nani anamiliki uchumi wa tz na nini athari zake? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

nani anamiliki uchumi wa tz na nini athari zake?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mharakati, Feb 6, 2012.

 1. m

  mharakati JF-Expert Member

  #1
  Feb 6, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  kuna swala moja nyeti la muundo wa uchumi na nani haswa wamiliki wakuu wa huo uchumi. Tukirudi shule kidogo kwenye elimu ya msingi ya sayansi ya siasa tunaambiwa dola na serikali vinazaliwa ili kusimamia uzalishaji na ugawaji wa matunda ya uzalishaji huo katika jamii yenye mgongano wa kimaslahi..Serikali inafuata au inakuja pale wazalishaji wanapokuepo na serikali inakua na kukomaa pale inapofanya kazi na kukuza huo uzalishaji. mfano ni uanzishwaji wa dola za kitaifa na serikali zenye nguvu za ulaya na marekani ilikuja baada ya mapinduzi ya viwanda na kuongezeka kwa uzalishaji na nguvu kubwa ya tabaka la wazalishaji lilozifanya jamii hizi kujizatiti zaidi katika utaifa wao.

  Hapa la msingi ni uzalishaji ambao mimi kwa kurahisiaha nitauita ni uchumi wenyewe wa taifa. Katika huu uzalishaji tabaka la wazalishaji litakua na nguvu kubwa katika kuhakikisha serikali inakua makini, (kwa sababu serikali isipokua makini uzalishaji unashuka na hili tabaka kuumia na jamii nzima kuumia). Vile vile hili tabaka lina nguvu kubwa ya ushawishi katika siasa na serikali na katika nchi nyingine hawa ndiyo wanasiasa wenyewe. Sasa kama hili tabaka au wengi au sehemu kubwa ya hili tabaka wana uchungu na nchi yao, basi la hasha nchi itapiga hatua za kimaendeleo na kama siyo hivyo basi tabaka litakua pale kuchuma tu.

  Sasa hapa Tanzania waendesha uchumi ni wahindi, wawekezaji uchwara na wanasiasa ambao kutokana na historia ya nchi yetu bado wamevaa majoho ya ujamaa. Wahindi ambao sina haja ya kusema wana uzalendo kiasi gani na taifa hili.(wahindi ni chuma popote, naishi popote) na hata kwao India tatizo kubwa linaloifanya India iendelee kuwa maskini huku ikiwa inaingiza hela nyingi ni tamaduni ya kudharau sheria na taratibu zilizowekwa hali ambayo inayochangia rushwa na ufisadi wa hali wa juu. Hawa wawekezaji ni wale wanaokuja kwa migongo ya wahindi na wanasiasa ambao mwisho wa siku taifa haliambulii kitu zaidi ya kuneemesha mifuko ya wachache.

  Wanasiasa mara nyingi uogopa kuonekana kua wanamiliki biashara kubwa kubwa kwani katika nchi maskini wanaopiga kura wengi ni maskini na wanaogopa kuonekana kua ni wezi wa mali za umma, (kwa sababu vipato vyao halali haviruhusu kua matajiri wakubwa haswa haswa kwenye nchi maskini kama Tz).

  Ukiangalia hili tabaka sasa utakuta kwa sababu moja au nyingine halina nia thabiti ya kuendeleza nchi au kuboresha serikali na taasisi zake kwa sababu kama tulivyoona hapo juu hawa wafanayabiashara/wawekezaji pamoja na nguvu yao lakini hawana uchungu na nchi hii ni kama wapita njia na hivyo wanatumia nguvu yao ya ushawishi kuwaingiza wanasiasa wetu (ambao wengi wao wametokea katika familia za hali ya chini kidogo) katika mtandao wa uchumaji tumbo huku maslahi binafsi yakiwa juu kuliko ya taifa na hapa tunapata serikali isiyosikiliza wananchi wake inayotawalia na kutokua na uzalendo wa kweli wa kulikomboa taifa na maendeleo duni.

  Tanzania tuna kila sababu ya kuendelea kiuchumi (rasilimali zetu, na amani iliyopo) ila kama nguvu za ziada hazitatumika kutengeneza tabaka la wamiliki uchumi wenye uzalendo tutabakia kuwa taifa la walalamikaji huku tukisubiri tabaka hili lituonee huruma, litosheke, au lianze kulipuana lenyewe kwa lenyewe ili tuweze kujivunia nchi yetu.


  Nb:ningependa kusema kwamba hili tabaka siyo kwamba wawekezaji wote, wahindi wote au wanasiasa wote siyo wazalendo ila wengi wao wako hivyo... nafikiri ilikua ni muhimu kugusia msingi wa kutengenezwa au kukomaa/kujizatiti kwa tabaka hili kumekuja baada ya uanzishwaji wa biashara huria 1985 kutokana na presha iliyokuepo toka benki ya dunia na IMF. Sina uhakika kama serikali ya enzi hizo ingeweza kuchukulia hili zoezi taratibu ili kuwapa nafasi wazawa kumiliki uchumi wao.
   
Loading...