Nani anaiua CUF je ni CCM, viongozi wenyewe wa CUF au wananchi au muda wake umefika? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani anaiua CUF je ni CCM, viongozi wenyewe wa CUF au wananchi au muda wake umefika?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Iron Lady, Mar 2, 2012.

 1. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #1
  Mar 2, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,077
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  CUF kilikuwa chama chenye nguvu sana nchini tanzania.watu walikikubali wengi walijiunga nacho na wale ambao hawakujiunga walikubali nguvu iliyokuwa nayo CUF tena kilikuwa chama chenye uongozi imara. damu nyingi imemwagika kukipigania chama hicho haswa zanzibar. 2011-1-2012 tumekuwa tukisikia migogoro mingi ndani ya CUF, lakini pia pale CUF ilipoungana na CCM kule Zanzibar ule ngangali wa CUF ukapotea ghafla na wananchi pia wakasikika wakilalamika kuwa viongozi wao hawawajali tena bali kutekeleza ilani ya CCM. sasa viongozi wanajitoa wanachama wanajitoa chama si chama tena ila imekuwa vurugu tupu CUF hiyoooooooooooooooo inakufa taratibu na hakuna wa kuonesha kuisimamia isiondoke viongozi wake waasisi wenye uchungu na chama hiki wako wapi? au ndio wamenamazishwa au siku hizi uzalendo na chama hichi haupo tena au wameshapata walichokuwa wanatafuta?
  jukwaa hili laweza changanua mambo kwa kina kujua haswa nani aliyoiua CUF kwa data mbalimbali pasi shaka yaweza kuwa msaada kwa vyama vingine .
   
 2. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #2
  Mar 2, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  ndoa yao na ccm haikuzingatia maslahi ya wanachama bali viongozi wachache waroho wa madaraka.
   
 3. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Mbona umeleta thread ya kupotosha watu? CUF haijafa ila imemeguka vipande viwili na kupoteza mwelekeo ndiyo maana bado inatambuliwa kwa msajili wa vyama.
   
 4. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #4
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,859
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Maalim Seif kwa tamaa ya madaraka na ndio maana akakubali haraka haraka matoke ya uchaguzi uliopita ili tu apate umakam wa rais feki, sasa ndio wanavuna walichopanda.
   
 5. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #5
  Mar 2, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  NJAA ndio imeiua CUF kifo cha Mende...
   
 6. M

  Marytina JF-Expert Member

  #6
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Wanainchi wasilaumiwe kwa kifo cha cuf

  timu ikifungwa kocha mbovu, kampuni ikiyumba meneja bovu so jibu umeshapata
   
 7. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #7
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Ndoa ile ndo imeiua CUF watake wasitake ndo maana wanatimuana
   
 8. Nicas Mtei

  Nicas Mtei JF-Expert Member

  #8
  Mar 2, 2012
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 11,569
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Unaa umeimega CUF
   
 9. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #9
  Mar 2, 2012
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,419
  Likes Received: 3,757
  Trophy Points: 280
  HAMAD ndo aniuwa CUF
   
 10. M

  Molemo JF-Expert Member

  #10
  Mar 2, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Kinachoipeleka kaburini CUF ni kauli za hovyo za viongozi wake.Mfano wa karibuni ni pale kiongozi wake Ismail Jussa alipotoa kauli rasmi ya chama kuwa CUF ilishindwa jimbo la Uzini kwa sababu ya Ukristo na Ubara.Ni mtanzania gani anayependa kauli za kibaguzi hivi?
   
 11. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #11
  Mar 2, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Heshima kwako Iron Lady,

  Kwanza naomba nikusahihishe kidogo CUF bado haijafa bali kimepoteza uelekeo.

  Kuna sababu kadhaa zilizo sababisha CUF kufikia hapo ilipo.

  [1] Viongozi wa CUF hasa Maalim Seif Shariff na Jussa waliweka mbele uZanzibar kuliko uTanzania.Hii liliongelewa sana na Bwana Rwakatare naibu katibu mkuu [T] kabla hajakimbia chama hicho kutokana na mizengwe aliyofanyiwa na Maalim na kundi lake haramu.Uwekezaji wa rasilima hasa mgawo wa fedha za ruzuku za chama ulielemea Pemba zaidi kuliko Tanzania bara.Mfano bajeti ya uchaguzi wa Rais wa Zanzibar Maalimu alichotewa zaidi ya 200 milioni huku Prof Lipumba akiambulia 70 milioni.Ukiitzama hiyo bajeti utagundua kwamba Zanzibar yenye eneo dogo na idadi ya wapiga kura wachache walipendelewa kupita kiasi huku Prof Lipumba akiachwa kama mtoto yatima na bajeti ndogo ilimwezesha kutembelea maeneo machache sana ya Tanzania bara kama ukanda wa Pwani pekee yake.

  [2] Maalimu baada ya kushindwa mara nne katika uchaguzi wa Zanzibar aliaamua kukizika chama chake kwa kuongwa nafasi ya umakamu wa Rais wa Zanzibar nafasi ambayo kazi yake kubwa ni fitina na kupambana na madawa ya kulevya kazi ambazo zinazofanywa na polisi chini ya uongozi wa wizara ya mambo ya ndani.

  [3] Maalimu pia alikuwa na ajenda nyingine isiyofahamika rasmi UDINI na Uzanzibar.Kwakuwa Zanzibar ina Idadi kubwa ya waIslam huku Tanzania bara ikiwa na idadi inayolingana baina ya wakristo na waIslam Maalim alianzisha mkakati wa siri wa kukifanya CUF chama kinachopendelea sera za kubagua wakristo na kuenzi uIslam ili kujipatia uungwaji mkono zaidi huko Zanzibar.Sera hii bahati mbaya imezidi kukitenga CUF na waTanganyika.

  [4] Maalimu alikuwa na tamaa ya ving'oora kavipata kakisahau chama chake na wanachama wake ambao wengine walipoteza maisha,wengine waligeuka wakimbizi,wangine walibakwa,wengine walifilisika na wengine walifungwa jela.Maalimu Seif kageuka Mtume anachosema yeye hakihojiwi wala kukosolewa.
   
 12. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #12
  Mar 2, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,077
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  inategemea maana yako ya neno kifo kama ilivyotumika hapo. lakini mimi kwangu naona imekufa. CUF hii siyo ile tuliyokuwa tunaijua na kuisikia iliyokuwa inaogopwa na ccm na kumkosesha CCM usingizi kila leo.
  leongo la kuleta thread hii ni kujaribu kuamsha mjadala wenye kutafuta kiini cha tatizo la CUF kuwa hivi ilivyo.na sio kuangalia kwa juu juu.naamini humu kuna watu wazuri wa tafakari wenye data za kutosha kuweza kuleta mjadala wenye manufaa kwa wengine siku za usoni.
   
 13. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #13
  Mar 2, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,077
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  maalimu seif mbona hasikiki? na kama kasikika kasema nini? siku hizi hana tena uchungu na chama? narudia au kapata alichotaka?
   
 14. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #14
  Mar 2, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Mkuu Iron Lady. Matatizo ya CUF yamejikita ktk malengo ya kuanzishwa kwake ambayo yalikua ni kuchukua madaraka ya dola huko Zanzibar. Walikuja Tanganyika kwasababu ya kutimiza masharti ya kupata usajili. Ninashangaa ninaposikia eti wanachama wao upande wa huku Bara wakilalamika kubaguliwa sasa! Ingawa ugomvi kati ya Maalim na HR ulikwisha anza kabla ya uchaguzi mkuu wa 2010 lakini sasa umekolezwa baada ya HR kukosa ukuu wa kambi ya upinzani Bungeni. Mnakumbuka jitihada kubwa alizofanya ili kuiengua CDM ili aongoze kambi ya upinzani. Kwa hiyo aliungana na wenzake walikosa nafasi ktk SUK wakaanzisha uhasi ambao sasa tunaona umefika mpaka bara.
   
 15. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #15
  Mar 2, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,077
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  dadavua ndugu yangu.kivipi hamad ndiyo anayeiua CUF?
   
 16. M

  Mr.Busta JF-Expert Member

  #16
  Mar 2, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 672
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
   
 17. U

  ULIMWAKI Member

  #17
  Mar 2, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kuwa CDM mshauri wake mkuu ni Kadinali Pengo ngoja tuone hatma yake nacho...2015 si mbali.
   
 18. M

  Mr.Busta JF-Expert Member

  #18
  Mar 2, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 672
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  JUSSA nafikiri kaiua Cuf baada ya kuchaguliwa kuwa Mbunge.kwan mawazo ya Hamad yalianza kupuuzwa.mawazo tu.
   
 19. M

  Molemo JF-Expert Member

  #19
  Mar 2, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  CDM inahusikaje na kifo cha CUF?
   
 20. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #20
  Mar 2, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Wenzenu tunaojua siasa tuling'amua zamaaani kuwa CUF imefika ukomo. Wanasiasa huwa wanapenda madaraka si wananchi ambao huwa nyuma yao na wengine kufa kwa ajili yao. Kumbukumbu zinaonyesha kwamba Komandoo alimnyang'anya Maalim Seff haki zake za Waziri Kiongozi mstaafu kisha ukaja muafaka Maalim akarudishiwa haki zake; akapoa. Umekuja huu muafaka na Maalim amepata Umakamo wa Rais; Mungu ampe nini wakati huu ambao ni jioni kwake na bila shaka akitoka hapo atarudi Pemba kupumzika na kula kwa raha hadi siku ambayo Mungu wake atamvuna.Mission accomplished hata CUF ikifa wacha ife malengo ya mwenye Chama yametimizwa. Ninyi wafuasi shauri yenu mtajiju. Madaraka jamani matamu nyie acheni tu.
   
Loading...