Nani analeta foleni barabarani: Polisi, taa za kuongoza au mzunguko (round about)

Mama Mdogo

JF-Expert Member
Nov 21, 2007
2,961
2,138
Katika mihangaiko yangu katika nchi mbalimbali na hapa nchini, nimeona kwa wenzetu walioendelea magari barabarani yanaongozwa na taa (traffic lights, robots) na hawana roundabout nyingi ila wana interchanges na flyovers nyingi. Hapa nchini kwetu tuna taa za barabarani, traffic police na round about hasa katika majiji.

Sasa najikita katika barabarani za jiji la Dar. Barabarani ya Bagamoyo ina traffic lights nyingi kuanzia Tegeta hadi Mwenge. Barabara ya Mwai Kibaki haina taa ina round about Mona ya Africana na Kawe. Barabara ya Morogoro ina taa pale Bucha na Kibo na round about pale ubungo. Baada ya kuondolewa trafic police pale ubungo na kuacha taa zitawale pale Bucha na Kibo, foleni Han na tena, na foleni imepotea. Kule barabarani ya Bagamoyo na Mwai Kibaki trafic police wanatawala na taa hazitumiwi tena hasa asubuhi na jioni. Matokeo yake kuna foleni ya kufa mtu. Rekodi ya foleni zote inaletwa na polisi wanaoongoza magari barabarani ya Mwai Kibaki, ni shida!!!!

Narudi katika swali la msingi, nani analeta foleni barabarani: polisi traffic, taa za kuongoza au mzunguko (round about)?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
polisi traffic ( wanaelewemewa na kazi na kuchoka, huwa wanapoteza umakini wanakuwa bora liende ) na taa za kuongoza ( wameziweka karibu karibu sana, na hazipo sawa na teknlojia zinashindwa hata ku sense ni upande upi una foleni kubwa na kuruhusu, ilivyo fanyiwa setup ndio hivyo hivyo, hazina uwezo wa kuchange kutokana na mazingira ) ... ndio majipu hayo.... :D:D:D:D
 
Back
Top Bottom