Nani anamkumbuka msanii Ali Kiba?, Kwa sasa yupo wapi?

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
Habari wakuu,

Ni kitambo sana msanii Ali Kiba hajasikika vinywani mwa watu, hajaonekana kwenye matukio yoyote na wala haandikwi kabisa na vyombo vya habari vya Tanzania, Afrika na hata dunia nzima.

Hata hapa JF nimejaribu kuangalia Jukwaa la ''Celebrities'' page ya KWANZA mpaka ya TANO hakuna mada inayomhusu moja kwa moja. Iliyopo kati ya Page hizo ni Kwanini Ali Kiba hataki bifu lake na Diamond liishe?.

Nilisikia ana show ulaya lakini sioni video wala picha mnato. Je, ni kwamba Show zimebuma mpaka anaogopa kuwaonesha mashabiki zake nini kinaendelea?

Mara ya mwisho katoa wimbo wa AJE na kaufanyia remix zaidi ya mbili, je ni kwamba kaishiwa utunzi?

[HASHTAG]#BringBackKingKiba[/HASHTAG]
 
ukimya wa Ali una stua, kwanza ana mwaka sasa hajatoa wimbo wowote mpya, ila mashabiki wake utakuta wana mwita king, king gani ana kuwa anatega hivi?, jamaa ni mvivu kiaina. mashabiki wengi wa AK wamejikuta wakishadadia heka heka za Harmorappa kwa sasa. Ali hawatendei haki watu wanao mkubali kwa kukaa kimya hivi
NB: sina timu
 
anakuja na mkakati maalumu wa kuhakikisha watu waliyomchukia diamond kisa bashite wanakuwa mashabiki wake
 
Bado anafuta mavumbi kwanza akimaliza ndio atakaa kwenye kiti.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom