Nani anakumbuka Hotuba ya JK alipolihutubia Bunge 2006?

ashakum

Member
Apr 25, 2012
24
4
JK aliwachimba mkwala wenzake pale bungeni. Alisema yeye pamoja na kuwa ana sura ya tabasamu lakini ni mkali kwenye mambo ya msingi. Mbona hawi mkali na pesa ya walalahoi inayoliwa na serikali anayoiongoza? Ameshindwa hata kuwawajibisha mawaziri ambao bunge limeshafanya kazi kubwa ya kueleza sababu? Nipeni michango yenu kwa kuanzia na ile hotuba yake kwenye nukuu ya "I might be wearing a smiling face, but I am firm on issues"
 
Sioni kosa la mtoto wa mkulima kama bosi kubwa mwenyewe yuko kimya na jambo kubwa kama hilo. Sasa tunamuona JK halisi, sio yule wa kwenye kampeni, yule wa maisha bora kwa kila Mtanzania, wanawake watawezeshwa! Mawaziri hawatajiuzulu maana bosi kubwa hana mpango wa kuwawajibisha.
 
JK aliwachimba mkwala wenzake pale bungeni. Alisema yeye pamoja na kuwa ana sura ya tabasamu lakini ni mkali kwenye mambo ya msingi. Mbona hawi mkali na pesa ya walalahoi inayoliwa na serikali anayoiongoza? Ameshindwa hata kuwawajibisha mawaziri ambao bunge limeshafanya kazi kubwa ya kueleza sababu? Nipeni michango yenu kwa kuanzia na ile hotuba yake kwenye nukuu ya "I might be wearing a smiling face, but I am firm on issues"

Ilikuwa hotoba nzuri sana iliyokuwa imejaa matumaini baada ya awamu ya mzee mkapa kuboronga,kutokana na watendaji na wasaidizi wa Jk kumuangusha hali imekuwa tofauti
 
Back
Top Bottom