Nani analea ufisadi kati ya CHADEMA na CCM?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,113
33,623
Vyama vikubwa vya siasa hapa nchini CHADEMA na CCM kwa nyakati tofauti huwa vinaonesha kwamba vinachukia sana ufisadi. Lakini kila wakati vyama hivi vimekuwa vikitupiana mpira kuhusu kutamalaki kwa ufisadi kwenye nchi yetu.

CCM huwa inawashutumu CHADEMA kuwa kuwapokea "mafisadi" wanaotoka kwenye chama hicho na CHADEMA nayo inawashutumu CCM kwa kuzalisha "mafisadi" wanaoliangamiza taifa.

Lakini inavoonekana ni kwamba CHADEMA na CCM inawajua hao "mafisadi" kwa undani sana ama kinagaubaga. Sisi kama taifa tusiishie kusema fulani na fulani ni "mafisadi" bali ni lazima tulazimishe hao "mafisadi" wachukuliwe hatua.

Lakini inavoonekana kati ya wazalisha "mafisadi" (CCM) na wapokea "mafisadi" (CHADEMA) lazima kati yao wapo ambao wanaulea na kuulinda ufisadi. Ili kumalizana na ufisadi kwenye nchi yetu ni lazima kwanza tupambane na walinda "mafisadi".

Lazima tujiulize ni kwa nini mafisadi hawashitakiwi badala yake tunaishia kusikia CHADEMA na CCM wakiishia kurushiana vijembe majukwaani? Mwenyekiti wa CCM Taifa anasema kwamba "majizi" na "mafisadi" wanakimbilia CHADEMA. Lakini yeye si Rais wa nchi ni kwa nini hawachukulii hatua huko huko CHADEMA walikokimbilia hao "majizi" na "Mafisadi"?

Ni lazima tujue ni nani anawalinda mafisadi kati ya vyama hivi viwili !!
 
Sisi CCM hatuna utaratibu wa kuitana fisadi hata kama mtu ameibia nchi kwa kiwango cha DIVISION ONE na hatunaga utaratibu wa kuwajibishana kabisa.Mara nyingi saana huwa tunasubiri ikitokea mtu amehama chama chetu ndo tunaanza kumnanga.
 
Iko wazi CCM ni kichaka kama sio pori la kila aina ya ufisadi na ubadhilifu wa mali za umma.......

Na ndio maana wawakilishi wa wananchi wanyonge(wabunge) wana jitahidi kwa kila hali kuyaibua majizi kwenye hicho kichaka au pori kwa tuhuma tunazoambiwa kuwa ni za uhakika......

CCM kwa kuleana kwao wanashindwa kuwawajibisha hao wezi ambao ushahidi wao hauna shaka......

Lakini jambo la ajabu na la kumshangaza kila mwenye akili timamu ni kuwa mafisadi hao hao kutoka kwenye pori hilo wanakimbilia upande wa pili wa pori la tunaowaita wakombozi.....mara tu wanapoingia wanaitwa watakatifu na wasio na dhambi......tena tunaambiwa mwenye ushahidi wa wizi huo au ufisadi wao wapeleke mahakamani..........

7e1f91bdfd7db2b332afd62d2f6f0561.jpg
 
Nionavyo mimi CCM ni mtambo wa kufyatua Mafsadi. Wanazaliwa huko, wanakulia huko na kuota huko. wawako huko huwa salama na huendeleaa kuzaliana na kuzaliana.
Itokeapo wkawa wameisha tamalaki na Ufisadi wao na wao kama binadamu huhitaji mazingira yasiyolea na kutunza ufisadi hivyo hutafuta pakwenda na kutengeneza toba ya kuokoka dhambi zao za ufisadi nako si pengine bali ni CHADEMA.
 
Na sisi huku upinzani hata akihamia shetani kuanzia muda huo anaotangaza kuhamia kwetu anakuwa malaika na hautakiwi kumsema au kuhoji matendo yake ya nyuma kwani utaonekana ni adui wa harakati za kuiondoa CCM madarakani......

Sisi huku lengo letu ni CCM kuondoka madarakani hata kama kiongozi wa mbio hizo ni shetani....bali kinachotakiwa tu CCM waondoke alafu mambo MENGINE yatajulikana baadae......
 
Nionavyo mimi CCM ni mtambo wa kufyatua Mafsadi. Wanazaliwa huko, wanakulia huko na kuota huko. wawako huko huwa salama na huendeleaa kuzaliana na kuzaliana.
Itokeapo wkawa wameisha tamalaki na Ufisadi wao na wao kama binadamu huhitaji mazingira yasiyolea na kutunza ufisadi hivyo hutafuta pakwenda na kutengeneza toba ya kuokoka dhambi zao za ufisadi nako si pengine bali ni CHADEMA.

Nani kawapa mamlaka ya kusamehe wezi CHADEMA...!!?
 
Mleta hoja, ukweli mnauona halafu mnaanza kuzunguka mbuyu?! Chama chenye madaraka yote ni kipi?! Tena wakuu wa vyombo vyote vya dola, wanateuliwa na mwenyekiti wa chama hicho!! Na kawaida wanapokea maagizo kutoka juu . Halafu unakuja kuuliza swali la chekechea hapa!!!

CCM kabla ya Lowassa kuhamia CDM ni lini walitamka wazi kuwa wanauchukia ufisadi?! Kila lilipoibuliwa ufisadi, walitetea kupitia wasemaji wa serikali au mkuu wa nchi kabisa. Sasa leo unaleta swali la kitoto hapa?! Nakumbuka lilipoibuliwa ufisadi jeshini, jamaa mara moja aliperekwa ubalozini!!

Kosa la chadema ni kutaka ushindi kwa gharama zozote, hata kama njia hiyo inakichafua chama!!
 
Iko wazi CCM ni kichaka kama sio pori la kila aina ya ufisadi na ubadhilifu wa mali za umma.......

Na ndio maana wawakilishi wa wananchi wanyonge(wabunge) wana jitahidi kwa kila hali kuyaibua majizi kwenye hicho kichaka au pori kwa tuhuma tunazoambiwa kuwa ni za uhakika......

CCM kwa kuleana kwao wanashindwa kuwawajibisha hao wezi ambao ushahidi wao hauna shaka......

Lakini jambo la ajabu na la kumshangaza kila mwenye akili timamu ni kuwa mafisadi hao hao kutoka kwenye pori hilo wanakimbilia upande wa pili wa pori la tunaowaita wakombozi.....mara tu wanapoingia wanaitwa watakatifu na wasio na dhambi......tena tunaambiwa mwenye ushahidi wa wizi huo au ufisadi wao wapeleke mahakamani..........

7e1f91bdfd7db2b332afd62d2f6f0561.jpg
umeishiwa hoja kama mbowe
 
Nionavyo mimi CCM ni mtambo wa kufyatua Mafsadi. Wanazaliwa huko, wanakulia huko na kuota huko. wawako huko huwa salama na huendeleaa kuzaliana na kuzaliana.
Itokeapo wkawa wameisha tamalaki na Ufisadi wao na wao kama binadamu huhitaji mazingira yasiyolea na kutunza ufisadi hivyo hutafuta pakwenda na kutengeneza toba ya kuokoka dhambi zao za ufisadi nako si pengine bali ni CHADEMA.
tuichambuwe chadomo, Mbowe mkwepa kodi, lema mwizi wa magari, lisu kibaraka wa ACCACIA, nyalandu kibaraka wa USA na makampuni ya utarii ya kimarekani, Lowasa Richmonduli, nani amebaki, malizia,

ruzuku milioni 300 kila mwezi za chadomo zinaenda wapi, ofisi hakuna
 
Unadhani kutajataja majina kunasaidia? Tunataka kujua ni kwa nini mafisadi hawapelekwi mahakamani? Ni nani anayewalinda na kulea ufisadi huu!?
 
wataje hao mafisadi hambao hawajapelekwa mahakamani, na wako wapi, na walifisadi nini???
hacha majungu, mhasibu TAKUKURU amefunguliwa kesi, wakurugenzi wa tegeta Escrow wako mahabusu, mkurugenzi wa tanesco anakesi ya kujibu, wewe unataka nani apelekwe ulidhike????
 
Vyama vikubwa vya siasa hapa nchini CHADEMA na CCM kwa nyakati tofauti huwa vinaonesha kwamba vinachukia sana ufisadi. Lakini kila wakati vyama hivi vimekuwa vikitupiana mpira kuhusu kutamalaki kwa ufisadi kwenye nchi yetu.

CCM huwa inawashutumu CHADEMA kuwa kuwapokea "mafisadi" wanaotoka kwenye chama hicho na CHADEMA nayo inawashutumu CCM kwa kuzalisha "mafisadi" wanaoliangamiza taifa.

Lakini inavoonekana ni kwamba CHADEMA na CCM inawajua hao "mafisadi" kwa undani sana ama kinagaubaga. Sisi kama taifa tusiishie kusema fulani na fulani ni "mafisadi" bali ni lazima tulazimishe hao "mafisadi" wachukuliwe hatua.

Lakini inavoonekana kati ya wazalisha "mafisadi" (CCM) na wapokea "mafisadi" (CHADEMA) lazima kati yao wapo ambao wanaulea na kuulinda ufisadi. Ili kumalizana na ufisadi kwenye nchi yetu ni lazima kwanza tupambane na walinda "mafisadi".

Lazima tujiulize ni kwa nini mafisadi hawashitakiwi badala yake tunaishia kusikia CHADEMA na CCM wakiishia kurushiana vijembe majukwaani? Mwenyekiti wa CCM Taifa anasema kwamba "majizi" na "mafisadi" wanakimbilia CHADEMA. Lakini yeye si Rais wa nchi ni kwa nini hawachukulii hatua huko huko CHADEMA walikokimbilia hao "majizi" na "Mafisadi"?

Ni lazima tujue ni nani anawalinda mafisadi kati ya vyama hivi viwili !!
hacha unafiki kama lisuuu, wataje hao mafisadi, na walicho fisadi
 
Majiz na mafisadi wakija chadema sirikali haiwez wakamata ndio maana ccm wanalialia tu kwenye majukwaa ya siasa.Wanamaanisha chadema ina power zaidi yao hapo hapo wanasema tena chadema inakufa imepoteza mwelekeopyuu pyuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom