macho_mdiliko
JF-Expert Member
- Mar 10, 2008
- 21,688
- 39,369
Baadhi ya shule za chekechea zinazomilikiwa na madhehebu ya dini ni hatari. Wanachapa vikoko ni balaa. Nilimpeleka wa kwangu ana miaka minne tu shule ya kikatoliki wanafundisha masista. Alikuwa analia shuleni kila siku mpaka wakasema tumchukuwe. Viboko na kufinya na yeye ni mwoga. BTW niwatahadharishe watu msiangalie tu matokeo mazuri ya mitihani. Siku hizi kuna shule wanafanya kila iwezekavyo ili tu wapasishe na shule zipate soko. Kufaulu mtihani siyo kuelimika! Ni fedha tu zinazokosekana lakini shule kama Tanganyika International School ndiyo hutowa elimu na wanafunzi wamaliza wanakuwa wameelimika kiukweli.Ngoja nikahamishe katoto kangu kakaingie chekechea hapo maana kule kalipo usanii mwingi. Nilidhani wasabato wenzangu wanathamini thamani ya mtoto ila sio km nilivyodhani. Hali hatarishi uangalizi mdogo. Mchungaji utanisamehe boresheni mazingira ya shule zetu.