Nani ana habari za kabila hili la watembea uchi

Kabila la Bodi nchini Ethiopia.
Wanaume huwa wana kipindi cha kushindana nani ni handsome kuliko wote. U handsome hutafasiriwa kwa unene ma kitambi. hivyo wanaume wanaoshiriki shindano hutunzwa sehemu maalamu kwa muda wa miezi sita au zaidi wakila saana na kunywa zaidi maziwa na damu ili kutengeneza kitambi na mshindi ni yule atakaewazidi wenzie na hupewa nafasi ya kuchagua mwanamke katika kabila hilo.

Sio wote wanakuwa na matumbo hayo ni wale wanaoshiriki shindano na ni vijana ambao hawajaoa na hutunzwa na wanawake vijijini humo kwa kuwaletea vyakula ambavyo ni asali, damu na maziwa.
 
kumbe woote ni wanaume, basi wewe husemi kweli labda ni vichaa! walizaanaje km wote ni madume km hivi
Akili zako ni fupi sana kiasi kwamba huwezi kuelewa baadhi ya hoja hata zikiwa za kawadia soma upya mada kisha jibu tena sio unakurupuka tu kuna wakati sio lazima uweke mahali maoni yako
 
1. Kuvaa nguo ni matokeo ya dhambi

2. Adam na Eva walijiona wako uchi tuu baada ya kutenda dhambi,hivyo kama hutendi dhambi nguo haina maana yoyote kwako

3. Ona Ndege wenye rangi nzuuri kama tausi,chiriku, ona pundamlia,twiga, mbwa na paka hasa hasa vikizaliwa vikiwa vidogo vinavyovutia wote wale wapo uchi lakini hatujawahi kufikiri kama wapo uchi na tunatamani hata tuwashike, wale hawatendi dhambi na ndio neema ya kukikingwa dhambi ya asili ambayo Babu zetu Adam na Eva waliitenda

4. Wamasai, watindiga na wabarbaigi hawavai nguo lakini wanaishi kwa amani

5. Asili ya waafrika wote walikuwa hawavai nguo na hizi nguo zimeletwa kama tamaduni za waarabu na wazungu waliokuja na dini na kutulazimisha tubebe dini pamoja na mila na desturi zao

6. Huwa ninapinga vikali baadhi ya watu kwa imani zao walizolishwa na wakoloni kuwalazimisha watu wengine wavae watakavyo wao bila kujali yule mtu ana imani tofauti na yeye.
Hata mimi sivai nguo, navaa kondom tu!
 
Wame’en, jamaa hawa huishi katika Bonde la Omo Kusini mwa Ethiopia na baadhi ya wanaume hutembea uchi wa nyama; wanapofika sehemu zilizostaarabika hushangaza wengi.
Kwenye bonde hilo hawapo peke yao kwani kuna makabila mengine mengi madogomadogo arobaini na tano lakini kwa mila na tabia wanafanana na Wabodi japokuwa hao wengine hawana tabia ya kipekee ya Wabodi ya kujinenepesha kwa sababu maalum kama tutakavyoona mbele.
Arbore ni moja ya kabila linaloishi katika Bonde la Omo na linalofanana kwa baadhi ya tabia na Wabodi kwani hawa nao huishi katika bonde hilo na ni majirani na makabila mengine mengi kama tutakavyoona.
Waarbore nao kama walivyo wenzao, ni wakulima wafugaji ambao hufuga ng’ombe na mbuzi.
Tofauti yao na Wabodi ni kwamba hawa hupendelea kucheza ngoma na kuimba nyimbo za kienyeji wakiamini kwamba kwa kufanya hivyo, wanatukuza mila na desturi zao, hivyo imani yao ni kwamba kitendo hicho huwaongezea utajiri wao ambao ni kuwa na idadi kubwa ya ng’ombe na mbuzi wanaowafuga.
Wanawake wa kabila la Waarbore ni tofauti na Wabodi kwani hawa hufunika vichwa vyao kwa kutumia nguo nyeusi na huvaa shanga za rangi tofauti shingoni pia kwenye masikio yao huweka hereni maalum kwa ajili ya kujiremba wakati wanawake wa Wabodi wao hunyoa vipara au ‘viduku’.
Licha ya kuwa wafugaji Wabodi ni wakulima na mazao yao huyalima katika miteremko ya udongo uliotokana na milipuko ya volcano.
Lakini Wabodi mara nyingi wengi wao wake kwa waume na watoto, hawapendelei kufuga nywele na badala yake hupendelea kunyoa kwa mitindo mbalimbali ambayo vijana wa leo hapa nchini wamekuwa wakinyoa, ‘kiduku’.
Unyoaji huo hufanywa hata kwa watoto wadogo wanaobebwa mgongoni na hauchagui jinsia.
Watoto wao wengi hunyolewa viduku na hata wasichana hunyoa mitindo hiyo na bila shaka mtindo huo ulienea hadi Ulaya ambapo sasa tunaona jinsi hata wachezaji wa mpira wa miguu wakubwa huko wanavyouiga.
Kutokana na utamaduni huo kuenea duniani ni wazi kwamba bila shaka waanzilishi wa mtindo huo ni Wabodi kwa sababu wao wamekuwa wakinyoa hivyo enzi kwa enzi.
Wengi wa wenyeji hawa wana miili midogo na siyo wanene, hivyo basi wale wanaume wenye umbo kubwa na vitambi hupendwa na wanawake wa huko kuliko wanaume wembamba.
Lakini ili kupata umbo kubwa na vitambi kuna kazi kubwa hufanyika kwani kuna mbinu ambayo hutumika na ni ya gharama kubwa kwa wanaohitaji kuwa na kitambi kikubwa.
Kuna wakati vijana hushindanishwa ili kuwa na umbo kubwa na vitambi vikubwa vilivyochongoka kwa mbele.
Zamani mshindi alikuwa anapewa zawadi ya ng’ombe au mbuzi lakini siku hizi zawadi zimeongezwa kwani mshindi hupewa pia kombe ambalo ni tuzo kwa kushinda kutokana na kujinenepesha na kuwa na kitambi kikubwa kuliko washindani wenzake.
Mara nyingi vijana wa kiume ndiyo hushirikishwa kwenye kuwania ubingwa wa kitambi na wahusika huweza kushinda baada ya kukaa kambini kwa miezi wakila vyakula ambavyo siyo vya kawaida lakini hawana budi kufanya hivyo ili kuwa wanene.
 
duhh na bahati mbaya sana hata jando wanalisikia tu! weusii wako sudan? au mali?
 
Elimu nnuufunguo wa Maisha
IMG-20191115-WA0000.jpeg
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom