Nani anaiongoza CCM?

Kuhani

JF-Expert Member
Apr 2, 2008
2,944
1,195
...mimi ni mkazi wa kijiji cha Kinyerezi, nimezungukwa na high profiles politicains wa zamani na wa sasa ninawaona waliokuwa wazuri na wabovu kwa sababu you can tell kutokana na life style zao, mmoja wa majirani zangu wa karibu sana ni Mzee Apiyo na Mahita, you can tell kwamba Mzee apiyo alikuwa ni kiongozi safi, masikini ya Mungu hana kitu kabisaa, lakini ninawangalia majirani zangu wengine kama Mahita.

...sasa hatuwezi kuwatukana viongozi wetu wote kwa sababu ya wezi wachache

Kwamba kiongozi ambae hakuiba ndio kiongozi safi hilo sidhani ni kweli. Kutokuiba, unategemewa usiibe, si sifa. Kutokuiba yabidi kuwe the least common denominator. Zaidi ya maadili, tupime viongozi kwa ufanisi, maono uzoefu, matokeo, fikra, kujitoa katika utumishi, na uchochezi chanya, na pia kutovumilia maovu. Field Marshall ni muadilifu, msafi, sawa, je alifanya nini alipoona uchafu? Ana balls za kukemea maovu?

Na uadilifu wenyewe tusiupime kwa kuangalia "life styles" za wastaafu. Hao unaosema majirani zako wastaafu wasafi wa Kinyerezi, wametangaza mali zao zote Tume ya Maadili? Ni vigumu kujua. Utawezaje kujua mali na vipato vya Kingozi wa Tanzania wakati hata mshahara wa Rais ni siri kali ya serikali?
 
Field Marshall ES

JF-Expert Member
Apr 27, 2006
12,665
0

- Ndio maana tunasema kwamba vijana mkazane sana ili kuwa samba samba ya kinachoendela bongo, kwani tatizo laetu sasa hivi bongo ni viongozi wezi ambao ndio mafisadi, ukiondoa haya mawili bongo sasa hivi, maana yake utakuwa una-itroduce utawala wa kuheshimu sheria, ukiliweza hili tu basi mengine yote unayoyasema yata-fall into their place.

FMES!
 
Renegade

JF-Expert Member
Mar 18, 2009
6,276
2,000
I seriously respect your view, lakini naomba nikuulize kwa nini umeng'ang'ania kubaki ndani ya chama wakati uongozi wa juu mzima wa CCM hivi sasa ni wanamtandao? They are ineffective na walikuwa part and parcel of one of the most corrupt and sleazy campaign in the history of Tanzania.

MKUU
UNAJUAJE KAMA FMES siyo mmoja wao hao uliowataja hapo juu?
Ngoja nikukumbushe, wakiwa kwenye majukwaa na maeneo yao ya kujidai wanawakemea mafisadi,lakini waulize waseme ni nani kati yao? kila mtu hamjui nani ni fisadi kati yao!!! inawezekana kweli? Maneno mazuri ndiyo silaha yao ,je unakumbuka ile slogan ya "HARI MPYA ,NGUVU MPYA NA KASI MPYA? iko wapi ni NGUVU YA GESI, NI KASI YA KINYONGA? HARI YA GONJWA?
MAJIBU UNAYO MKUU ,FMES .MKIONGEA LUGHA NI NZURI KWENYE VITENDO NI UBADHIRIFU.
 
- Walifanya kampeni za kisasa ambao wa-Tanzania tulikuwa wageni nazo, lakini ndio kampeni za kisasa hatutarudi tena kwenye kampeni za mtu na giza zile zimepita done! Hata kwenye general elections za 2005 wapinzani pia walifanya kampeni chafu. Tatizo sasa sio mbinu za kampeni zilizopita, ila wanafanya nini kwenye utawala sio siri kwamba hawafanyi vizuri sana sasa ni wajibu wetu kuonyesha wapi wanakosea, mimi siku zote ninapowashambulia watawala huwa ninashambulia kwa facts na specificity.

- Nipo CCM kwa sababu ninaamini kwamba ni chama kizuri, kimenilea toka nikiwa mdogo, kimenisomesha ndani na nje ya nchi, sasa wajibu wangu kukilipa back na hasa taifa langu, ninaamini ninaweza kukisaidia nikiwa ndani yake na sio kwa nje, lakini sina tatizo na wanaojaribu kwa nje kama wewe, kwa sababu lengo letu ni moja nalo ni mabadiliko ya kulisaidia taifa letu litoke lilipo sasa na kusogea mbele, ila tofauti yangu na wewe ni moja tu nayo ni mimi ninajaribu kuwa realistic.

Mkuu ninaheshimu sana post yako kwa sababu ni ya kistaarabu sana na una some strong points.

FMES!
 
Field Marshall ES

JF-Expert Member
Apr 27, 2006
12,665
0
Kwa kuwa kuna wanaofaidika na hali hii sasa ni wakati muafaka wa kuwakataa na haya maghala ni lazima yachomwe moto. Kwa kuwa maghala yanalindwa usiku na mchana, hawa walinzi wa maghala haya ya kifisadi lazima tuanze nao kwa kuwachoma moto.

- Mkuu Chonde chonde, hii lugha ni nzito mno kwa taifa letu.

FMES!
 
Madela Wa- Madilu

JF-Expert Member
Mar 24, 2007
3,065
1,195
CCM inaongozwa na MH Rostam Aziz Mbunge wa jimbo la Igunga chini ya mshauri mkuu wa Mambo ya Siasa na Uchumi MH Lowassa Mbunge wa Richmonduli.Rostam anaiongoza CCM kwa uhakika wa hali ya juu kwa kutumia Remote Control yake ya kitita cha Noti ambayo ni wana CC wachache sana wawezao kufurukuta mbele ya Remote hiyo.

Rais Kikwete ni Boya.
Wabunge wa CCM ni mihuri.
Wanachama wa CCM ni magharasha( Karata zisizo na thamani)
Chochote atakacho MH huyu hufanyika kwa nguvu ya Remote yake.

Remote ile si yake,wenyenayo wanajua kwamba si yake lakini wamempa uwezo wa kuitumia ili nao wapate kufaidi. Wanamlinda usiku na mchana kwa sababu taabu na mashaka yao ni juu ya remote ile na si mwenye uwezo wa kuitumia.
Wengi wataangamia na mahali pao patatoweka, hata wale wasiofaidika na matumizi ya Remote ile, kama muda apewao Rostamu kuitumia Remote ile hautafupishwa.

Bisha!
 
Last edited:

Mkandara

JF-Expert Member
Mar 3, 2006
15,535
2,000
FMES,
heshima mkuu unajua... najuuuta kukufahamu maanake haya maneno yako huwa mazito sana. Binafsi ynayapokea kwa mikono yote na hakika Taifa letu litakombolewa na mapambano ndani ya chama na nje.. hata vitani siku zote mapambano hufanywa toka nje lakini pia Upinzani ndani huyasaidia majeshi ya nje, lengo kubwa ni kuwashinda maadui..Maadui wetu sote sii chama, ninaamini kabisa maadui wangu ni maadui wa mwanachama yeyote wa CCM ambaye kashikwa pabaya!..
Ndio maana huko nyuma nimesema CCM ina cancer mkuu wangu sikuwa natukana ama kuwajuza ila ni ukweli ambao hadi mtakapo kubali kuwa chama kimekosa mwelekeo na sasa hivi mafisadi (virus) ndio wanakipeleka mputa.mtakujja jutia na pengine kuliweka taifa mahala pabaya zaidi..

Kuna kila alama mkuu wangu kila dalili za kuonyesha kwamba chama kinapoteza maadili yake..
Kibaya tu ni pale unapojaribu kuweka list ya vyama pinzani kuonyesha sijui kitu gani?..
Uongozi bora hautokani na mtu mmoja na kama ingewezekana hivyo basi kina Stalin na Mao Tse Tung wangekuwa wabora zaidi kuliko viongozi wote duniani kwa sababu ndio walikuwa sauti ya chama kizima....wako wapi?..
Uongozi bora unatokana na team work..toka kina W. Churchill, Trudeau, A. Lincon hadi leo hii jaluo Idi Kanye - Obama, kachukua Taifa kubwa..nani kati yetu aliweza kumlinganisha na list ya viongozi wanaofaa kwa macho na fikira pevu...
Mbowe na Chadema ni mbora mara 100 kuliko CCM chini ya Mafisadi, hauhitaji kufikiria hilo hata kidogo.
 
Field Marshall ES

JF-Expert Member
Apr 27, 2006
12,665
0
CCM inaongozwa na MH Rostam Aziz Mbunge wa jimbo la Igunga chini ya mshauri mkuu wa Mambo ya Siasa na Uchumi MH Lowassa Mbunge wa Richmonduli.Rostam anaiongoza CCM kwa uhakika wa hali ya juu kwa kutumia Remote Control yake ya kitita cha Noti ambayo ni wana CC wachache sana wawezao kufurukuta mbele ya Remote hiyo.

Rais Kikwete ni Boya.
Wabunge wa CCM ni mihuri.
Wanachama wa CCM ni magharasha( Katata zisizo na thamani)
Chochote atakacho MH huyu hufanyika kwa nguvu ya Remote yake.

Remote ile si yake,wenyenayo wanajua kwamba si yake lakini wamempa uwezo wa kuitumia ili nao wapate kufaidi. Wanamlinda usiku na mchana kwa sababu taabu na mashaka yao ni juu ya remote ile na si mwenye uwezo wa kuitumia.
Wengi wataangamia na mahali pao patatoweka, hata wale wasiofaidika na matumizi ya Remote ile, kama muda apewao Rostamu kuitumia Remote ile hautafupishwa.

Bisha!

- Sikujua kwamba Rostam kuwa rais wa jamhuri, alichaguliwa na wanachama wa CCM peke yao na sio na taifa zima, Wapinzani included.

FMEs!
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,834
2,000
wanafalsafa hawawi wafalme!

Maneno yako ni kweli. Prof. Issa Shivji aliwahikuandika mahali, kuna wanasiasa, wanaopenda siasa lakini hawapendi uongozi. na kuna viongozi wa siasa, wanafanya siasa lakini hawapendi siasa bali wanapenda madaraka. Nakumbuka pia nilikutahadhariha MMKJ jihadhari na ma-opportunist kwenye foleni ya kutafuta ulaji 2010 kwa kisingizio cha kutafuta uongozi.
 
Karandinga

Member
Jun 25, 2008
66
0
Katika utaratibu wa kumsaidia mtu mlevi (kama aliyelewa madaraka) ujulikanao kama "Hatua 12). Hatua ya kwanza kabisa inamtaka mhusika kukubali kuwa ana tatizo na ya kuwa hakuweza kulikabili. NI hatua ya "kuown" your problem.

Hadi CCM itakapoanza hapa ndipo itaanza kweli kurudi kwenye misingi yake. NI vigumu sana kutoka denial kwenda acceptance. But slowly, watafika tu hata kwa kulazimishwa au kuanzishwa kauli.

"Hi, mimi ni mwana CCM, na Chama chetu kina matatizo!".

Wana CCM wote rudieni kauli hiyo hadi izame kwenye mitima yenu!

Hi my name is CCM and I'm leaderless.....Lol
 
Recta

JF-Expert Member
Dec 8, 2006
855
195
Mimi nadhani mjadala unaeleweka vizuri sana. Ila bado haujajibiwa kwa ufasaha.

Kwa maoni yangu, mtu mmoja mwenye uwezo (influence) anayoweza kuitumia kusimama kwenye hadhara na kusema au kukemea serikali au hata CCM ni John Samwel Malecela (kama ataamua kufanya hivyo). Wananchi watamsikiliza kama atasema na kusimamia yanayotakiwa kwa nyakati hizi.

Mzee huyu ana nguvu nyingi sana ndani na nje ya CCM. Ni mtu ambae amejijenga sana katika kipindi chote cha uongozi wa juu wa serikali na CCM. Ana support kubwa kutoka kwa wazee wengi na wenye kuheshimika nchini. Hana kitu kinachoweza kumfanya aogope kuchukua jukumu hilo. Tatizo ni kwamba hajaamua kuchukua jukumu hilo. Sababu zinaweza kuwa nyingi. Baadhi zimetajwa na FMES katika post zake ndani ya hii thread. Lakini pia (kwa maoni yangu) si mtu anaependa malumbano na viongozi walioko madarakani. Hili linaweza kuwa ndio chimbuko la yeye kutokuwa Rais wa TZ hivi sasa, ama kila anapokusudia kuomba ridhaa. Kwa maneno mengine, hajathubutu kuchukua jukumu hilo la kukemea serikali wala CCM.

Mzee Malecela ndie aliesimamia utungwaji wa Katiba ya JMT iliyopo hivi sasa nchini (baada ya kufanyiwa marekebishi makubwa sana 1992), ndie aliesimamia mabadiliko ya kisiasa nchini (kuruhusu upinzani katika siasa), ndie aliebadili mwelekeo wa siasa za nchi kiuchumi. Ni mtu anaeifahamu nchi kwa kina na zaidi anajua sana siasa za TZ na uongozi wake. Zipo sababu nyingi zilizomfanya akosane na watawala waliopita. Ila sababu zote hazijawahi kumdondosha na kumuacha hoi.

Matamanio yangu siku zote ni Mzee huyu kuchukua jukumu linalomsubiri la kuiondoa nchi hii katika utawala uliopotoka (kabla nguvu hazijamuishia). Hana la kupoteza katika umri alionao ambalo ni kubwa kiasi cha kumnyima usingizi.

Mzee huyu ni mmoja kati ya watu wenye busara nyingi sana kutokana na ujuzi wake pamoja na exposure aliyonayo. Lakini kubwa zaidi, huyu ni mtu mvumilivu kuliko mtu yeyote ninaeweza kumlinganisha nae. Amepoteza mengi lakini bado yuko imara.

FMES Mkuu, kama una ushawishi wowote kwa Mzee Malecela, nakuomba umuombe akomboe nchi hii, walau kwa kauli zinazokubalika tu. Najua ndani ya moyo wake anajua nini kinachotakiwa TZ. Naomba umueleze kuwa nchi imepotea njia, na taa ameishika mkononi. Mwambie asimamie watoto wake wanaopotelea msituni wasiangamie. Mwambie siku ya mwisho tutamlilia kama atatulinda kwa nguvu zake zilizobaki sasa (walau kama Mwalimu).
 
Jamco_Za

JF-Expert Member
Jul 14, 2007
1,330
1,225
nafikiri cha maana ni je akismama na kuwakaripia CCM watamsikiliza? kama watamsikiliza na yeye anaridhika na hii hari ya taifa kwa sasa? maana yeye anatakiwa hawe amekea matatizo yote unless na yeye anafaidika na huu ufisadi.

Kwa mawazo yangu nafikiri Mzee Malecela hakubaliki tena ndani ya chama kwani mvuto unatakiwa sasa ndani ya chama hana, CCM sasa hiviinahitaji watu wenye pesa na ndio maana kama pesa huna hauthaminiwi na yeyote, ndio maana wanashindana kurundika mapesa kwa ajiri ya kutetea nafasi zao katika chama.
 
Mkuu Jamco, ni kweli kwamba ni vyema kama mtu yeyote ambae atajitokeza kukemea yanayofanywa na viongozi wetu awe pia na uwezo wa kusikilizwa nao.

Ninavyojua ni kwamba, Mzee Malecela ni mtu anaesikilizwa sana na viongozi wetu. Uthibitisho wa hilo ni katika utegemezi uliopo katika kusaidia kwenye kampeni za uchaguzi mbalimbali (mfano Mbeya na sasa Busanda).

Kwa maoni yangu, mtu anaetakiwa kusimama na kusema, anatakiwa awe na uwezo wa kupanga kwa makini yale atakayoyasema. Wakusudiwa wakuu ni wananchi, ambao ndio wenye nguvu zaidi. Serikali na CCM pia, huhofia sana wanapoona mtu anatamka mambo yanayoweza kuwadhoofisha katika uchaguzi. Mzee huyu akisimama na kusema, serikali na CCM watalazimika kumsikiliza, na sia ajabu kutekeleza anayoyasema. Naamini hivyo kutokana na uwezo wake wa kushawishi kwa hoja zinazotokana na mpangilio wa maneno yake.
 
Rutunga M

JF-Expert Member
Mar 16, 2009
1,763
2,000
Wakuu
naomba mwenye maelezo yanayoweza kunisaidia anifaganulie ,Hivi kati ya wanasiasa hawa ni yupi anaweza kutamka neno kuhusu CCM tukalichukulia kama ndiyo CCM halisi bila kujali vyeo vyao ndani ya chama.

nauliza hivyo kutokana na kuchanganyikiwa baada ya kusikia matamko ya watu hao ambayo yamenixcha nikiwa kama kichaa bila kujua nichukue la nani.

nisaidieni jamani .
 
Masanilo

Platinum Member
Oct 2, 2007
22,291
1,250
All those are dead old woods! Enzi zao zimepita wameng'ang'ania madaraka. Ingekuwa vizuri wakapumzika nafasi zao zikashikwa na vijana wenye mitazamo ya karne hii. Binafsi huwa nawaona ni kama wapiga porojo no substance on their talks....!
 
Mr Kiroboto

JF-Expert Member
May 3, 2008
350
225
Wakuu
naomba mwenye maelezo yanayoweza kunisaidia anifaganulie ,Hivi kati ya wanasiasa hawa ni yupi anaweza kutamka neno kuhusu CCM tukalichukulia kama ndiyo CCM halisi bila kujali vyeo vyao ndani ya chama.

nauliza hivyo kutokana na kuchanganyikiwa baada ya kusikia matamko ya watu hao ambayo yamenixcha nikiwa kama kichaa bila kujua nichukue la nani.

nisaidieni jamani .

Tatizo lianzia hapo,watu wanataka wajue msemaji ili wafuate kauli zake.Chamsingi watakiwa upime pumba zao,za nani zimeziidi uzito ili uamue mwenyewe,maana hata watu wakisema kingunge ndio msemaji,na wakati huo huo yawezekana katka hilo alilozungumza alitoa pumba,itakuwaje????
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom