivi ni lini jeshi la polisi litaachana na tuhuma za aina ya Ng’anzi? Tumechoka, tunataka kuona hatua zinachukuliwa.IGP Mwema usiwafumbie macho askari aina ya RCO huyu. Hivi polisi wameumbwa watu wa kulalamikiwa kila kukicha? Nani anamlinda RCO Kilimanjaro?
 
Daudi Mchambuzi

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Messages
39,393
Points
2,000
Daudi Mchambuzi

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined Nov 25, 2010
39,393 2,000
askari wa kilimanjaro ni wauwaji wakubwa wa raiya.
 
K

katalina

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2012
Messages
264
Points
0
K

katalina

JF-Expert Member
Joined Apr 4, 2012
264 0
Kama vile ulikosa mgao vile....?! Mkuu wa mkoa amhoji RCO kwani yeye PCCB au hujui mamlaka yake. RCO anashirikiana na TRA, mbona hukumtaja huyo wa TRA kama ulivyofanya kwa RCO - huoni kama unachuki binafsi na RCO? Hata hivyo nakupongeza kwa uthubutu wako huo........
 
M

Magesi

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2012
Messages
2,588
Points
0
Age
35
M

Magesi

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2012
2,588 0
Mkuu mkoa wa kilimanjaro polisi wanapenda sana kufanya kazi mkoa huu sababu ya madili hata wakuu wa polisi nchini wanajua Rpc Ngoboko kilichomuua ni presha dili flani hivi lilitaka kulipuka.
 
N

ngonani

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2012
Messages
1,371
Points
1,250
N

ngonani

JF-Expert Member
Joined Aug 27, 2012
1,371 1,250
Mtoa mada ni polisi na kama sikosei alikuwa ofisi hiyohiyo ya RCO na inawezekana aliondolewa na RCO kutokana na tuhuma za kujihusisha na magendo,kwa hiyo ana visa binafsi na RCO,anataka RCO aondolewe ili yeye asuke arudishwe tena ofisi ya upelelezi ili aendelee kufanya magendo ya sukari.Askari bwana.........
 
Sangarara

Sangarara

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Messages
13,114
Points
2,000
Sangarara

Sangarara

JF-Expert Member
Joined Sep 29, 2011
13,114 2,000
wewe ngonani unasema mtoa mada ni polisi kama hukosei na kwamba alikuwa ofisi hiyo hiyo ya RCO na nataka RCO aondolewe ili jamaa arudishwe,hebu soma vizuri hiyo makala na ukasome makala iliyoandikwa kwenye gazeti la mtanzania jumapili novemba 25,2012 kwenye waraka kutoka mwitongo page 8 utaona jina la aliyeandika hiyo makala na ufanye uchunguzi kama aliwahi kuwa askari katika ofisi ya RCO K'njaro,acheni kupakazia mwandishi kaandika maoni yake kazi yako ni kusoma na kutoa maoni na si kusema ni chuki binafsi umefanya uchunguzi gani kubaini ni chuki binafsi?,au na wewe upo kwenye mtandano wa RCO?,kwanza huyo RCO Ng'anzi kaja juzi tu lakini tunaona amekuwa na mabadiliko makubwa kiuchumi,wewe unatetea nini kama si uchuro?
 
Inno laka

Inno laka

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2012
Messages
1,604
Points
1,500
Age
27
Inno laka

Inno laka

JF-Expert Member
Joined Mar 24, 2012
1,604 1,500
Ebu fanyeni mambo yenu achen kufatilia maisha ya watu...tafuten na nyie.
 
B

Bangoo

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2011
Messages
5,600
Points
1,195
B

Bangoo

JF-Expert Member
Joined Nov 3, 2011
5,600 1,195
# kumwambia aache kusema siyo sawa , kama ni kweli huku jf maofisa wengi wanapitiaga hapa watalifanyia kazi.
Safisha nchi itakate
 
Zogwale

Zogwale

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2008
Messages
12,290
Points
2,000
Zogwale

Zogwale

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2008
12,290 2,000
Kilimanjaro wanapapenda sana maana dili ni nyingi sana!! Ikiwemo za wezi wa magari!!
 
Nicholas

Nicholas

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Messages
25,231
Points
2,000
Nicholas

Nicholas

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2006
25,231 2,000
polisi jamii ipi kaanzisha Mwema?Sisi tumekuwa na Sungusungu kwa miaka kibao.
 

Forum statistics

Threads 1,296,633
Members 498,713
Posts 31,254,458
Top